Bei ya trekta ya kulimia. Iwe mpya au mtumba

Bei ya trekta ya kulimia. Iwe mpya au mtumba

Halafu update MF 385 acha tu Aiseee lazima unuke pesa!!! Nashangaa DSM MTU ana Massey anazolea taka!??
ha..ha...ha...unategemea zifanye nini ikiwa wanaume wengi tu wanakula viungo vya mboga(chips) huku trekta zitafanya nini? unaweza tembea nyumba zaidi ya tatu unatafuta panga
 
Kuna hizi ursus ni nzuri
mkuu angalizo ni ikiwaimetoka Asia ni hatari, ka ni nje ya hapo lazima uangalie upartikanaji wa spear part, ila katika utendaji hayatofautiani sana labda kwa wanayoyajua sana ndo wanajua na ndo maana mi naweza kuambia MF 375 ni nzuri zaidi ama john deer flan,
 
mkuu 2WD kwenye mashamba ya mpunga ni tabu. ila kwa bei za kawaida unaweza pata 4WD massey furguson kama MF290 na series nyingine ambazo kwa mtu mmoja mmoja zinanunulika, hayo ma new holland mtu wa kipato cha kawaida hawezi nunua
Mkuu kama unapata wasafirishaji wazuri Barcelona hapo Spain,UK na Holland kwa used bei haijachangamka hata SA pia yapo bei za kawaida na ni Trekta kweli unaweza kutumia 24 hrs machine isizime na hakuna tatizo naifananisha na machine ya Man diesel Truck au Mercedes Benz Astros...
 
kweli mkuu kunajama alikuwa finland alitaka niuzia mzigo sema sikuwa poa, yeye huwa ananunua huko then anasafirisha kuja huku anamkabidhi mtu amuuzie
 
2WD itakwama kila mara kwenye tope huko inayotakiwa na hasa maeneo ya mashamba ya mpunga ni New Holland hili ni tractor bora sana linaweza kulima kwa Massa mengi kuliko matrector mengine shida linauzwa bei hata lililotumika kuliko brand zingine...Sema upate lenyewe maana kopi zake kutoka Pakistan na kwingineko yapo sasa hivi...
Beo ya New holland mpya ni kuanzia ngapi na used ni kuanzia ngali?
 
Kuna hizi ursus ni nzuri
Hizi tractor kutoka Poland ni mbabu sana!! Wizara ya kulimo imepewe izigawe kwenye taasisi za serekali wkiridhika nazo wazinunue zinaharibika balaa!! Tractor 85HP inauzwa milion 60 tena brand new??
Zimetolewa 45 mpaka sasa 12 zipo landad chini ya miezi 11!
 
Umekalili mzee chukua vatra ni zuri sana mpya ni milioni 60 unapewa tela disk za kulimia na halo complet.
Valtra ipovizuriz sana ila kwa bei sio kweli tumenunua Valtra 2016 hp 85 miion 110 iko poa sana!! Kumbuka VALTRA ni VALMET
 
Hizi tractor kutoka Poland ni mbabu sana!! Wizara ya kulimo imepewe izigawe kwenye taasisi za serekali wkiridhika nazo wazinunue zinaharibika balaa!! Tractor 85HP inauzwa milion 60 tena brand new??
Zimetolewa 45 mpaka sasa 12 zipo landad chini ya miezi 11!
Embu fafanua kiongozi. Mbona URSUS tumeambiwa ni massey funguson? Ina maana serikali inatuingiza chaka?
 
Embu fafanua kiongozi. Mbona URSUS tumeambiwa ni massey funguson? Ina maana serikali inatuingiza chaka?
URSUS ni URSUS na MF ni MF mkuu ka kunamtu anakwambia yote ni sawa jua unakuongopea bora angekuambia TAFFE na MF ni sawa ningeweza kukwambia zinakaribia kufanana
 
Kivipi, fafanua kidogo mkuu.
Upatikanaji wake wa spare ni mzuri sana na nafuu pia sema na unaweza kuzipata spare zake hata usiku wa manane na pia kuna mafundi wengi sana hapa tanzania wanaozijua massey,ila ni zile mtumba sio za pakistan.
 
Halafu update MF 385 acha tu Aiseee lazima unuke pesa!!! Nashangaa DSM MTU ana Massey anazolea taka!??
Ila hapa ukiwa unafanyia kazi mwenyewe ndio utaiona hela na sio kumkabidhi mtu mwingine halafu wewe upo town
 
Tafuta John Deere 6125 (Hp 125), zinakujaga aina mbili, autogearboxvna manual gearbox, CHUKUA MANUAL, utakuja kunishukuru baada ya saa 3000 za kazi. Bei inacheza 120M plus

Au tafuta New Holland Hp 90, Turkey. Nasisitiza, chukuwa ya Turkey, bei around 70m-90m, kama kazi si zaidi ya eka 15 kwa siku chukuwa TT75 Newholland 4WD, Turkey please.

Kama unataka used, Tafuta New Holland 90-110 (Original New Holland), bei around 7000$ - 12,000$
 
Mkuu 165 itaweza kulima kwenye ardhi ngumu?au wewe unalimia wapi?
mkuu hiyo inauwezo wa kufukua udongo wa aina yoyote huna haja ya kuwa na wasiasi na hiyo mashine ila nzuri iwe na engine model A4 212
 
Embu fafanua kiongozi. Mbona URSUS tumeambiwa ni massey funguson? Ina maana serikali inatuingiza chaka?
Hapana mkuu zinatoka Poland na zipo kama majaribio hivi!! Wanayoa hasa kwenye taasisi za kilimo ukiridhika nalo unalipa likizingua anlikagua then unalirudisha!
Jarib kugoogle mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom