Benki Kuu (BoT), yasitisha leseni za maduka ya kubadilishia fedha za kigeni Tanzania

Uchumi wa nchi ya kusadikika kamwe hautakuzwa kwa vitisho na mabavu, mala wajeda!!! Bali ni mikakati madhubuti na mipango mizuri!!!
 
Akiongea na wanahabari jijini Arusha,Gavana Prof.Luoga ameeleza kuwa sababu ya kutumia wanajeshi ni kuwa Polisi walikuwa kwenye usimamizi wa mitihani ya form two. Ameongeza kuwa wanajeshi hawakuwa na silaha

BBC imerushwa taarifa hiyo katika matangazo ya idhaa ya Kiswahili.
 
Naamini Askari JWTZ waliohusika katika operesheni huko nchini Tanzania wakishirikiana na BOT hawazidi hamsini, Je ikitokea maandamano polisi wanakosa Askari hamsini?

Kwa kuwa ni operesheni na inaendeshwa na msimamizi mkuu wa uchumi wetu, Je, kwanini gavana hakuona ni busara kuchukua askari polisi waadilifu mikoa na maeneo tofauti na kuwalipa gharama zao za safari ambazo naamini hazizidi milioni kumi wakafanya hiyo operesheni kuliko kutumia Jeshi na kuzua taaruki kimataifa na pia kuwapeperusha wawekezaji na watalii?
 
Km ww ni mtali au muwezaj unatakiwa kufuata mashart ya nch,sio kwa kuwa ww ni mtali au nan ndio uvunje sheria za nch.
 
Jeshi limeanza kutumika kwenye mambo ya hovyo.

Kwamujibu wa katiba: -
i/Jeshi linawajibu wa kulinda mipaka ya nchi.
ii/ kulinda & kuitetea katiba ya nchi.
Sasa hayo mambo ya sijui kukusanya korosho, sijui kuimarisha ulinzi kwenye 'Bureau de change' sijui yanatoka wapi.
 
Sasa hivi jwtz tutaliona kama mgambo...
Huyu profeseri ndo anatoa haya maneno. Inamaana now arusha hakuna usalama kwamba polisi wote wako kwenye mitihani?? si mchezo...tulipofikia pabaya.
 
Hahaha tunachotakiwa kushukuru ni kwamba angalau wanajisumbua kujibu. Hapo haijalishi tunadanganywa au ni kweli
 
Nimesikitika sana.. Kudanganya mchna kweupe.. Ina maana jiji LA arusha lina maduka mengi ya kubadilisha pesa hadi polisi hawatoshi... Ina maana mitihani ikianza police woote wanaenda kusimamia!???
 
Sasa hivi jwtz tutaliona kama mgambo...
Huyu profeseri ndo anatoa haya maneno. Inamaana now arusha hakuna usalama kwamba polisi wote wako kwenye mitihani?? si mchezo...tulipofikia pabaya.
Arusha ukipita barabarani kila baada ya mita 200 utakuta polisi wa usalama barabarani zaidi ya kumi.
Leo tuna aminishwa polisi walikuwa kwenye mitihani.
Kwanini trafiki hawakutumiwa kwa zoezi la BoT??
Nakumbuka zama za JK alikuwa anatumia wana funzi wa chuo cha polisi Moshi.
Leo kubeba na kulinda magodown ya korosho ni Jw, kulinda ukuta wa Mererani ni Jw. BoT nao kulinda maduka ya kubadilisha pesa ni Jw, kazi inayo fanywa na mgambo na virungu.. Jamaniiii
Sidhani kama jeshi letu linatumika sawa..
Something wrong some where...
 
Jeshi limeanza kutumika kwenye mambo ya hovyo.

Kwamujibu wa katiba: -
i/Jeshi linawajibu wa kulinda mipaka ya nchi.
ii/ kulinda & kuitetea katiba ya nchi.
Sasa hayo mambo ya sijui kukusanya korosho, sijui kuimarisha ulinzi kwenye 'Bureau de change' sijui yanatoka wapi.
fear of the unknown, kwa mujibu wa Sumaye
 
Hapo zamani kulikuwa na Ze Comedy, walipoonekana mwiba wakanunuliwa na kupelekwa ile TV ya Chama kikuu kisichopendwa, kisha ikajibadili jina na kujiita Original Komedi. Hapa ndipo usanii ulipoanzia. Kila kitu nchini kikawa "komedized". Kwa mleta mada hii ya Arusha kukosa askari Polisi 24(Siyo 50 kama ulivyodhani) ni Komedi tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom