Bei za maji katika Nyumba za kupanga ni mateso

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Bei ya maji kwa Dar es Salaam ni Tsh. 1,663 kwa Unit moja(1) ambayo ni sawa Lita 1000 za maji, yaani Madumu 50 makubwa ya Lita ishirini.

Wapangaji wengi wakiamia kwenye Nyumba za kupanga za kushare maji au kulipiwa na mwenye Nyumba unakuta anaambiwa alipie Tsh. 15,000 hadi Tsh. 30,00 kwa mwezi. Tuafanye Tsh. 30,000 ambayo ni sawa na Unit 18, yaani lita 18,000 za maji sawa na Madumu 900 ya maji ya lita 20.

Kiwango hichi ni kikubwa kwa matumizi ya kawaida ya nyumban, ni sawa na maji ya mahoteli, guest, bar na migahawa mikubwa tena kuna muda inakuwa Chini ya hapo. Ila wewe mpangaji unalipia bila kufikiria.

Mamlaka ya Maji Imekaa Kimya katika hili wakati walipaswa kuwa mstari wa mbele kutetea wananchi katika suala hili la maji. Maji yamekuwa ni Biashara na sio Huduma tena.

Wapangaji wanaumia sana na hii hali ya Gharama za maji katika nyumba za kupanga. DAWASA tamisemi Saidie hili litokomwezwe, hii ni Utakatishaji Fedha kwa wananchi wa hali ya Chini.

images.jpeg
 
Solution ni simple sana kiongozi
Tafuta nyumba ambayo haina maji ndani uwe unachota kwa ndoo nje sh 100/200...!
Otherwise mambo ya wewe na mwenye nyumba wako Dawasco wanaingiaje hapo?
 
Mbona kama sijaelewa? Tatizo lipo Dawasa au wenye nyumba?
Tafteni mageto yenye mita.
Mamlaka ya Maji, ndo inapaswa kusimamia haki katika duma wanayoisimamia, kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa Usawa
 
Maji Yako kwa mwenye nyumba huko mi nanunua 100 dumu za hizi mvua zinanyesha ni kukinga mwanzo mwisho
 
Tsh. 100 ndoo, kwenye unite Moja ya Tsh. 1,663 kuna ndoo 100, ambazo zitakugharimu Tsh. 10,000.. we unaona ni akili hilo?
Kuna mzee wangu mmoja aliwahi kuniambia
Epuka kuonekana mbele za watu kama una maisha mazuri ilhali unateseka moyoni mwako
Yanini ukakae sehemu nzuri wakati bili ya maji ya 15,000 inakufanya ujieleze sana

Nenda kaishi buza,vikindu,kisemvule huko pia ni watz wanaishi
 
Mimi nipo nyanda za madini

Huku
Unit moja ni tsh 2100
Na hakuna kelele
 
Mimi nilikuwa bachela nikaambiwa niwe nalipia 10,000 badala ya 15,000 wanayolipa wenzangu.
Nilikataa nilisema nitakuwa nalipia kadri ninavyotumia yaani 100 kwa ndoo kwa sababu nikioga asubuhi napotea nikirudi saa 9 natumia maji ya bar kisha narudi kulala tu home usiku saa 3.
 
Wengi wa watanzania ni wapigaji, matapeli na watu wasio na upendo.

Miongoni mwao ni wenye nyumba za kupanga zenye wapangaji zaidi ya mmoja.
 
Wengi wa watanzania ni wapigaji, matapeli na watu wasio na upendo.

Miongoni mwao ni wenye nyumba za kupanga zenye wapangaji zaidi ya mmoja.
Kaka kitimoto Umeongea Point sana, tofauti na Kitimoto wenzio 🤣🤣🤣
 
Mimi nilikuwa bachela nikaambiwa niwe nalipia 10,000 badala ya 15,000 wanayolipa wenzangu.
Nilikataa nilisema nitakuwa nalipia kadri ninavyotumia yaani 100 kwa ndoo kwa sababu nikioga asubuhi napotea nikirudi saa 9 natumia maji ya bar kisha narudi kulala tu home usiku saa 3.
Tsh. 10,000 ni kubwa sana kiukweli kwa Bachela
 
Back
Top Bottom