Benki ya Dunia: Toleo la 15 la Ripoti ya Hali ya Kiuchumi ya Tanzania

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,101
2,000
Benki ya Dunia inatarajia kufanya uzinduzi wa Toleo la 15 la Ripoti ya Hali ya Kiuchumi ya Tanzania “Tanzania Economic Update” kesho tarehe 3 Machi, 2021.

691E8995-1D6A-47DE-8F9F-7C8647CF3815.jpeg


Ripoti hii ya uchambuzi huru wa Benki ya Dunia inaangazia changamoto, mafanikio ya kiuchumi, hali ya umasikini, vipato, rasilimali watu n.k

Vilevile inaangazia kila sekta na namna ilivyochangia pato la taifa na ukuaji wake.

Katika ripoti ya mwaka huu jambo kuu lililojadiliwa ni Tanzania kuingia katika nchi za uchumi wa kati wa chini (LMIC) na namna tunaweza kubaki hapo katika siku zijazo.

UPDATE:

1) Benki ya Dunia yasema Tanzania haikuwa serious na COVID19 mwaka 2020, yatushauri kujiandaa tu kabisa na ugawaji wa chanjo

2) Ripoti ya Hali ya Uchumi Tanzania: Benki ya Dunia yapendekeza mfumo wa ncha 3 kupambana na COVID-19 na Mporomoko wa Uchumi
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,304
2,000
Hivi maana ya kuingia kwenye uchumi wa kati ni vifaa vya ujenzi kupanda, sukari, nauli n.k? toka umetangwa huu uchumi fake wa kati kwangu maisha yamekuwa magumu sn hakuna nafuu hata kidogo nimebaki kujikimu pekee sifanyi maendeleo yoyote.
 

Gilbert A Massawe

Senior Member
Feb 18, 2021
106
225
Hivi maana ya kuingia kwenye uchumi wa kati ni vifaa vya ujenzi kupanda, sukari, nauli n.k? toka umetangwa huu uchumi fake wa kati kwangu maisha yamekuwa magumu sn hakuna nafuu hata kidogo nimebaki kujikimu pekee sifanyi maendeleo yoyote.
Njoo nikupe ujira ulinde shamba langu hapa kibiti bwashe..
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
52,597
2,000
Inabidi wamshauri rais wao na wamwambie ukweli kuwa anavyoIdi kukataa chanjo sio kwamba ni ujanja.
Ni upumbavu na nchi utatumbukia shimboni.
Kuna biashara hasa za utalii anajua kabisa fika umuhimu wa utalii.
Amenunia mindege ila akiendelea kukataa chanjo haki ya nani ile mindege ataenda kulala nayo chato.

Mshaurini huyu mzee.
Kwanza inasemekana ameshachanja
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,113
2,000
Time wastage. There won't be any credible statistics.

Kila mwenye akili timamu anajua. Zitachongwa chongwa na kupakwa polish ili kumfurahisha Korosho.

- Utasikia kuna ongezeko la ajira kwa 15%🤣

- Pato la Mtanzania limeendelea kukua vizuri kwa wastani wa asilimia 14.

- Umasikini unaendelea kupungua siku hadi siku 🤣

- Kutokana na kasi ya miundombinu inayojengwa, tunakadiria uchumi kukua kwa kasi zaidi ya asilimia 8 ndani ya miaka 3 ijayo.

- Madeni ya nje na ndani yanahimilika na tunaenda Vizuri sana.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,377
2,000
Hili Neno Benki ya Dunia linaweza likaonekana kubwa sana na kuipa Ripoti authenticity kubwa sana..., ingawa kumbe ndani ni cooked Data zilizopikwa kutoka kwa mdau / wadau Tanzania wakiwa kwenye laptops zao kwa kuchanganya nadharia na assumptions za kutosha...
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,450
2,000
Hivi kushuka kwa kupungua umasikini, yaani, umasikini kuongezeka ni matokeo ya COVID-19 pekee au inachangiwa na sera za 'ukapa' kwa sababu hakukuwa na lockdown? Kwa kipimo cha kimataifa, asilimia 50 ni masikini, serikali ipo wapi?
 

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
771
1,000
Hili Neno Benki ya Dunia linaweza likaonekana kubwa sana na kuipa Ripoti authenticity kubwa sana..., ingawa kumbe ndani ni cooked Data zilizopikwa kutoka kwa mdau / wadau Tanzania wakiwa kwenye laptops zao kwa kuchanganya nadharia na assumptions za kutosha...

Mbona huna imani hata kidogo mkuu? Wamekukosea nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom