ze-dudu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 18,696
- 24,743
Ilipaswa kuwa elfu kumi na sio buku tanoHivi punde Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamezua gumzo kubwa mitaani na mitandaoni baada ya kutangaza viwango vya tiketi kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.
View attachment 3471831
Tiketi za mzunguko zitauzwa kwa shilingi elfu 5, VIP C shilingi elfu 20, VIP B elfu 30, VIP A shilingi laki moja na Platinum shilingi laki tatu. Bei hizi zimeibua maswali makubwa kuhusu nia halisi ya kuwajumuisha mashabiki wengi uwanjani au kuwabagua.
View attachment 3471832
Kwanza, TFF imeshindwa kuzingatia ukweli wa hali ya maisha ya Mtanzania wa kawaida. Katika taifa ambalo kipato cha wananchi wengi ni cha chini, tiketi ya elfu 20 hadi laki moja ni mzigo usiobebeka. Matokeo yake, wapenzi wa mpira wanabaki kutazama mechi kwenye runinga au kupitia kurasa za habari mitandaoni kama Fawanews pamoja na Livesports088 badala ya kushuhudia uhalisia wa uwanjani.
View attachment 3471831
Pili, ulinganifu wa bei unaacha pengo kubwa. Mzunguko wa elfu 5 unaonekana kuwa na nafasi ya watu wengi kukimbilia hivyo kumaliza nafasi mapema. Lakini hatua ya kuruka moja kwa moja hadi elfu 20 au zaidi inawaziba mashabiki wa kipato cha kati ambao wangependa kuwa karibu na wachezaji wao. Kwa mfano, kama VIP C ingekuwa elfu 10 na VIP B elfu 15, basi mashabiki wengi wangejipanga kupata tiketi hizo bila kuona kama ni mzigo mkubwa.
View attachment 3471832
Matokeo ya mfumo huu ni kudhoofisha motisha ya mashabiki kwenda uwanjani. Uwanja usiokuwa na mashabiki unakuwa kimya, na kimya hicho hufifisha morali ya wachezaji. Kwa upande mwingine, mapato yanayotarajiwa na TFF yanaweza yasifikie lengo kwa sababu idadi ya wanaolipa tiketi kubwa ni wachache mno.
Mpira wa miguu ni burudani ya watu wote, si ya tabaka maalum, msitengeneze uvhawa wa kuanza kupeleka kampeni za CCM. Nchi nyingi zimefanikisha kutengeneza mazingira rafiki kwa kila kundi la mashabiki—wapo wanaoweza kulipia VIP ya juu, lakini pia wapo wanaohitaji tiketi nafuu ili tu kushiriki hamasa ya taifa lao. Bila uwiano huu, soka linageuka bidhaa ya kifahari badala ya urithi wa kijamii.
View attachment 3471830
Kwa muktadha huu, TFF inapaswa kutathmini upya sera za bei na kutengeneza viwango rafiki vitakavyowezesha uwanja kujazwa na mashabiki. Kadri mashabiki wanavyoongezeka, ndivyo mapato ya jumla yanavyokua. Lakini kwa mfumo wa sasa, mashabiki wengi wanahisi wametengwa na hawana budi kubaki watazamaji wa mbali kupitia mitandao.
View attachment 3471832
Kwa ufupi, mfumo huu wa bei si kikwazo tu kwa mashabiki, bali pia ni doa kwa maendeleo ya soka la Tanzania. Wapenzi wa mpira wanahitaji uwepo wa uwanjani, na si tiketi za bei zisizo rafiki zinazowafanya kuwa wageni kwenye mchezo wanaoupenda.
Zama za buku tano kiingilio zilishapitwa na wakati sasa hivi waweke buku ten tu inapatikana vizuri hata maisha yawe magumu kama zege