Mr. Bigman
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 2,560
- 1,299
Tangu jana kuna habari inanitatiza kwamba Tanzania yamlilia Gaddafi, nashindwa kuelewa hivi huyu Membe akitoa ya moyoni mwake kuhusu kifo cha Gaddafi anawakilisha watanzania wote? Hivi huyo Gaddafi ametusaidia nini watanzania mpaka tumlilie. Huyu Membe na viongozi waseme wao ndio wanamlialia. Mbona hao walibya zaidi ya Elfu 50, walio uliwa kwa amri yake sio binadamu, na wale watanzania walio uliwa na wanajeshi wa Gaddafi pale Kagera akimsaidia Dictator mwenzake Idd Amini vipi au viongozi wetu wamesahau au hawakujua wala kusikia. Jamani viongozi wetu waache unafiki.
Huyu Membe naye tayari ameshakuwa Gamba,achilia mbali Joka la Mdimu