Bei ya sukari yapaa tena

Bei ya sukari yapaa tena

Faru John alipoingia Ikulu na sukari ikapanda bei na haijawahi kushuka, na inazidi kupanda
 
Uzuri wetu sisi ni kutoa malalamiko binafsi(unafiki). Nauli ya daladala huwa inapanda mara kwa mara, tunapinga kwa maneno tu, unaweza ukamsikia mtanzania yuko ndani ya daladala akishangaa watu kulalamika kupanda kwa nauli.

Nadhani ni mpaka tutakapopangiwa bei ya pumzi ndio tutakuwa wamoja.
 
Matukio hayaishi? ilikuwepo wafanyakazi hewa, mara njaa, juz juzi madawa ya kulevya, sasa tena sukari; wapi tunaelekea? yote yanaibuka na kupotea bila majibu kamili. tujitafakari upya!!!!!
 
Hapa Morogoro imepanda toka 98000/= hadi 110,000/=kilo nauza 2600 dukani kwangu, sipendi ujinga mimi.
 
Matamko yahasaidii kitu mkuu.

Inabidi tu kucheza ngoma kama inavyopigwa.

Kama kawaida ya kila mwaka kipindi cha masika viwanda vya sukari vimeanza kufungwa na sukari imepanda bei.

Hapa Arusha bei ya jumla imepanda kutoka tzs 98,000 kwa mfuko wa kilo 50 hadi TZS 1050,00. Bei ya rejareja ni TZS 2,500 kwa kilo kutoka 2,200.

Tunaomba Waziri Mkuu atoe tamko kama hii ni halali na serikali inachukua hatua gani kuziba pengo kama kuna upungufu.
 
Kama kawaida ya kila mwaka kipindi cha masika viwanda vya sukari vimeanza kufungwa na sukari imepanda bei.

Hapa Arusha bei ya jumla imepanda kutoka tzs 98,000 kwa mfuko wa kilo 50 hadi TZS 1050,00. Bei ya rejareja ni TZS 2,500 kwa kilo kutoka 2,200.

Tunaomba Waziri Mkuu atoe tamko kama hii ni halali na serikali inachukua hatua gani kuziba pengo kama kuna upungufu.
Haijawahi kushuka hiyo bei tangu hiyo kampeni ya kuzuia sukari inayotoka nje, kiukweli kama nchi hii tunataka tupige hatua inabidi siasa ziwekwe pembeni kwenye mambo ya kitaaluma, demand na supply ni somo pana lakini kwa ajili ya siasa viongozi wetu hawakutaka kujuua lolote kuhusu nguvu mbalimbali zinazoweza kufanya kuwe na punguzo la bei, utoshelevu wa vitu n.k. kilichofanyika ni kupiga marufuku bila kutathmini matokeo yake. Pamoja na hotuba na hamasa nyingi nashauri mambo ya kitaalam tuwaachie wataalam na mambo ya siasa yajikite kwenye siasa vinginevyo mtajipiga roba mshindwe pakutokea kama sasa, sukari inapanda wale wananchi wanyonge wanashindwa kunywa chai matokeo yake watarudi kusaga miwa kwenye kinu ili watumie utamu wake kuchanganya na maji waaite chai. Haya mambo fanyeni taratibu hatuna haraka nchim hii itakuwepo tu fanyeni hata vitu viwili vya msingi mtakumbukwa tu kuliko hizi haraka za mambo.
 
kinachonishangaza sukari inazalishwa Kilimanjaro lakina being inakuwa sawa na wale wa mikoa ambayo sukari tunawpelekea
 
Amini Amini nawaambia nchi inaenda kusimama. Hakuna kinachoendelea. Haya ndo madhara ya One Man show. Wakija kwenye sukari, bandarini wanaendelea na mambo yao, wakienda bandarini, sembe inapita airport, wakija kwenye sembe, bei za bidhaa zimepanda. Sijui nifananishe na nini hata.
 
Watanzania walipolilia katiba mpya toleo la Warioba, Kondakta akaenda kumtwanga makofi mzee wa watu. Sasa yanatutokea puani. Tunahitaji mfumo wa uendeshaji nchi ambao Rais atapunguziwa madaraka ya maamuzi na badala yake taasisi husika ziwe na nguvu kisheria na kiutendaji. Bila tume huru ya uchaguzi, bila bunge na mahakama kuingiliwa na dola (hii nimetaja mifano tuu), nchi hii hatuendi popote
 
Hapa wafanyakazi ni mwendo wa kuumia tu,
kama kweli tuna nia ya dhati kuisaidia nchi hii
tuondoe siasa kwenye mambo ya msingi.
wafanyabiashara wetu ni wepesi wa kupiga
kelele soko la ndani lilindwe huku hawajajipanga
kufanya biashara.

Msimu wa mvua hautokei kama kimbunga
au majanga mengine ambayo hutokea bila taarifa.
msimu wa masika unafahamika majira yake,
sasa iweje wanashindwa kujipanga kulikabili soko?

Kuna ukweli usiopingika kuwa wakulima
wa miwa wanafanyiwa hujuma na wenye
viwanda ili wanunue miwa yao kwa bei rahisi
hivyo waliowengi wameamua kuacha kulima miwa
mtu analima shamba na kulitunza kwa gharama
wakati wa kuvuna kunatokea mizengwe
mpaka miwa inaharibikia shambani.

Tunaweza kuzungumzia msimu wa mvua
lakini kumbe nyuma ya pazia kuna sababu
nyingine nyingi ambazo si rahisi kuzitoa
mpaka mvua inyeshe ionekane kuwa sababu.

Mamlaka zinazohusika ziliangalie suala
hili kwa makini ili kupata ufumbuzi
wa kudumu,vinginevyo wachache wataendelea
kunufaika kwa kucheza na soko,ili sukari
ionekana ni bidhaa adimu na bei iwe juu.
 
Kama kawaida ya kila mwaka kipindi cha masika viwanda vya sukari vimeanza kufungwa na sukari imepanda bei.

Hapa Arusha bei ya jumla imepanda kutoka tzs 98,000 kwa mfuko wa kilo 50 hadi TZS 1050,00. Bei ya rejareja ni TZS 2,500 kwa kilo kutoka 2,200.

Tunaomba Waziri Mkuu atoe tamko kama hii ni halali na serikali inachukua hatua gani kuziba pengo kama kuna upungufu.
Hii nchi kwa drama si mchezo, hivi wale waliokamatwa na sukari kipindi kile suala hilo liliishia wapi, maana tuliahidiwa kupewa sukari bure kutoka kwa wahujumu uchumi walioficha sukari, lakini sikuona tena lolote likitendeka, tukaahidiwa kuwa bei elekezi ya sukari itakua Sh 1,700/- kwa kilo lakini wapiii, sukari inazidi kupanda mlima kilimanjaro, Kina Bashite wanaacha kusimamia mahitaji ya msingi kwa kuwa hayana kiki kama hayo mengine, ndio maana basic needs kwa wananchi wanazipotezea, mbaya zaidi pesa hakuna kitaa, tusishangae kunywa chai kwa pipi.
 
Back
Top Bottom