Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Benjamin Mkapa: Nashuhudia mambo ya ajabu baada ya uongozi wangu!

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na amesikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni. Akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma, Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote.

“Katika kipindi cha uongozi wangu, viongozi wa madhehebu yote walikuwa wakinisisitizia kuwa sisi sote ni ndugu pamoja na tofauti zetu za kiimani. Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,” alisema Mkapa, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 1995-2005.

Mkapa alionya kuwa taifa limeacha misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye mara zote alisimamia umoja wa taifa.

“Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii,” alisema.

Mkapa ambaye hakupanga kuongea lolote katika tukio hilo, alitaka taifa lijenge utamaduni wa kupendana, huku akilaumu kuwa kizazi kipya cha uongozi kimeanzisha mambo ya ajabu ya kukosa upendo na kudhalilishana.

Pia alitahadharisha kuwa zama hizi kumeibuka mitafaruku mbalimbali na kuwakumbusha Watanzania kuwa ni wakati wa kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Mkapa alisema mara nyingi alishauriana na viongozi wa dini katika masuala ya kijamii na kiroho na kumtaja askofu mpya wa Bukoba, Rwoma na Mtangulizi wake aliyestaafu Nestory Timanywa kuwa alishirikiana nao katika masuala ya wananchi. Onyo la Mkapa limekuja siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kukemea mambo ya kidini na kutetea Serikali yake haiongozi kwa misingi ya ubaguzi.

Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kudai amekuwa akilalamikiwa na viongozi wa madhehebu ya Kikristo na yale ya Kiislamu.

Maneno ya Mkapa na Kikwete yamekuwa katika kipindi hiki taifa likiwa limetikiswa na matukio yenye mwelekeo wa chuki za kidini. Matukio makubwa yakiwa yale ya kuuawa wa Padri Evarist Mushi huko Zanzibar na Mchungaji Mathayo Kachila wa Geita.

Pia kupigwa risasi kwa Padre Ambrose Mkenda na kumwagiwa tindikali kwa Sheikh Fadhil Soraga na vurugu za mambo ya kuchinja huko Geita na Tunduma.

Askofu Mpya wa Bukoba Rwoma alimshukuru Mkapa kwa kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi, huku akisisitiza suala la upendo miongoni mwa wananchi.

Mkuu maneno hayo mazito sana ila tupe sosi!hata ka picha au ka clip
 
Watanzania mtanikumbuka! By Benjamin William Mkapa 2005
Nakweli tumeshamkumbuka kwa mengi,Kumbe kweli (The devil You Know is far Much Better Than an Angel you have never met)!
 
Nini maana ya mwenyekiti, yeye kama kiongozi mkuu wa chama ndiyo mwisho wa maamzi, JK kipindi kile alikuwa mtu mdogo kufanya mabadiliko maklubwa ndani ya chama, hata JK mwenyewe aliwahi kuongea na vyombo vya habari na kusema kuwa yeye mambo ya mahakama ya kadhi ameyakuta. suyo yeyey mwanzilishi wa jambo hili. au memory yako inapoteza.
Si sahihi maoni yako. Mgombea ana kauli ya kukubali au kukataa maoni yanayowekwa kwenye ilani yake. Na hata wakilazimisha anapoingia madarakani anayo haki kukataa kutekeleza na kueleza msimamao wake. Sihyo asu bili mpaka wanan hi walalmike nfiyo anatafuta sababu na kujityoa/kusukuma lawama kwa wengine.


Hata Mh Mkapa naye hawezxi kujivua lawama kwa Watanzania kwa kugtokemea au kunyamaxia mambo haya ya udini wakati Chama chake na Serkali yake vikionekana kushabikia mwanzoni mpaka mambo yamefika hapa tunapokuwa na uhasma mkubwa wa kidfini.
 
Ni upepo tu utapita.

But then again Ikulu yetu siku hizi ya makuti, ata upepo tu unaweza kuipa mauti!
 
Kipindi kile serikali ya Mwalimu Nyerere(R.I.P.) ilikuwa inawapeleka vijijini na kuwafungia huko bila ya kuruhusiwa kutoka hao unaowaita wachochezi. Unataka na serikali ya dunia ya leo ifanye vivyo hivyo?

Bila shaka serikali hii ya leo ikifanya kama ile ya Mwalimu Nyerere wewe ndiyo utakuwa wa kwanza kulalamika serikali inakandamiza uhuru wa watu kujieleza.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Je ben nae aliwafungia vijijini?
 
Wewe ambaye maisha yamekushinda na kazi hutaki kufanya unaishia kuja kulialia mitandaoni ndiye mwenye IQ kubwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Wewe ambae unakaa na kucoment mambo ambayo hujui mwelekeo wake una IQ ya kukutosha ama ni wale wale kina fastjet
 
Hivi kabisa huwa anakaa na kusema anafanya hata 1/8 ya BMW? sasa video ya nini wakati anajijua kabisa hakuna analolifanya

Kifulambate umesummarise it all.......wakati Kenyatta Jana anamwaga sera za laptop mashuleni sisi tunagombania nani achinje kitoweo,na jamaa yetu alikuwa pale full kucheka tu na kutikisa tikis a boat zake......jamaa ndio wanatuacha speed 800!
 
Watanzania mtanikumbuka! By Benjamin William Mkapa 2005

Hii kauli ni nzito nadhani haijapata mchambuzi mahiri wa kuidadavua, pengine Mkapa alikuwa anajua CCM wanatuletea Rais wa aina gani na kweli sasa tunamkumbuka, chipsi yai ilikuwa 500 mpaka anaondoka na alipoingia baba fulani we! mbona tunakoma.
 
Uko sawa kabisa nakupa big up mwanawane. Hata yeye anajua hana maneno ya kuongoza nchi. Hata ukisikia speech zake unashangaa hivi urais aliupataje?
Naanza kukumbuka kuwa ndiyo maana alikataa midahalo maana alijua uwezo wake wa ku communicate ni shallow.
Ukisikiliza maspeech na mainterview ya nje ya nchi, unaweza ukajificha kwa aibu.
Kwa hapo waTZ tulijichora.
He will be remembered as the worst president in the history of our country. Mark my words
 
Kweli hyu jamaa ni dhaifu kweli kama natafuta hivyo vitu. sasa akivipata atafanyeje atafuta hayo maneneo?
 
Kwa kweli hilo la kuuziana nyumba za serikali na genge lake la waporaji sijui alitumia akili gani,hapo alitumia ----- sio ubongo tunachataka sisi nyumba zilizouzwa zirudishwe,hilo ndio sharti la raisi ajaye kama ataweza zirudisha vinginevyo sisi vijana tutajazirudisha wenyewe baadaye
 
Kifulambate umesummarise it all.......wakati Kenyatta Jana anamwaga sera za laptop mashuleni sisi tunagombania nani achinje kitoweo,na jamaa yetu alikuwa pale full kucheka tu na kutikisa tikis a boat zake......jamaa ndio wanatuacha speed 800!
sisi tutagawa Bajaj kwa wajawazito... Yaani mjamzito anatoka na bajaj pale ndongosi moani ruvuma anapelekwa lituhi hospital ya misheni kwa bajaj, au mjamzito anatoka Namatuhi anapelekwa songea hospital kwa bajaj
 
Kwani hawaamini nini? Kwani ni uongo kuwa haya mambo yana lelewa na serikali yenyewe
 
Wewe ambaye maisha yamekushinda na kazi hutaki kufanya unaishia kuja kulialia mitandaoni ndiye mwenye IQ kubwa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Bwawa wewe mbona unamjibia huyo jamaa wewe mke wake nini? tuelewe?
 
Kukimbilia ikulu ndio matokeo yake hayo!Ikulu ni mahala patakatifu,unakimbilia ikulu kuna bishara gani pale?maneno mazito kabisa ya JKN.Ukiingia ikulu kwa kalamu utatawala kwa mabavu na mtutu!F.Sumaye
 
mkapa alifanya ovyo ila JK KIkwete kazidi......swala la udini hebu angallia mfumo wa uongozi kwenye ngazi za juu kam vite mkuu wa jeshi la polisi, mkuu wa jeshi la wananchi, mkuu wa magereza, mkuu wa Usalama wa taifa, jaji mkuu, takukuru, wizara nyeti km fedha, mambo ya ndani, ulinzi nk katika vipindi vyote vya uongozi wao then fanya comparison....lakini pia angalia hata namna ya ku-hendle matatizo ja kijamii hasa confrict za makundi tofauti ya imani katka jamii.......tukiachilia mbali mkapa lakini mzee wa Ruksa kipindi kile kulivyo zuka swala la mabucha ya the bressed animal( mzee wa meza)alilichukulia na kuli-handle vipi... mbona leo yanatokea haya Mkuu hasemi kitu mpaka matamko ya mabaraza yatoke ndo aongee.....''big fail'' mkapa au mwinyi wanakila sababu ya kusema "afadhali sisi" then mkapa ameprove asivyo kuwa mwadilifu na mwaminifu kwa watanzania wakati ule wa kampeni za alumeru mashariki, hii ni kwasababu wengi wa viongozi wetu sio wakweli na wafuata mikumbo kwasababu ya njaa zao wasijali uwezo wa mtu bali kubaki wakitetea vyama vyao vinavyo wapa ulaji na vinavyo walinda baada ya kutoka madarakani kwa udhalimu na ufisadi walioufanya... kwanini wasiige nchi za wenzetu kama USA, tukampa mtu anaeweza na sio kwa mapenzi ya chama fulani? KUNA TATIZO tena kubwa..... kwakweli wote hamna cha maana walichokifanya kwa mstakabali wa nchi, ila '''''''kati ya hawa wawili (ndugu wanachi' na mzee wa safari) bora 'NDUGU WANANCHI" hata ukienda kwenye ward ya vichaa kuna mjanja wao........
 
Huyu jamaa ni mr clean kweli maana kuna majizi mengine yamekamatwa red handed lakini mpaka leo hayataki kukubali. Huyu alivyobanwa kuhusu kiwira alikubali na akaomba radhi kisha akaurudisha mgodi kwa serikali. Hongera mr clean kama una vijisent kule uswis sio mbaya ukiturudishia. Mungu akubariki sanaaaa. wote semeni ameen

unasifia ufisad, upumbavu, ulafi na roho mbaya bila ata HAYA!
 
Kwakweli hapa sijaona point ilipo, hizi ni zile mind zina discus watu,mtanisaidia vile zinaitwa.
Sasa kma yey Ndug wananch ameliona/ameyaona hayo, amechukua hatua gani kukemea/kukomesha hayo?
Huyu jamaa wa kiwira naona kama hana tofaut sna na jamaa wa fake smile.
Kwakua kma ameliona tatizo, basi angechukua hatua za kujitahdi kurekebisha hlo, sidhani kama anaweza kutoa tamko na huyo the traveller akapinga, so naona kama wote ni walewale tu, sema the traveler yupo some miles ahead.
Badala yke anatumia makanisa kujisafisha bdala ya kucheki namna ya ku rescue taifa?
Inatia hasira sna,wacha nitafte panado ntarejea
 
Back
Top Bottom