Bei ya Tiketi Katika Mchezo wa Ngao ya Jamii

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,148
Reaction score
10,571
Hivi punde Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamezua gumzo kubwa mitaani na mitandaoni baada ya kutangaza viwango vya tiketi kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.
1757838490330.jpg

Tiketi za mzunguko zitauzwa kwa shilingi elfu 5, VIP C shilingi elfu 20, VIP B elfu 30, VIP A shilingi laki moja na Platinum shilingi laki tatu. Bei hizi zimeibua maswali makubwa kuhusu nia halisi ya kuwajumuisha mashabiki wengi uwanjani au kuwabagua.
1757838475610.jpg

Kwanza, TFF imeshindwa kuzingatia ukweli wa hali ya maisha ya Mtanzania wa kawaida. Katika taifa ambalo kipato cha wananchi wengi ni cha chini, tiketi ya elfu 20 hadi laki moja ni mzigo usiobebeka. Matokeo yake, wapenzi wa mpira wanabaki kutazama mechi kwenye runinga au kupitia kurasa za habari mitandaoni kama Fawanews pamoja na Livesports088 badala ya kushuhudia uhalisia wa uwanjani.
1757838490330.jpg

Pili, ulinganifu wa bei unaacha pengo kubwa. Mzunguko wa elfu 5 unaonekana kuwa na nafasi ya watu wengi kukimbilia hivyo kumaliza nafasi mapema. Lakini hatua ya kuruka moja kwa moja hadi elfu 20 au zaidi inawaziba mashabiki wa kipato cha kati ambao wangependa kuwa karibu na wachezaji wao. Kwa mfano, kama VIP C ingekuwa elfu 10 na VIP B elfu 15, basi mashabiki wengi wangejipanga kupata tiketi hizo bila kuona kama ni mzigo mkubwa.
1757838475610.jpg

Matokeo ya mfumo huu ni kudhoofisha motisha ya mashabiki kwenda uwanjani. Uwanja usiokuwa na mashabiki unakuwa kimya, na kimya hicho hufifisha morali ya wachezaji. Kwa upande mwingine, mapato yanayotarajiwa na TFF yanaweza yasifikie lengo kwa sababu idadi ya wanaolipa tiketi kubwa ni wachache mno.

Mpira wa miguu ni burudani ya watu wote, si ya tabaka maalum, msitengeneze uvhawa wa kuanza kupeleka kampeni za CCM. Nchi nyingi zimefanikisha kutengeneza mazingira rafiki kwa kila kundi la mashabiki—wapo wanaoweza kulipia VIP ya juu, lakini pia wapo wanaohitaji tiketi nafuu ili tu kushiriki hamasa ya taifa lao. Bila uwiano huu, soka linageuka bidhaa ya kifahari badala ya urithi wa kijamii.
images (65).jpeg

Kwa muktadha huu, TFF inapaswa kutathmini upya sera za bei na kutengeneza viwango rafiki vitakavyowezesha uwanja kujazwa na mashabiki. Kadri mashabiki wanavyoongezeka, ndivyo mapato ya jumla yanavyokua. Lakini kwa mfumo wa sasa, mashabiki wengi wanahisi wametengwa na hawana budi kubaki watazamaji wa mbali kupitia mitandao.
1757838475610.jpg

Kwa ufupi, mfumo huu wa bei si kikwazo tu kwa mashabiki, bali pia ni doa kwa maendeleo ya soka la Tanzania. Wapenzi wa mpira wanahitaji uwepo wa uwanjani, na si tiketi za bei zisizo rafiki zinazowafanya kuwa wageni kwenye mchezo wanaoupenda.
 
Mkuu usilalamike,,,,ukiona haifai angalia kwenye TV.... mtu kama kipato ni kidogo unafata nini uwanjani ? Nenda banda umiza tazama game

Ama nenda kaa kuna tickets za 5000....

Maisha hayajawahi kuwa na usawa, na haitotokea......
 
Tena nabhuku banda umiza tunaweka buku 2. Kama vipi afuatilie redioni tu kama hana tv kwake.

Lipia buku 5 hiyo kabla haijaisha.
 
Kwanza hata hii buku 5 TFF wanatudharau sana. Sisi sio wanyonge, walau kiingilio kianzie buku 10.

Sasa hivi wajumbe na wananchi wanahela sana hizi zinazotolewa kwenye kampeni. Tupo vizuri, buku 5 viingilio enzi za Magu.
 
Hivi punde Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamezua gumzo kubwa mitaani na mitandaoni baada ya kutangaza viwango vya tiketi kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC.
View attachment 3471831
Tiketi za mzunguko zitauzwa kwa shilingi elfu 5, VIP C shilingi elfu 20, VIP B elfu 30, VIP A shilingi laki moja na Platinum shilingi laki tatu. Bei hizi zimeibua maswali makubwa kuhusu nia halisi ya kuwajumuisha mashabiki wengi uwanjani au kuwabagua.
View attachment 3471832
Kwanza, TFF imeshindwa kuzingatia ukweli wa hali ya maisha ya Mtanzania wa kawaida. Katika taifa ambalo kipato cha wananchi wengi ni cha chini, tiketi ya elfu 20 hadi laki moja ni mzigo usiobebeka. Matokeo yake, wapenzi wa mpira wanabaki kutazama mechi kwenye runinga au kupitia kurasa za habari mitandaoni kama Fawanews pamoja na Livesports088 badala ya kushuhudia uhalisia wa uwanjani.
View attachment 3471831
Pili, ulinganifu wa bei unaacha pengo kubwa. Mzunguko wa elfu 5 unaonekana kuwa na nafasi ya watu wengi kukimbilia hivyo kumaliza nafasi mapema. Lakini hatua ya kuruka moja kwa moja hadi elfu 20 au zaidi inawaziba mashabiki wa kipato cha kati ambao wangependa kuwa karibu na wachezaji wao. Kwa mfano, kama VIP C ingekuwa elfu 10 na VIP B elfu 15, basi mashabiki wengi wangejipanga kupata tiketi hizo bila kuona kama ni mzigo mkubwa.
View attachment 3471832
Matokeo ya mfumo huu ni kudhoofisha motisha ya mashabiki kwenda uwanjani. Uwanja usiokuwa na mashabiki unakuwa kimya, na kimya hicho hufifisha morali ya wachezaji. Kwa upande mwingine, mapato yanayotarajiwa na TFF yanaweza yasifikie lengo kwa sababu idadi ya wanaolipa tiketi kubwa ni wachache mno.

Mpira wa miguu ni burudani ya watu wote, si ya tabaka maalum, msitengeneze uvhawa wa kuanza kupeleka kampeni za CCM. Nchi nyingi zimefanikisha kutengeneza mazingira rafiki kwa kila kundi la mashabiki—wapo wanaoweza kulipia VIP ya juu, lakini pia wapo wanaohitaji tiketi nafuu ili tu kushiriki hamasa ya taifa lao. Bila uwiano huu, soka linageuka bidhaa ya kifahari badala ya urithi wa kijamii.
View attachment 3471830
Kwa muktadha huu, TFF inapaswa kutathmini upya sera za bei na kutengeneza viwango rafiki vitakavyowezesha uwanja kujazwa na mashabiki. Kadri mashabiki wanavyoongezeka, ndivyo mapato ya jumla yanavyokua. Lakini kwa mfumo wa sasa, mashabiki wengi wanahisi wametengwa na hawana budi kubaki watazamaji wa mbali kupitia mitandao.
View attachment 3471832
Kwa ufupi, mfumo huu wa bei si kikwazo tu kwa mashabiki, bali pia ni doa kwa maendeleo ya soka la Tanzania. Wapenzi wa mpira wanahitaji uwepo wa uwanjani, na si tiketi za bei zisizo rafiki zinazowafanya kuwa wageni kwenye mchezo wanaoupenda.
Kaa nyumbani tazama kwenye Tv kuna mambo mengi ya msingi sio soka tu
 
Mimi hofu yangu kwenye hiyo mechi ipo kwa kocha tubRoamin Fokz! Ataanza na wachezaji gani? Angekuwa mocha bado ni Miloud Hamdi ambaye amewazoea wacjezaji kwa muda mrefu, hata nisingekuwa na chembe ya hofu.

Kimsingi Yanga ina kikosi kizuri sana msimu huu. Mtihani uko kwa kocha namna atakavyo wapanga hao wachezaji ili wampe matokeo.
 
Hio ndo mechi pekee ya TFF kutajirikia maana kujaza uwanja mpaka derby zingine
 
Mbona bei za kawaida hizo Alafu kama mtu anaona nyingi unachukua tu mzunguko huo
 
Tuna faida ya kuwa na benchi letu la ufundi lile lile, Presha kubwa itakuwa kwao Yanga kwasababu wana benchi jipya la ufundi lakini pia wametoka kupata matokeo katika mechi nyingi dhidi yetu.

Fadlu David kuelekea mechi ya derby
20250915_135543.jpg
 
Back
Top Bottom