Bei ya SUKARI mikoa mbalimbali Tanzania

Bei ya SUKARI mikoa mbalimbali Tanzania

Serikali inapotoa bei elekezi kwa baadhi ya bidhaa muhimu ni lazima zifuatwe. Anayekiuka bei hizi elekezi cha mtema kuni huwa anakipata. Tumeona kwa mfano bei elekezi za mafuta ya taa na petrol wanaozikiuka jinsi wanavyoshughulikiwa perpendicularly!

Kwa nini sasa hawa wenye viwanda vya sukari au mawakala wao wameachwa hivi hivi wakikiuka bei elekezi ya sukari. Kwa nini wasifuate hiyo bei hata kama watamaliza kabisa hiyo sukari toka viwandani mwao au kwenye maghala ya mawakala wao? Kwani ikiisha kuna mtu ataumia au kufa kwa kukosa sukari? Sukari kwanza haina umuhimu kama mafuta ya petrol au disel ambayo wafanyabiashara yake wanafuata bei elekezi. Watanzania wengi walishaacha kutumia hiyo kitu kwani hata hiyo bei elekezi bado ni kubwa mno. Tulitegemea itaendelea kushuka hadi angalao sh 500 kwa kilo.

Kwanza hii ilikuwa fursa nzuri kwa wenye viwanda na mawakala wao kuuza sukari yao kwa wingi. Si ni wao wenyewe ndiyo walikuwa wakilalamikia soko lao kuporwa na sukari toka nje wakati wana uwezo wa kutosheleza mahitaji ya nchi na kuwa sukari imerundikana viwandani kwa kukosa soko. Wamepewa fursa hiyo lakini ndani ya wiki chache tu wamevurunda ili waongeze faida kwa kupandisha bei kiasi hichi. Kumbe hili ndilo lilikuwa lengo lao?

Kwa nini serikali haijawatumbua jipu hawa jamaa hadi sasa? Mawakala wanaokiuka hizi bei elekezi wanajulikana kila mahali. Wanauza mfuko mmoja wa kilo 50 Shs 120,000 hadi 150,000 badala ya bei elekezi ya shs 70,000 hadi 80,000/. Mawakala hawa wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa hatua kali za kisheria. Kama kuna wenye viwanda ambao walikuwa wakiuzia mawakala wao kwa bei zaidi ya ilivyoelekezwa nao washughulikiwe mara moja.
Kwa nini wanabembelezwa?

Ushauri: serikali ianzishe maghala yake makubwa ya sukari kama ambavyo inavyofanya kwa nafaka (National Grain Reserve) ili kuwalinda walaji wa sukari hadi pale viwanda vyetu vitakapokuwa na uwezo na discipline ya kukidhi mahitaji. Maghala haya ya sukari (National Sugar Reserve) yanaweza kupata sukari yake toka nchi za nje yenye ubora unaohitajika. Viwanda vyetu vinapokuwa na upungufu wa sukari mawakala wa sukari wataipata kutoka maghala haya. Hii pia itazalisha ajira kwa maafisa kilimo na watu wengine. Na inawezekana hii apparent shortage imetokana na wananchi wanaotumia sukari kuongezeka baada ya bei kupungua kidogo kuwa sh 1,800. Ni kama ilivyotokea kwenye elimu ya bure. Tunataka wananchi wengi wa kawaida nao wanywe chai au uji wa sukari. Hili litawezekana tu pale bei itakapopungua zaidi. Hili kwa kuanzia litawezekana tu kwa kuwa na maghala haya ya serikali, baadaye viwanda vya sukari vitakapojengwa vingi basi umuhimu wa hizi National Sugar Reserve (NSR) utahitimishwa.
 
Hivyo ndivyo tutakua tunaendelea kulipia ada Kwa mfumo huo.
Unafikiri walipo kuwa wanasema wamefuta ada unafikiri wenyewe hawakupiga hesabu serikali Siku zote hawajawahi kuwa wajinga.
 
Hivyo ndivyo tutakua tunaendelea kulipia ada Kwa mfumo huo.
Unafikiri walipo kuwa wanasema wamefuta ada unafikiri wenyewe hawakupiga hesabu serikali Siku zote hawajawahi kuwa wajinga.
Walijua na ndiyo maana wakasema ni bure hadi kidato cha nne kwani hesabu ilionyesha mzigo ambao serikali ingeweza kuubeba ni hadi kidato cha nne kwa sasa. Ndiyo maana hawakusema bure hadi kidato cha sita au hadi chuo kikuu.

Lakini mada hapa ni sukari na bei elekezi kukiukwa. Hapa bei elekezi ya sh 1,800 iliyotolewa ili kuwa ni baada ya kukokotoa mahesabu wakiwa pamoja na wenye viwanda kukubaliana. Ndiyo maana punguzo lilikuwa ni dogo tu la sh 200 na hii ilikuwa kwa manufaa zaidi kwa wenye viwanda kupata soko. Cha ajaabu wamekiuka na serikali inachelewa kuwatumbua.
 
Uji ni wanga, na wanga una sukari ya kutosha sana kwa ajili ya energy. Ukiweka sukari ni anasa za kutaka flavour tu. Thats why diabetic patients hawatumii wanga mwingi..!

Ila chai bila sukari ni maji + caffeine tu.

Bora hata maziwa japokuwa ni waTz wachache wenye uwezo wa kunywa maziwa kila siku.

Ila uji najua wengi wanaweza kuupiga. Unga si tunao bhana..! Nilipokuwa shule nilipiga sana fororo (uji usio na sukari) & nilinenepa mno.
Uji bila sukari inawezekana lakini Chai bila sukari mmmhhh ni shidaaaa.
 
Hii habari sasa imekua mbaya hapa mjini sina uhakika kama muheshimiwa Magu alikurupuka au vp lakini ninaimani alifanya haya kwa nia njema tu kwa wafanya biashara wa hapa ndani ya nchi lakini pia na uhakika hakufanya upembuzi yakinifu kama viwanda vya ndani ya nchi vinauwezo wa kusambaza na kutosheleza mahitaji ya nchi kwa sasa au la matokeo yake ametengeneza dili kwa wafanya biashara sasa wananchi wanataabika naona tunarudi sasa kwenye enzi zile za mwalimu
 
Itabidi kujikaza tu hiki kipindi cha mpito. Au kama vipi unaacha kabisa kutumia, kwan shida nini.
Kwanza sukari inaleta kisukari.
 
Ili kujifungua lazima upite uchungu mkali wakati wa Mwalimu akina Salim waliulegeza uchungu tusingekuwa hapa tuvumilieni akili itapanuka
 
Naona kina Mizengo wanafanya yao baada ya kuzuiwa kuingiza utamu wa chai nchini
 
Sisi huku vijijini tunakula viporo au tunakula ugali asubuhi kabla ya kwenda kwenye kazi zetu shauri yenu nyie watu wa mujini
 
Hii habari sasa imekua mbaya hapa mjini sina uhakika kama muheshimiwa Magu alikurupuka au vp lakini ninaimani alifanya haya kwa nia njema tu kwa wafanya biashara wa hapa ndani ya nchi lakini pia na uhakika hakufanya upembuzi yakinifu kama viwanda vya ndani ya nchi vinauwezo wa kusambaza na kutosheleza mahitaji ya nchi kwa sasa au la matokeo yake ametengeneza dili kwa wafanya biashara sasa wananchi wanataabika naona tunarudi sasa kwenye enzi zile za mwalimu
Enzi za Mwalimu sukari ilikuwaj
 
Anza kunywa supu badala ya CHAI.matumizi mengine ya sukari tumia njia mbadala
 
  • Thanks
Reactions: 999
Hakawii kusema tule miwa kama tunaona sukari ni ghali, hahahahaaha si alisema tupige mbizi??
 
  • Thanks
Reactions: 999
Kwani mlishalegeza mkanda mlioambiwa mfunge kipindi cha miezi 18 kilipotangazwa na "mchonga"

Ambao hawajalegeza mikanda yao hata ikifika 12,000 kwa kilo haita waathiri, watachekelea tu maana kodi kubwa itakusanywa i.e VAT

Kitaa wanasema katelefon ametoa boko,
Tunataka kuona RIAKSHENI ya magu, maana kuna mtumishi alikuwa hachuku"agi" mshahara akamrukia fasta!!!! hatujui kutokuchukua mshahara kulituhasarishaje,
Mwingine akasoma taarifa aliyoandaliwa "hakuna watumishi hewala" akadandiwa fasta

Sasa huyu mpaka watoto wanaona hasara aliyoisababisha kwa kutokujua kwake kuwa kauli yake ni sheria, "watoto wanakunywa uji mchuchu" akili itatoka wapi (ndio maana akitokea kama yule aliyehutubia YUENI mpaka vigwangala wanajitwika kuwasomesha, kwa kuwa ni ajabu kweli kweli, ametokea wapi huyu)

Katelefon kazua balaa
 
Sioni umuhimu mkubwa wa sukari hadi malalamiko kiasi hiki. Chai bila sukari mbona inapita tuu.
 
  • Thanks
Reactions: 999
Mwenye mada utakuwa na duka hivo unatafuta njia na sababu kupitia maoni ya watu!!
 
acheni kunywa chai jaman mbona mnakuwa hampend serikali yenu.................................................................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom