Benjamin William Mkapa: Shujaa, Mzalendo, Muumini wa Utandawazi

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Nimepokea kwa masikitiko sana taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Ndugu Benjamin Mkapa. Kifo chake kimegusa moyo wangu na ninaamini kabisa kwamba kimegusa mioyo ya wengi sana.

Binafsi nimemfahamu Marehemu Mzee Mkapa kwa muda mfupi sana na katika kipindi kifupi nilichomfahmu amenijenga sana hasa katika misingi ya uongozi, maendeleo na ujenzi wa jamii. Mzee Mkapa katika uhai wake amekuwa ni mtu aliyeishi kwa kusema, kufanya na kusimamia kile alicho amini kwa maslahi mapana ya nchi.

Mbobezi huyu wa Diplomasia na siasa za Utandawazi ni mmoja wa waasisi wa Mabadiliko mengi sana katika Taifa letu. Amejijenge heshima nchini na nje ya dunia kutokana na umahiri wake wa kutetea kile alicho amini na kukisimamia.

Mzee Mkapa alikuwa ni mtu wa misimamo lakini mwenye kiwango kikubwa cha unyenyekevu. Hakuogopa kuonekana mbaya hasa pale ambapo aliamini kwamba kile alichosimamia ni sahihi na ni kwa maslahi mapana ya nchi. Alikuwa na ujasiri wa kukemea na kushauri pale inapobidi.

Mzee Mkapa ni Muasisi wa Tanzania mpya ambayo bado inajengwa. Alisimamia mageuzi makubwa sana katika uchumi wetu ikiwamo sekta ya fedha, uchumi na uwekezaji. Aliasisi sera ya ubinafsishaji na kuisimamia kwa udhabiti kwa kadiri ya uwezo wake. Alikuwa ni muumini wa Utandawazi na aliheshimika duniani kwa misimamo na mitazamo yake.

Mzee Mkapa ameendelea kuwa mshauri na mtetezi wa maslahi mapana ya nchi yetu na kwa hakika aliishi maisha ya mfano kwa uzalendo na utumishi.

PUMZIKA KWA AMANI MZEE WETU BEN MKAPA
 
Mbobezi huyu wa Diplomasia na siasa za Utandawazi ni mmoja wa waasisi wa Mabadiliko mengi sana katika Taifa letu. Amejijenge heshima nchini na nje ya dunia kutokana na umahiri wake wa kutetea kile alicho amini na kukisimamia.
Ninakubaliana na haya uliyoandika hapa.

Alikuwa ni kiongozi mwenye kuheshimika hata nje ya mipaka ya nchi yetu.

Alikuwa na uwezo wa kuelewa na kuelezea mambo aliyoyajua na kuwa na msimamo juu yake na watu wengine wakamwelewa.

Hakuwa na tabia ya kinafiki, kujifanya anakubaliana na jambo fulani hadharani akirudi faragha anasema mengine.
 
Masikitiko yangu ni kuwa amekufa kabla hajarudisha ile Ikilu ndogo ya Lushoto aliyolipoka Taifa.

Ile nyumba Ina historia ndefu sana katika Ukoloni. Baada ya Wajerumani kushindwa WWI Uingereza ikawa rasmi mtawala wa East Africa yote kuanzia Kenya, Uganda na Tanganyika. Wajerumani waliazimia kulirudisha koloni la Tanganyika kwenye himaya yao na waliazimia kumcharaza Mfalme Gerge VI vibaya sana.

Wakati wa WWII, Wajerumani walijua Kenya ndiyo moyo wa Mfalme Gerge ulipo katika Africa na alipanga kujificha huko. Intelljensia za Waingereza zilipojua hilo ziliamua kumjengea King George maficho kwenye milima ya Lushoto.

Katika ziara za kikazi Mkapa akiwa Rais alifikia Ikulu ndogo ya Lushoto na aliipenda sana. Baada ya hapo alifanya hila zote kujimilikisha Ikulu ile.

Mkapa hakuwa mzalendo, alikuwa mbinafsi mno.
 
Sina Cha kuongeza hapo umegusa nilivyokuwa nayo kwangu.
R.I.P shujaa mh.william b.mkapa hakika:shujaa ameumaliza mwendo
 
Pia alikuwa mtu katili na mkandamizaji.
Tusiwe wanafiki, tuseme yote.
Mkuu nilikuwa natafuta atakayesema kinyume na waliotoa maoni yao hapo juu.

Binadamu tu wanafiki balaa. Huyu ndiye tuliyemlaumu na sera yake ya uwekezaji tukasema kauza viwanda na mashamba kwa mabepari na hatuoni faida.

Leo tunamsifu kwa 100% alikuwa mwadilifu na mwenye heshima kwa watu. Mengine tumesahau. Dunia simama nishuke, wanadamu siwawezi.
 
*Marehemu hasemwi*

Kuna Malaika huwa wapo kwa ajili ya kuitikia kila baya na zuri la marehemu na kumuandikia.

Mfano..

1. Huyu jamaa alikuwa Mwizi sana..Amin apewe anachostahili kwa wizi wake.

2. Huyu alikuwa na huruma sana..
Amen, apewe anachostahili kwa huruma yake.

Mwisho wa yote inamuongezea ktk mafurushi ya malipo yake huko aendako.

Tusemane kabla ya kufa ili tujirekebishe mapema...

Ingawa ukisemwa pia baada ya kufa kuna mawili, yule mwenye kujawa na hofu na kubadirika na yule mwenye kusema lolote liwe kwani si nitakuwa nimeshakufa.
 
Pamoja na hayo yote lkn pia yapo mazuri ya kukumbukwa. Ktk kipindi chake ndo kipindi kilichoibua vyombo vya habari vingi kuanzishwa uhuru na utawazi. Lakini pia ndo kizingiti pekee tulichokuwa tunakitegemea kuzuia watu kufanya yao ktk katiba yetu baada ya 2025. Maana ndo mtu anaeonekana kum mudu mwafulani.
 
Ingekuwa vizuri kila mtu akawa anaandika maovu yake yanayojulikana na yasiyojulikana ili kwamba siku akifa naye maovu yake yasomwe ili watu wajifunze.
 
Back
Top Bottom