Bei ya mafuta ya kupikia yapaa!

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,132
5,785
Baada ya kauli iliyotolewa na rais JPM wakati akizindua kiwanda cha mafuta huko shinyanga kuwa ataongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta zinazoingizwa nchini kutoka nje,bei ya mafuta yanaozalishwa hapa nchini imepanda ghafla. Bei ya mafuta lita 20 ilikuwa tsh. 58000/-imepanda hadi tsh. 62000/-.ctn ya mafuta lita tano ilikuwa 57000/-sasa ni 61000/-ctn ya lita moja ilikuwa 36000/-sasa ni 39000/-my take :rais angeongeza kodi kimya kimya badala ya kutamka hadharani kuwa ataongeza kodi kwenye mafuta yanayoingizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.
 
Wala hamna tatizo. Yapande hata kufikia 100,000/= kwa lita. Hiyo ndo fursa kwa wakulima wa Alizeti, Ufuta, Pamba na Maweze ndani ya nchi. Lazima tuwalinde wakulima wetu na wazalishaji wa mafuta ya kula wanaotumia mbegu zinazozalishwa ndani ya nchi. Mafuta ya kutoka nje ya nchi lazima iwekewe kodi kubwa ili kulinda wakulima wetu wa ndani pamoja na wazalishaji wa mafuta ya kula ndani ya nchi.
 
hii ingekua na maana zaidi kama mafuta yanayozalishwa nchini yanakidhi mahitaji lakini ikuhalisia kuna tofauti kubwa sana, tuna upungufu wa karibu tani laki tatu
 
Kama ilivyokuwa kwenye sukari tu.

Viwanda vya ndani hujitapa vinauwezo lakini uagizaji WA nje ukizuiwa vinashindwa.
 
Sasa kila mtu akitaka kuwa Mchumi tutafika kweli?

Muheshimiwa hakutaka apandishe kimya kimya, na mpaka kutamka vile lazima ana baraka za Washauri wake wa uchumi.
 
hii ingekua na maana zaidi kama mafuta yanayozalishwa nchini yanakidhi mahitaji lakini ikuhalisia kuna tofauti kubwa sana, tuna upungufu wa karibu tani laki tatu
Kuweka kodo katika mafuta yanayotoka nje ndo kutafanya uzalishaji wa mafuta ndani ya nchi kuongezeka maana wanaoagiza mafuta hayo nje ya nje ni wafanya biashara wa Kitanzania wenyewe. Ukifanya uagizaji toka nje kuwa wa gharama kutawafanya wawekeze katika uzalishaji wa mafuta hayo kwa kutumia mbegu zinazozalishwa mndani ya nchi na wenyewe watawekeza katika uzalishaji ndani ya nchi. Ndivyo wanavyofanya nchi zote zilizoendelea. Ukitaka kukuza uzalishaji ndani ya nchi unaweka kodi katika bidhaa ya aina hiyo toka nje ya nchi. Just simple ,ike that, You make import expensive. Hiyo itawasaidia wakulima wetu wa Alizeti kule Manyara, Singida, Dodoma, Shinyanga, Arusha na Rukwa kwa kupata bei nzuri ya alizeti yao na kuongeza uzalishaji maana soko la uhakika litakuwepo.
 
Mi yangu macho maana sukari iliuwa hivihiviii,,angewaona wataalamu Wa uchumi wamulze ,,tunazalisha kiasi gani na tunaingiza kiasi gani
 
Kama ilivyokuwa kwenye sukari tu.

Viwanda vya ndani hujitapa vinauwezo lakini uagizaji WA nje ukizuiwa vinashindwa.
Sukari kwa sasa ni tsh 3000kg. wakati tuliambiwa bei elekezi ni 1800/-
 
Kuweka kodo katika mafuta yanayotoka nje ndo kutafanya uzalishaji wa mafuta ndani ya nchi kuongezeka maana wanaoagiza mafuta hayo nje ya nje ni wafanya biashara wa Kitanzania wenyewe. Ukifanya uagizaji toka nje kuwa wa gharama kutawafanya wawekeze katika uzalishaji wa mafuta hayo kwa kutumia mbegu zinazozalishwa mndani ya nchi na wenyewe watawekeza katika uzalishaji ndani ya nchi. Ndivyo wanavyofanya nchi zote zilizoendelea. Ukitaka kukuza uzalishaji ndani ya nchi unaweka kodi katika bidhaa ya aina hiyo toka nje ya nchi. Just simple ,ike that, You make import expensive. Hiyo itawasaidia wakulima wetu wa Alizeti kule Manyara, Singida, Dodoma, Shinyanga, Arusha na Rukwa kwa kupata bei nzuri ya alizeti yao na kuongeza uzalishaji maana soko la uhakika litakuwepo.
Mbona sukari imeshindwa matokeo bei imepanda,maFuta mtaweza?
 
Kwakuwa bado tuna vigereji vidogo dogo hapa nchini, afute kabisa kodi kwenye kuingiza magari ili kuchochea maendeleo kwenye usafiri....

Hatuzalishi magari nchini.....kodi kubwa ni kwaajili ya nini?
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana. Kila siku wanalalamika kuwa Watanzania wamekuwa maskini. Serikali ikuchukua hatua kuwainua hao hao Watanzania wanalalamika tena. UKWELI UNABAKLI PALE PALE. HAKUNA NAMNA NYINGINE YA KUWASAIDIA WAKULIMA WETU ZA MAZO HAYO YA MBEGU ZA MAFUTA TUSIPOWEKA MAZINGIRA MAGUMU YA UINGIZAJI WA MBEGU KAMA HIZO NA MAFUTA YA KULA KUTOKA NJJE YA NCHI. HIVYO NDIVYO WANAVYOFANYA NCHI NYINGI ZILIZOPIGA HATUA. HIYO NDO FURSA HATA KWAKO, NENDA KAWEKEZE KATIKA KILIMO CHA ALIZETI, UFUTA, PAMBA NA MAWESE. SERRIKALI IMEKUHAKIKISHIA SOKO. HATUWEZI KUTUMIA AKIBA YA FEDHA NYINGI ZA KIGENI KUAGIZA MAFUTA YA KULA NJE YA NCHI WAKATI WAKULIMA WETU WANAZALISHA MBEGU HIZO HIZO NDANI YA NCHI.
 
Baada ya kauli iliyotolewa na rais JPM wakati akizindua kiwanda cha mafuta huko shinyanga kuwa ataongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta zinazoingizwa nchini kutoka nje,bei ya mafuta yanaozalishwa hapa nchini imepanda ghafla. Bei ya mafuta lita 20 ilikuwa tsh. 58000/-imepanda hadi tsh. 62000/-.ctn ya mafuta lita tano ilikuwa 57000/-sasa ni 61000/-ctn ya lita moja ilikuwa 36000/-sasa ni 39000/-my take :rais angeongeza kodi kimya kimya badala ya kutamka hadharani kuwa ataongeza kodi kwenye mafuta yanayoingizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.
Hata sukari alituponza kutoka sh 1800 mpaka sasa 2800 na 3000
 
Kwakuwa bado tuna vigereji vidogo dogo hapa nchini, afute kabisa kodi kwenye kuingiza magari ili kuchochea maendeleo kwenye usafiri....

Hatuzalishi magari nchini.....kodi kubwa ni kwaajili ya nini?

capital goods zote ikiwemo matreka, tipa, machine za uzalishaji hazina kodi muda mrefu. Kama wewe una mtaji fanya biashara ya kuingiza matreka, mashine za kusindika, mashine za viwandani, mashiune za kurahisha kilimo mashambani n.k hazina kodi. Ila kama unataka kuingiza saloon car yako ili utuongezee foleni Dar hiyo tutaipiga kodo ya kufa.
 
Huyu Mzee hajifunzi kabisa. Hakujifunza kwanye sukari leo ameangukia kwenye mafuta. KAAAAAAAAAH!!!!!!!!!!!!
 
Baada ya kauli iliyotolewa na rais JPM wakati akizindua kiwanda cha mafuta huko shinyanga kuwa ataongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta zinazoingizwa nchini kutoka nje,bei ya mafuta yanaozalishwa hapa nchini imepanda ghafla. Bei ya mafuta lita 20 ilikuwa tsh. 58000/-imepanda hadi tsh. 62000/-.ctn ya mafuta lita tano ilikuwa 57000/-sasa ni 61000/-ctn ya lita moja ilikuwa 36000/-sasa ni 39000/-my take :rais angeongeza kodi kimya kimya badala ya kutamka hadharani kuwa ataongeza kodi kwenye mafuta yanayoingizwa kutoka nje ili kulinda viwanda vya ndani.
NIPE RTE INAPOELEKEA MPWAAA
NIKUPE EMERG AIRPORT ZA KUSHUKIA

ALTRN MWZ
ALTN JRO

KAMA YATASHINDWA KUTUA KIWANJA INAPOELEKEA ...YASHUKIE MWANZA AMA KILIMANJARO AIRPORT
 
Back
Top Bottom