Benki ya Dunia kutoa dola za Kimarekani Mil 425, kuboresha Elimu ya Juu Tanzania ili kuleta Mabadiliko ya Kiuchumi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,982
Salaam Wakuu,

Benki ya Dunia inatazamia kutoa Dola za Kimarekani Milioni 425 katika mpango wa miaka mitano wa uboreshaji wa elimu ya juu ili kwendana na Mabadiliko ya Kiuchumi

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inaandaa mpango wa miaka mitano wa uboreshaji wa elimu ya juu, mradi wa “Higher Education for Economic Transformation (HEET) project”, Lengo la maendeleo ya mradi huo ni kuimarisha mazingira ya kujifunzia na upatanisho wa soko la ajira ya mipango ya vipaumbele katika vyuo vikuu vya walengwa na kuboresha usimamizi wa mfumo wa elimu ya juu.

Mradi utawekeza katika miundombinu inayohitajika kwa ufundishaji na utafiti wa kisasa, na kutoa mafunzo kwa kiwango cha juu zaidi kwa Walimu, watafiti na wasimamizi wanaohitajika kwenye vyuo Vikuu.

Mradi wa HEET umekusudiwa kufikia malengo ya kimkakati kama ifuatayo;

(i) Kuongeza uandikishaji katika taaluma za kipaumbele,

(ii) Kuboresha umuhimu na ubora wa programu katika vyuo vikuu ili kukidhi hali na viwango vya soko la ajira la sasa na la baadaye,

(iii) Kuimarisha uratibu wa kiwango cha mfumo, usimamizi wa ubora wa elimu ya juu nchini Tanzania, na

(iv) Kuongeza kiwango cha ajira kwa wahitimu kupitia kuboresha mitaala na kuunda programu mpya zinazoendeshwa kulingana na mahitaji.

1610550703082.png

Katibu Mkuu wa Elimu,Sayansi Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akizungumza katika kikao cha wadau kujadili rasimu ya miongozo ya usalama wa mazingira na jamii katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya juu wa mabadiliko ya kiuchumi (HEET) nchini kilichofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dr Leonard Akwilapo akiongea na Wadau wakati wa kujadili rasimu ya miongozo katika utekelezaji wa mradi wa kiboresha elimu ya Juu wa Mabadiliko ya kiuchumi (HEET), amesema Malengo ya Mradi huu ni;

i) Kuongeza rasilimani watu

ii) Kuongeza vifaa vya maabala na Vifaa vya kufundishia

iii) Kuhuwisha Mitaala ili kuendana na Mapinduzi ya nne ya Viwanda

iv) Kuongeza Udahili wa Wanafunzi wa Ndani ya nchi na Kuongeza Udahili wa Wanafunzi wa Kimataifa katika vyuo vyetu vya Nchini

v) Kuimalisha mfumo wa Malezi ya Wanafunzi wa vyuoni na kuwapa stadi ya Maisha ili kupata wahitimu wenye maadili na Uzalendo.

vi) Kusomesha Wanataaluma katika ngazi ya Uzamili 639

vii) Mradi huu Unatarajiwa kuborehsa mitaala 290

viii) Miundombinu ya Barabara, Majengo, Maji, Umeme itaboreshwa katika Vyuo 14 vya Umma.

ix) Mradi huu utawezesha Wataalam wanakuwa na ujuzi wa kujiajiri na kuajirika katika kujenga uchumi wa kisasa.

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dr Leonard Akwilapo amewataka wadau wote kutoa maoni kabla ya miongozo hiyo kuwasilishwa kwa kiwango kingine ili kuboresha na kuhakikisha wanafikia Malengo haya ya miaka Mitano
 
Pesa za ndani zimeisha?

Dona kantri, pesa za ndani, sijui mavi gani huku chini kwa chini watu wanalamba mabeberu makalio.
 
Kwa hiyo mtaondoa madeni ya kubambika plus retention fee kwenye elimu ya wanyonge?
 
Kuongoza nchi kwa uwoga wa kunyimwa misaada, ni kuwaruhusu wahuni Baadhi ya watu wa Chadema na wapinzani uchwara kuchezea sharubu za Raisi,

JPM, nchi inakutazama wewe! Ukiweza Sana na Tanzania inaweza Sana!!
 
Hiyo pesa ni msaada au mkopo, kama ni msaada ikiingizea kwenye mikopo ya wanafunzi serikali itakuwa wezi, haiwezekani wanafunzi waje kulipishwa kwa riba.
 
Uwekezaji zaidi wa fedha hizi tushawshi ulenge zaidi kwenye tafiti za sayansi na teknolojia kulingana na hadhi ya uchumi wetu kwa sasa kipindi hiki cha mageuzi"socio ec transformation" hususani kilimo na viwanda
 
Back
Top Bottom