Ben Mtobwa "tutarudi na Roho zetu" afariki dunia

Katika malaika wa shetani,kwa kusema ukweli Ben Mtobwa alitenda haki. RIP
 
SIMANZI SANA: Kapumzike Beny, wewe na mwenzako Elvis mlinifanya niamini mlikuwa mnaandika mliyoyashudia kumbe ni mawazo yenu mliyatafsiri katika uhalisia fikirishi. Mlitufanya vijana wa kipindi hicho tufikirie uzalendo juu ya nchi yetu. Mlitufanya tutamani kuwa wapelelezi japo hatukujua hatua za kupitia, tuliwaona characters wenu kama watu halisi walioishi na tukatamani kuwa kama Joramu Kiango na Willy Gamba. Nitawakumbuka daima kama waandishi mahili mliojitoa kutetea nchi yenu kwa kuwahamasisha vijana kuwa wazalendo kupitia riwaya zenu. Nina huzuni juu yako Beny lakini nafarijika kwa sababu ulitimiza vema wajibu wako. Ulitumia kwa manufaa ya wote kipaji ulichojaliwa na muumba wako, hukuwa mchoyo, ulitugawia weledi wako kupitia vitabu vyako. NENDA BENY, MSALIMIE ELVIS, mwambie kuna watu umewaacha hai ambao hawatasahau Kazi zenu zilizotukuka.
 
R.I.P alikuwa akikimbizana na ELVIS MUSIBA kwa kutunga hadidhi za kusisimua za kipelelezi....nilizipenda sana hadidhi zao...na kila mara wakati nasoma nilisubiri vitabu vyao vipya.......huwezi kumfananisha hawa na watungaji wa sasa kina shigongo ..ambao wana copy and paste!!!....mnawakumbuka ma sterling wa mtobwa na musiba??
Joram kiango na prosper kwenye salam toka kuzimu.wily Gamba koffi na ozu katika kikosi cha kisasi akiwemo mrembo tete na mwadi bila kuwasahau kundi la magaidi waliokuwa na garage kina papa muteba na max
 
Duh.. this is very sad..

Nimesome hadithi zake nyingi sana na vitabu vyake na kwa hakika ni miongoni mwa watu ambao kupitia kazi zao walinishawishi sana kuanza kuandika hadithi.

Nakumbuka:

Malaika wa Shetani
Tutarudi na Roho zetu
Salam toka Kuzimu
Dar-es-Salaam Usiku
Najisikia Kuua Tena

N.k kwa kweli nitamiss sana kazi zake. I need to get a collection of his books.

RIP patner..!
""mgeni mwenye miwani myeusi...""
daahh....R.I.P Uncle Benny....
 
R.I.P BEN.miaka ya mwisho mwa80 na mwanzoni mwa 90 tulikuwa tukishindana sana na rafiki zangu GRACE BULEGI na JANETH MALUMWENE kusoma vitabu vyake.
 
SIMANZI SANA: Kapumzike Beny, wewe na mwenzako Elvis mlinifanya niamini mlikuwa mnaandika mliyoyashudia kumbe ni mawazo yenu mliyatafsiri katika uhalisia fikirishi. Mlitufanya vijana wa kipindi hicho tufikirie uzalendo juu ya nchi yetu. Mlitufanya tutamani kuwa wapelelezi japo hatukujua hatua za kupitia, tuliwaona characters wenu kama watu halisi walioishi na tukatamani kuwa kama Joramu Kiango na Willy Gamba. Nitawakumbuka daima kama waandishi mahili mliojitoa kutetea nchi yenu kwa kuwahamasisha vijana kuwa wazalendo kupitia riwaya zenu. Nina huzuni juu yako Beny lakini nafarijika kwa sababu ulitimiza vema wajibu wako. Ulitumia kwa manufaa ya wote kipaji ulichojaliwa na muumba wako, hukuwa mchoyo, ulitugawia weledi wako kupitia vitabu vyako. NENDA BENY, MSALIMIE ELVIS, mwambie kuna watu umewaacha hai ambao hawatasahau Kazi zenu zilizotukuka.
Elvis nadhani yupo hai
 
Hiyo title ya tutarudi na roho zetu imekaa vema sana japo sijawahi soma kitabu chake R.I.P
 
Back
Top Bottom