Jeshi la mtu mmoja analilia silaha na dola za USA!?
Wewe inaonekana hujui kabisa uhusiano kati ya Israel na Marekani:
Ufahamu kuwa Marekani ni taifa pacha la Israel.
Idadi ya wayahudi waishio Marekani ni karibia sawa na idadi ya wayahudi waishio Israel.
Wayahudi waliopo Marekani, karibia wote wapo maeneo muhimu ya tekinolojia, Sayansi, uvumbuzi na uchumi.
Kuna miradi ya ushirikiano katika tekinolojia kati ya Israel na Marekani.
Ndiyo maana kinachotolewa na USA kwenda Israel, hakihesabiki kama msaada bali wajibu wa ushirikiano.
Wajibu wa kifedha wa Marekani kwa bajeti ya jeshi la Israel ni dola bilioni 3 kwa mwaka. Huo ndio wajibu pekee wa Marekani kwa Israel. Israel haipokei msaada wowote wa kiuchumi au maendeleo ya jamii toka Taifa lolote Duniani. Uchumi wa Israel ni karibia mara 6 ya uchumi wa Tanzania, na karibia mara 2 ya ule wa Iran, licha nchi ni ndogo sana, na population yao ni ndogo sana. Ukilinganisha utajiri halisi wa Israel, ni karibia mara 70 ya ule wa Tanzania.
Tanzania per capita USD 1,160
Iran per capita
USD 4,075
Israel per capita
USD 60,009
2025 Total GDP Iran bilion $356. Mwaka 2010 ilikuwa bilioni $600. Iran inaenda kaburini1
Total GDP Israel bilion $610.75. Israel mwaka 2010 ilikuwa bilioni 238.9.
NB: Israel inazidi kupaa, Iran inazidi kudidimia. Kwa mwenendo wa Iran, kama hakutakuwa na mabadiliko, uchumi wake mwaka 2035, utakuwa sawa na huu wa Tanzania kwa sasa. Hapa ndipo Ayatollah alipowafikisha.