Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Wataalam tusaidieni.
Hivi ukiongezwa damu ya mtu aliyechanjwa chanjo ya Covid wakati wewe hujachanja je, damu hiyo mpya haiwezi kuhamia kwenye damu yako na chanjo ile kwamba huna haja ya kuchanja tena?
Kwa kuwa sayansi ya tiba iko kimya kwenye hilo, najaribu kujifikirisha kwamba endapo atatokea mtu aliye kinyume na chanjo hizi akaamua kutumia gap hiyo ya sayansi kutotoa jibu kwa shaka hili; kukampeni kwa watu kutilia shaka utoaji na uongezwaji damu kwamba mtu asiyetaka kuchanja ataogopa kuongezwa damu ya mtu aliyechanja na kwamba huenda tukajikuta kwamba ama Benki ya Damu inaingia kwenye ukata mkubwa wa damu au inakuwa na akiba kubwa ya damu yenye chanjo tu, ingawa hivi sasa uchunguzi usiyo rasmi unaonyesha kwamba wale walio kinyume na chanjo wamezama kwenye mfumo mpya wa utamaduni wa ulaji ambapo wanakula sana vyakula vya kuongeza damu (pamoja na kujikinga) ili wasije kuwa na uhitaji wa kuongezwa damu na kujikuta wakiongezwa damu ya mtu aliyechanja pale itapobidi damu kuongezwa, na huu ndiyo msingi wa mada yangu hii kama inavyojifafanua kwenye aya ya kwanza hapo juu.
Maswali magumu:
1. Je, Benki ya Damu itahitaji kubagua aina za damu inazokusanya katika makundi mawili ya waliochanja na wasiochanja?
2. Je, wakati sayansitiba bado iko kimya kuhusu shaka hili; ni haki kumuongeza mgonjwa damu yenye chanjo ilhali yeye hataki chanjo? Siyo uvunjifu wa #haki-za-mgonjwa/binadamu?
3. Je, kuna utafiti wowote umefanyika au unaendelea kufanyika kuhusu jambo hili? Kama upo majibu ya awali ya utafiti huo ni nini?
4. Je, kama ukiongezwa damu ya mtu aliye na Covid nawe unapata virusi hivyo (kama ulivyo Ukimwi), na kwa kuwa chanjo ni virusi vilivyofubazwa/punguzwa nguvu vinaingizwa kwenye damu ya mtu aishi navyo milele, vipi chanjo (virusi hivyo vilivyofubazwa) visiingie na kufanyakazi kwenye damu ya mtu aliyeongezwa ambaye hakuwahi kuchanjwa?
5. Je, kuna itifaki yoyote ya tiba ya dharura (Emergency Medical Protocol) kuhusu haki-za-mgonjwa kuongezwa damu katika mazingira kama haya?
6. Kama ni kweli kwamba ukiongezwa damu ya mtu aliyechanja na wewe usiyechanja unapokea chanjo hiyo kupitia damu uliyoongezwa je, hapa #Hiari-ya-kuchanja iko wapi? Siyo kwamba wote tunajikuta tumechanjwa kwa lazima?
7. Je, ukiongezwa damu ya mtu aliyechanjwa wakati wewe hujachanja na kwamba damu hiyo mpya imekupa chanjo automatically kupitia damu uliyoongezwa, vipi kwanini usipewe cheti cha chanjo kwa kuwa damu yako imeishapokea chanjo kupitia kuongezwa damu ya mtu aliyechanjwa na kwamba huhitaji kuzuiliwa mpakani unaposafiri wala kubaguliwa kwenye kupata huduma zozote zile?
Hakuna swali la kijinga duniani ila majibu ndiyo yanaweza kuwa ya kijinga. (No question is stupid but the answer)