Umeme Maporomoko ya Rusumo Wafikia Asilimia 99.9

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kuwa, mradi wa maporomoko ya umeme wa Rusumo wa megawati 80 unaotekelezwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi umefikia asilimia 99.9 na nchi hizo tayari zimeanza kupata umeme kutoka kwenye mradi huo.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Disemba 18, 2023 jijini Mwanza wakati akiongoza kikao cha ngazi ya Mawaziri wa Nishati ambaye yeye ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa wanaosimamia mradi huo kutoka nchi hizo tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.

"Tumeridhishwa na maendeleo mazuri ya mradi mpaka sasa, tunawapongeza Bodi na Watendaji kutoka kampuni ya umeme ya Rusumo na wakandarasi kwa usimamizi na utekelezaji wa mradi huu," amesema Dk Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amesema Mawaziri hao wamekubaliana kuwa, mradi huo uzinduliwe mwezi Machi, 2024 hivyo wamemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo mapema na atoe cheti cha kukamilisha mradi. Amesema uzinduzi huo utafanyika katika eneo la mradi huku mwenyeji wa shughuli hiyo akiwa ni Tanzania.

Pia, amesema kuwa, mradi huo una umuhimu kwa nchi zote tatu kwani bado nchi hizo zina changamoto ya upatikanaji wa uhakika wa umeme hivyo kukamilika kwa mradi huo kutapunguza changamoto hizo na kuongeza uimara kwenye gridi.

Vilevile, Dk Biteko ameshukuru wadau mbalimbali waliopelekea mradi huo kutekelezwa ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na amewakaribisha kuwekeza kwenye miradi mingine ya uzalishaji umeme inayotarajiwa kutekelezwa nchini.

Chanzo Habari Leo
 
-
Dk Biteko amesema hayo leo Disemba 18, 2023 jijini Mwanza wakati akiongoza kikao cha ngazi ya Mawaziri wa Nishati ambaye yeye ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa wanaosimamia mradi huo kutoka nchi hizo tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.
-
"Tumeridhishwa na maendeleo mazuri ya mradi mpaka sasa, tunawapongeza Bodi na Watendaji kutoka kampuni ya umeme ya Rusumo na wakandarasi kwa usimamizi na utekelezaji wa mradi huu," amesema Dk Biteko
-
Aidha, Dk Biteko amesema Mawaziri hao wamekubaliana kuwa, mradi huo uzinduliwe mwezi Machi, 2024 hivyo wamemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo mapema na atoe cheti cha kukamilisha mradi. Amesema uzinduzi huo utafanyika katika eneo la mradi huku mwenyeji wa shughuli hiyo akiwa ni Tanzania.
-
Pia, amesema kuwa, mradi huo una umuhimu kwa nchi zote tatu kwani bado nchi hizo zina changamoto ya upatikanaji wa uhakika wa umeme hivyo kukamilika kwa mradi huo kutapunguza changamoto hizo na kuongeza uimara kwenye gridi.
-
Vilevile, Dk Biteko ameshukuru wadau mbalimbali waliopelekea mradi huo kutekelezwa ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na amewakaribisha kuwekeza kwenye miradi mingine ya uzalishaji umeme inayotarajiwa kutekelezwa nchini.
-
Chanzo Habari Leo

View: https://www.instagram.com/p/C0_ojdXtVLD/?img_index=1

Mimi hawa wazee wa megawati za Tanzania kufikia mwaka fyokofyoko itauza umeme nje ya nchi, wala siwaelewi..!! Mpaka nione ndo ntaamini..!!
 
sasa kwa tanzania tumekuwa master kwa miradi ya us billions dollr sasa ni wakati wa kuwekeza kwenye kinu cha nyuklia kwa ajili ya umeme mkubwa kabisa.
 
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kuwa, mradi wa maporomoko ya umeme wa Rusumo wa megawati 80 unaotekelezwa kwa pamoja na nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi umefikia asilimia 99.9 na nchi hizo tayari zimeanza kupata umeme kutoka kwenye mradi huo.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Disemba 18, 2023 jijini Mwanza wakati akiongoza kikao cha ngazi ya Mawaziri wa Nishati ambaye yeye ni Mwenyekiti wa Mawaziri wa wanaosimamia mradi huo kutoka nchi hizo tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.

"Tumeridhishwa na maendeleo mazuri ya mradi mpaka sasa, tunawapongeza Bodi na Watendaji kutoka kampuni ya umeme ya Rusumo na wakandarasi kwa usimamizi na utekelezaji wa mradi huu," amesema Dk Biteko

Aidha, Dkt. Biteko amesema Mawaziri hao wamekubaliana kuwa, mradi huo uzinduliwe mwezi Machi, 2024 hivyo wamemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo mapema na atoe cheti cha kukamilisha mradi. Amesema uzinduzi huo utafanyika katika eneo la mradi huku mwenyeji wa shughuli hiyo akiwa ni Tanzania.

Pia, amesema kuwa, mradi huo una umuhimu kwa nchi zote tatu kwani bado nchi hizo zina changamoto ya upatikanaji wa uhakika wa umeme hivyo kukamilika kwa mradi huo kutapunguza changamoto hizo na kuongeza uimara kwenye gridi.

Vilevile, Dk Biteko ameshukuru wadau mbalimbali waliopelekea mradi huo kutekelezwa ikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na amewakaribisha kuwekeza kwenye miradi mingine ya uzalishaji umeme inayotarajiwa kutekelezwa nchini.

Chanzo Habari Leo
Ni vizuri ila mimi naamini ikiwa nchi haipigi vita ufisadi na vigogo wameambiwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba umeme itaendelea kua hadithi. Kila kigogo serikali kwa sasa anafanya biashara kuuza au kuhujumu huduma za umma na mali za umma kwa maslahi yake binafsi. Cheo chake amegeuza mtaji huku hajawekeza kitu. Mkanganyiko kati ya maslahi binafsi na yale ya umma ndio vinafanya hata umeme wa gesi unaotumika sana sasa na ule wa bwawa la nyerere ukija iwe kazi bure. Rushwa na hujuma vitatawala ila tu kama 2025 nchi itapata magufuli mpya. Mtu muadilifu mwenye akili na maono na asiye na masihara na ufisadi ndio anahitajika kuongoza taifa.
 
Back
Top Bottom