Kizuri sana....humu utaona wazalendo wanavyojitolea uhai wao kwa maslahi ya taifa kama kina KANDA WA KAMKANDA huku vibopa wakila maisha kama kina KANDILI ,lakini pia utayaona "mapenzi" na falsafa zake hasa kuhusu "kupenda kusiko na sababu" ,muhusika Dora anampenda kijana fukara ,hohehahe masikini kabisa ,lakini pia mwandishi ameonesha namna wanawake wanavyokosea kwa kuitumia vibaya huruma waliyopewa. Kandili alidhalilishwa shuleni na aliazimia kwenda kujiua, Dora katika kwenda kumnasihi asijiue akaona bora gauni lake lipande juu na suruali ya kandili ishuke chini(alimpa "utamu wote"hatimae akapata mimba). Kosa hilo hilo akarudia kulifanya akapata mimba ya pili......ni kitabu kizuri sana tena kinakwenda na wakati utadhani kimeandikwa jana tu mana yaliyomo humo hayatofautiani na haya ya "escrow"n.k lakini pia "mapenzi bwerere" yanayofanywa na vijana leo hii bila kujua athari yake.kitafute cha kiswahili kina "ladha nzuri" kuliko kile kilichofasiriwa kwa lugha ya malkia.
Mkuu Xie xie (Asante) can you do me a favour? Nisaidie namna gani naweza kupata hii copy. Xie xie!