Vipi hapo Upanga ubalozi wa Libya bendera inapepea nusu mlingoti?
Kama wataona hiyo bendera ya ccm pekee ikipeperushwa nusu mlingoti haitoshi, washushe na ya Bakwata (kama wanayo) maana huyu jamaa mchango wake mkubwa katika nchi hii ni ujenzi wa misikiti.Kama wanahamu ya kushusha bendera nusu mlingoti si washushe ya CCM? Wakishusha ya ccm wala hakuna atakae uliza maswali.
Mirembe panakufaa sana tu.Kufuatia kifo cha Dictator Gaddafi serikali kupitia Waziri Membe itapeperusha bendera ya nchi nusu mlingoti. Hili jambo linanichanganya kidogo, ni kwa heshima gani aliyostahili Gaddafi kupewa hadi bendera ipepee nusu milngoti? Dunia nzima inajua kwamba Gaddafi alikuwa Dictator amehusika na mauaji ya watu kama siyo halaiki tena kwa kiburi tu.
Gaddafi huyo huyo alishirikiana na Dictator wa Uganda Amini kuvamia nchi yetu na Watanzania wengi waliuawa, sasa hapa kuna umuhimu gani wa serikali ya Tanzania kupeperusha bendera nusu mlingoti? Mbona wakati IDD AMINI alipokufa Tanzania hatukupeperusha bendera nusu mlingoti?
Inamaana ile misaada yake ya kujenga Miskit ndiyo imetufanya tuchukue maamuzi hayo? Kwa maana nyingine ni kwamba hata IDD AMINI kabla hajafa angejenga shule au Kanisa hapa Tanzania, siku ya kifo chake ingepeperusha bendera nusu mlingoti?
Kama ni suala la IMANI lingeachiwa viongozi wa dini ndiyo waeleze msimamo wao kuhusu uzuri na ubaya wa Gaddafi.
Gaddafi huyo huyo alikuwa ni mshirika wa Gaidi OSAMA BIN Laden, inakuwaje tunawashangilia watu hatari kama hawa. Tunachokiona hapa siyo sera za nchi bali ni SIASA KWA AJILI ya 2015, sasa huu ndiyo ujinga wa serikali yetu.
Serikali kukataa kuwatambua waasi inamaana inafanya maandalizi kwenda Libya kuwafurusha serikali ya mpito ya Lbya. Tujiulize tena au tumuulize Waziri membe nini kauli yake kuhusu MAZISHI ya GADDAFI kufanyika BAHARINI kama ilivyokuwa kwa OSAMA BINLaden???
Watanzania tunaliona hili kuwa maombolezo hayo ni maalumu kwa MAFISADI na Wenyeuchu wa Madaraka ( Wachakachuaji na wezi wa KURA)na wala hayawakilishi Watanzania wenye nia njema.
mkuu wewe huwezi kufikiria hata kidogo? waasi wachache wakisaidiwa na mabeberu ndo wenye amri na ndo waliomuua Gaddafi sasa wewe unafikiri raia wa libya wanaujanja hapo? wamebaki kuumia kimoyomoyo tu. Kiukweli Mawazo ya Membe yamewakilisha mawazo ya wanyonge wa Libya ambao ni wengi. Hongera Membe kwa hilo.Hivi Ofisi za ubalozi wa Libya nchini nao wamepeperusha bendera nusu mlingoti? itakuwa ni AIBU na FEDHEHA kubwa sana kwetu kama wenye nchi waliofikwa na msiba bendera zao zipo juu kabisa na akina Membe wanahubiri ndivyo sivyo.
Well, huyo ni Membe bana. Kuna mbunge mmoja aliwahi kusema ndani ya bunge kwamba huyu bwana ni ''Joka la Kibisa'' (?)
Kama wanahamu ya kushusha bendera nusu mlingoti si washushe ya CCM? Wakishusha ya ccm wala hakuna atakae uliza maswali.
Kufuatia kifo cha Dictator Gaddafi serikali kupitia Waziri Membe itapeperusha bendera ya nchi nusu mlingoti. .