Bei za mafuta Afrika Kusini (SA) zashuka

Bei za mafuta Afrika Kusini (SA) zashuka

Nikuletee makasiriko wewe usiyejua hata comparison ya uchumi wa nchi na nchi?

Watu aina yenu huku huwa tinawaponda mawe tu ili mrudi kwenye zile nyuzi zenu za kula tunda kimasihara na upuuzi mwingine.

Usijifanye mjuvi sana wa uchumi kuliko wengine.! Oil crisis hasa Africa imekua kubwa toka vita ya Ukraine ianze nchi nyingi bei zimepanda na kusababisha mfumuko mkubwa wa bei hata kwa bidhaa nyingine.!

Shida kubwa ni viongozi wetu kutokufanya kitu kutatutua hili tatizo kama kupunguza utitiri wa tozo/kodi kwny mafuta na kuweka ruzuku ya kweli sio porojo kama ilivyo sasa.!
 
Mkuu huu ndio uzuzu mwengine tuliokua nao sisi watanzania lini 26=3500?yaani huoni kuwa kuna tofauti hapo?why na sisi isiwe 26ths?,Zambia diesel ni 28ZWK,Botswana ni 17.9BWP, why na sisi ingekua 26ths?,kuna uzuzu mkubwa hapa
Inaonesha kwamba wewe ndio zuzu.
 
Kipato cha AK ni > 10 000 USD wakati Tanzania < 1 500 USD, hivyo mafuta AK ni rahisi kwa sana tu klk TZ!
Mkuu we ndio umesema point ya maana

Kiuhalisia mafuta yanaweza kuwa bei sawa ZA, USA na TZ, ila kwa kwa mTZ mafuta kwake ni ghali

Mtu USA anaweza earn avaragely USD 50 per day ila tukirudi Tanzania tuseme kwa siku tunakupa wastani wa tsh 30,000 kwa siku., mda huo lita moja tuseme ni 3400TZS ~ 1.5 USD

Tukiangalia hawa watu katika pato lao la siku mTZ atatumia asilimia kubwa ya pato lake la siku kununua lita moja ya mafuta, yani zaidi ya Asilimia 10% la pato lake linatumika nunua wese lita moja. Mtu kutoka US Atatumia asilimia tatu tu 3% ya pato lake ka siku kuipata lita moja

Katika hawa mTZ lazima afanye yafuatayo ili angalau aishi

-Alie Kama tunavyolia
-Apunguze kiasi cha mafuta anachonunua
-Apaki gari kama sio lazima sana kuwa nalo

Tuache siasa kuipata Rand 136 ZA sio ngumu kama kuipata 3500 bongo
 
Yes and that's a real meaning ya Exchange rate.

We chukua Rand 3000 uje nazo Bongo uone utachonunua kama hakifanani na kile ulichonunua SOUTH AFRICA.
Sawa mtaalam wa uchumi
 
Samahani naomba nikusaidie kukuelewesha kidogo kama utanielewa lkn. Nimeamka vizuri leo kuweza kutoa majibu yanayoweza kukusaidia huko mbeleni.

1. Strong Currency sio kigezo cha kuwa na uchumi mkubwa. Unaweza kuwa na Strong Currency na ukazidiwa mbali kwenye Uchumi. Mf. JAPANNESE YEN inabadilishwa kwa Tsh 17 za kibongo. Wakati huo huo Shilingi ya Kenya inabadilishwa kwa Tsh 19 za Kibongo. Lkn ukiangalia JAPAN ana uchumi mkubwa sana kuliko nchi zote za Afrika na Asia kwa ujumla wake.

2. Currency inategemea sana hali ya Export and Import. Kuna nchi zina export sana kuliko kuimport na hii hupekekea kuwa na reserve kubwa ya pesa za kigeni na hivyo kuimarisha pesa yake. Turudi kwa Japan, Japan yeye Sio muuzaji sana wa bidhaa na sio Mnunuaji sana wa Bidhaa, bidhaa kubwa anazouza Japan ni Magari na ambapo makampuni yake yametoa leseni ili kuzalishwa maeneo mbali mbali duniani ili kupunguza gharama.

3. Kitua ambacho nataka ukielewe tena hapa ni kwamba, Ukichukua hiyo Rand 139 ukiwa South Africa bidhaa utazozipata ni sawa na Ukichukua Shilingi 3500 ya Tanzania ukanunua bidhaa zilezile hapa kwetu.

Hizo exchange rate zimeweka kwa muktadha kuwa Bidhaa fulani utaipata katika uzani sawa dunia nzima, simply ni kwamba mchakato wa kuipata 139 Rand ni sawa na ugumu wa kuipata 3500 ya bongo. Usione namba ndogo ukadhani inapatikana tu kirahisi hivyo.
GDP ya SA ipo juu, hata kote palingane bei mtanzania atatumia sehemu kubwa ya kipato chake kununua mafuta.

Halafu strong currency sio kuwa inaizidi mara ngapi currency nyingine, we mwenyewe huelewi maana ya strong currency, strong currency ni currency himilivu, haishuki ovyo thamani yake.
 
Mbona hizo bei hazina tofauti ni Tanzania? Au wewe kwakuwa umeambiwa zimepungua ndio umekurupuka tu??

Exchange rate ni RAND 1= 139.22 TZS
Saaaaawa,!
Lakini kwanini kwetu Bei ipande wakati wengine wakishusha?
 
Tanzania hata wanunue mafuta nje lita 1 kwa tsh 500 bado watauza 3400

Nchi hii wanachojuaga ni kupandisha not kushusha

Ova
Kama serikali haihojiwi. Kila mtu anatakiwa kuwa “mzalendo”; kuonyesha utii, uaminifu na heshima ya hali ya juu kwa amiri jeshi mkuu na mtoa fedha kwa nini ajisumbue na kero za wananchi?

Watu wanasema wananchi hawana haja na demokrasia halafu wanategemea wakilalamika tu serikali ishushe bei ya mafuta, ipunguze tozo …! Kazi iendelee tu.
 
Unamiscalculate mkuu, utapata Lita sawa tu. Iko hivi, exchange rate ipo pale ili kubalance manunuzi, ila tambua fika ugumu wa na ukubwa wa matumizi wa hiyo pesa uko sawa kila upande, ni ishu ya namba tu hapo.

Lita 200 za mafuta ukinunua ZAMBIA kwa Kwacha. Ni sawa na Lita 200 za mafuta ukinunua hapo Tz, kwa kuibadilisha hiyo Kwacha.

Usichanganye uwingi katika namba, kaa kwenye exchange rate ndio utaelewa hiki nikisemacho hapa.
mkuu maswala ya uchumi ni magumu sana msiyaparamie.

unajua pato la raia mmoja wa SA kwa mwaka ukilinganisha na la MTZ?hapa ndipo hoja inapozaliwa.

USA $1 ni pesa ndogo mno,ila ukiwa nayo bongo ni 2300,hizo fugure mbili zina thamani sawa ila nguvu tofauti,kutokana na kipato cha watu husika.
ndio maana malalamiko zaidi yanaazia nchi za 3rd class huku.
 
Ukipga hesabu R25 x 150 utapata 3750 bado kwetu kuna kaunafuu kdogo
nenda kalinganishe pato la msouth mmoja na mtz mmoja,ili ujue kiuhalisia nani ni bei rahisi kwake???

hapa bongo mwalimu analipwa mshahara 430k,kule mtu aina yake anacheza hata kwenye 2mln.
embu wote wanunue mafuta 50lt tuone nani kakatwa pakubwa.
 
mkuu maswala ya uchumi ni magumu sana msiyaparamie.

unajua pato la raia mmoja wa SA kwa mwaka ukilinganisha na la MTZ?hapa ndipo hoja inapozaliwa.

USA $1 ni pesa ndogo mno,ila ukiwa nayo bongo ni 2300,hizo fugure mbili zina thamani sawa ila nguvu tofauti,kutokana na kipato cha watu husika.
ndio maana malalamiko zaidi yanaazia nchi za 3rd class huku.
Hata huku 2300 ni ndogo mno au wewe unaona nyingi???
 
Hata huku 2300 ni ndogo mno au wewe unaona nyingi???
ndogo ndio ila sio ndogo kwenye kila jambo.

mfano kama unanunua kilo ya sukari hii ni pesa ndogo,ila kama unanunua mafuta ni nyingi maama hutanuna lita moja ikutoshe.
 
Samahani naomba nikusaidie kukuelewesha kidogo kama utanielewa lkn. Nimeamka vizuri leo kuweza kutoa majibu yanayoweza kukusaidia huko mbeleni.

1. Strong Currency sio kigezo cha kuwa na uchumi mkubwa. Unaweza kuwa na Strong Currency na ukazidiwa mbali kwenye Uchumi. Mf. JAPANNESE YEN inabadilishwa kwa Tsh 17 za kibongo. Wakati huo huo Shilingi ya Kenya inabadilishwa kwa Tsh 19 za Kibongo. Lkn ukiangalia JAPAN ana uchumi mkubwa sana kuliko nchi zote za Afrika na Asia kwa ujumla wake.

2. Currency inategemea sana hali ya Export and Import. Kuna nchi zina export sana kuliko kuimport na hii hupekekea kuwa na reserve kubwa ya pesa za kigeni na hivyo kuimarisha pesa yake. Turudi kwa Japan, Japan yeye Sio muuzaji sana wa bidhaa na sio Mnunuaji sana wa Bidhaa, bidhaa kubwa anazouza Japan ni Magari na ambapo makampuni yake yametoa leseni ili kuzalishwa maeneo mbali mbali duniani ili kupunguza gharama.

3. Kitua ambacho nataka ukielewe tena hapa ni kwamba, Ukichukua hiyo Rand 139 ukiwa South Africa bidhaa utazozipata ni sawa na Ukichukua Shilingi 3500 ya Tanzania ukanunua bidhaa zilezile hapa kwetu.

Hizo exchange rate zimeweka kwa muktadha kuwa Bidhaa fulani utaipata katika uzani sawa dunia nzima, simply ni kwamba mchakato wa kuipata 139 Rand ni sawa na ugumu wa kuipata 3500 ya bongo. Usione namba ndogo ukadhani inapatikana tu kirahisi hivyo.
Hii topic mpaka hapa nilikuwa sijaelewa chochote angalau nimepata mwanga. Nina swali... hii spidi ya kukopa nje sana na kununua sana nje na kuuza nje rasilimali madini na twiga tuu inaipeleka wapi shilingi yetu?
 
Always ss tunauza sana RAW MATERIALS wakati tunanunua sana zile Final Product. Bei ya Malighafi iko chini ukilinganisha na bidhaa iliyokamilika, hivyo basi sisi tunaingiza kiasi kidogo cha pesa za kigeni kupitia bidhaa na tunatumia kiasi kikubwa sana cha pesa katika kununua final product.

Hapa itabidi tuamue ama tutumie sana vitu vyetu wenyewe local product ili kubalance manunuzi au Tuendelee na kukopa ili kupata fedha hizo za kigeni zaidi kupata bidhaa kutoka nje.

Kuhusu mikopo, kuna baadhi ya miradi ni bora ukope ili kufinance kuliko kutumia fedha za ndani, hapa tunaweza kutumia njia mbili, mikopo ya muda mrefu (riba kubwa) au tuingie ubia na mashirika ya ndani au nje ili kufinance miradi na tugawane mapato for some years. Hii njia ya pili inatumika sana Ulaya ili kuleta maendeleo kwa haraka. Mfano, daraja la kigamboni ni la ubia kati ya Serikali na NSSF.

USHAURI.

Lazima tutafute leseni au ubia na makampuni ya nje ili yaweke viwanda hapa kwetu ili kuzuia manunuzi makubwa ya nje. Mfano, tunaweza ingia ubia na SAMSUNG, SONNY, TOYOTA, MAZDA NK waweke viwanda vyao hapa ili tuwe hub ya Afrika mashariki na kati katika bidhaa hizo nk.

Hatua hii inahitaji zaidi uthubutu na hali ya uhakika katika Sera, mipango, usalama, miundombinu nk katika kufanikisha hili.

Huwezi kuendelea bila kuwa na viwanda vikubwa au malighafi yenye uhitaji zaidi duniani.

Ikumbukwe madini sio bidhaa muhimu kwa mwanadamu hivyo sio ya kutegemea saaaana, labda SHABA ambayo hutumia sehemu nyingi zaidi.
 
3. Kitua ambacho nataka ukielewe tena hapa ni kwamba, Ukichukua hiyo Rand 139 ukiwa South Africa bidhaa utazozipata ni sawa na Ukichukua Shilingi 3500 ya Tanzania ukanunua bidhaa zilezile hapa kwetu.

Ndugu unasema???
 
Back
Top Bottom