Bei ya Godoro la Tanfom Arusha na QFL Dodoma

Ahsanteni kwa michango yenu wadau, niliwasiliana na makao makuu ya tanfomu Arusha kiwandani, wakanielekeza kwa wakala wao Mwanza , tukawasiliana na wakala na jmatatu naenda kuchukua kwenye godown lao hapa Mwanza, bei elekezi ni 330000 godoro la tanfomu 5×6 inch 8 edge
 
kwahyoo siku hizi ....great thinker wana uliza bei ya magodoro .....?


Mwakani great thinkers watauliza hadi bei ya chupi na chandarua ..........








Oh my enemy wants to kill me for no reasons.......
 
Kampuni iseme kitu la sivyo watapoteza wateja wengi. Mimi nimekuwa mteja wao lkn ukinunua miaka 2 bahati . Yani unaumia mgongo.
 
Hayo magodoro dodoma yananichanganya kuna siku muuzaji aliniambia kuna aina mbili za magodoro dodoma, kuna QFL magodoro dodoma na kuna magodoro dodoma asilia hata kwenye cover yameandikwa dodoma asilia sasa sijui ni kampuni mbili tofauti au ni kampuni 1
 
Usinunue godoro kwenye maduka ya kawaida hapo ulipo jitahidi ufike kwa wakala wa Tanfoam hutojutia.

Godoro madhubuti,imara na maridadi kabisa kwa thamani ya pesa yako.
 
Duh! Nili-search uzi wa aina hii ili kupata taarifa kwa 6x6 (x8 au 10). Sasa kama 5x6 ni 330K, 6x6 ( 8 au 10) si itakuwa zaidi ya gwala?! Akili zangu nazijuaga mwenyewe, sikawagi ku-import mimi, hata kama ni godoro!!
 

Hiyo ni lugha ya biashara.
Ukiona wanakuzingua, nenda moja kwa moja kiwandani au kwenye maduka ya viwanda husika. Achana na mawakala.
 
Mwaka wa 2016 nilinunua Tanfoam inch 8 5*6 kwa Tsh. 216,000. Fake ndio yapo na ili kuepuka mkenge, nilichukua kwenye Godown yao. Na bei zake japo ni inch8 5*6 zinatofautiana Kuna TANFOAM PREMIUM, TANFOAM LOLITA, TANFOAM BILA COVER nk. Msimu wa sikukuu hasa Pasaka na Christmas huwa wanatoa punguzo hadi la 25%.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…