Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,602
- 22,707
Kama umekuwa ukiangalia mechi za Japan mashindano ya Kimataifa hususan mechi ya kombe la dunia 2026 dhidi ya Uholanzi na kujiuliza ''Hivi huyu kipa mjapan mweusi ni nani?'' basi jua hauko peke yako.
Huyu anaitwa Zion Suzuki, na ni mmoja wa wachezaji wanaovuma sana kwenye kombe la dunia 2026 baada ya kuonesha uwezo thabiti wa kulinda lango lake dhidi ya timu yenye uwezo 'Uholanzi.
Suzuki alizaliwa Newark, New Jersey; baba yake ni Mghana na mama yake ni Mjapani, lakini alilelewa nchini Japan. Kwa maana hiyo, alikuwa na nafasi ya kuchezea nchi tofauti, ikiwemo Marekani. Lakini yeye aliamua kuichezea Japan na ameanza kuwawakilisha tangu akiwa mdogo.
Kwenye ngazi ya klabu, ameshacheza Japan, akenda Ubelgiji, na sasa hivi yuko Italia anakokipiga kwenye klabu ya Parma.
Mwaka 2023 aliwahi kupewa ofa na Manchester United, lakini aliikataa na kuchagua kujiunga na Sint-Truiden ya Ubelgiji ili kupata dakika nyingi za kucheza na kuendelea kukuza kiwango chake. Uamuzi huo umeonekana kumlipa baada ya baadaye kung'ara nchini Italia akiwa Parma. Soma Manchester UTD yamtaka Suzuki kama kipa wa akiba
Hata hivyo, safari yake haijakuwa rahisi kivile. Kwenye mashindano ya Kombe la Asia mwaka 2024, Suzuki alitukanwa sana mtandaoni kwa ubaguzi wa rangi baada ya timu yake kupoteza mechi. Baadaye alisema kuwa hana shida watu wakimkosoa kuhusu jinsi anavyocheza, lakini ubaguzi wa rangi ulikuwa umepita kiasi.
Sasa hivi ndio kipa namba moja wa Japan kwenye Kombe la Dunia, na ni mmoja wa wachezaji wanaobeba matumaini ya kizazi kipya cha timu hiyo ya 'Samurai Blue'.
Una maoni gani?