Bei ya mchele haikamatiki mtaani inakaribia 3,000

Morning_star

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2018
Posts
6,009
Reaction score
17,457
Jamani hili ni janga la taifa. Hivi wananchi hatuna utamaduni wa kutunza hakiba au wafanyabiashara wanakomoa wakitaka kutengeneza faida juu ya faida? Juzi juzi tu mchele mzuri Dar ulikuwa unapatikana kati ya 1,200 hadi 2,000. Sasa hivi kilo moja hadi 2,800??
 
Nilijua ni tatizo la mtaani kwetu, huku mchele umeadimika mno mamangi wanasema hali ni mbaya. Ule wa 1,800 ndo unapatikana kwa 2800
 
Naombea hali hii idumu mwezi mmoja ndio Niko navuna. Yaani ni mwendo wa kubeba tani mmoja hakuna ushuru kama alivyosema muheshimiwa
 
Wakulima wanakaribia kuanza kuvuna tulieni bei itashuka
Wapi huko wanakaribia kuvuna? Kwa sasa ndiyo kwanza unaanza kuchanua mmoja mmoja , ngoma bado sanaa
 
Mtaani kwangu umefikia 1700 kutoka kwenye 2000 na bado unatazamiwa kushuka zaidi.
 
Jamani hili ni janga la taifa. Hivi wananchi hatuna utamaduni wa kutunza hakiba au wafanyabiashara wanakomoa wakitaka kutengeneza faida juu ya faida? Juzi juzi tu mchele mzuri Dar ulikuwa unapatikana kati ya 1,200 hadi 2,000. Sasa hivi kilo moja hadi 2,800??
Na mshahara ndio umegoma kupanda hadi mwenyezi apende, tutalima kwa meno!
 
Jamani hili ni janga la taifa. Hivi wananchi hatuna utamaduni wa kutunza hakiba au wafanyabiashara wanakomoa wakitaka kutengeneza faida juu ya faida? Juzi juzi tu mchele mzuri Dar ulikuwa unapatikana kati ya 1,200 hadi 2,000. Sasa hivi kilo moja hadi 2,800??
Kwetu hadi juzi ni 2500 nashindwa kula ubwabwa kwa kweli
 
Mbona mchele umeshuka, kwa sasa nanunua mabatini Mwanza shilingi 1750 hadi 1850. Nikipeleka dukani kwangu napata faida kiasi, lakini zamani nilishauza hadi shilingi 2600, ila leo siwezi kabisa
Labda kwenu
 
Back
Top Bottom