Deus F Mallya
JF-Expert Member
- Jul 28, 2011
- 705
- 440
- Thread starter
- #21
madhara ya bangi za gerezani.
Ulivuta?
madhara ya bangi za gerezani.
Sishangazwi na coment za namna hii kwani hata vichaa huwa na vichaa zaidi yao.madhara ya bangi za gerezani.
madhara ya bangi za gerezani.
Sishangazwi na coment za namna hii kwani hata vichaa huwa na vichaa zaidi yao.
chizi anaporogwa ndo huwa hivo,msamehe
Source?
Kwa kukusahihisha ni kuwa iliyopitishwa ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si Rasimu ya Katiba.
Kuhusu kurudi kwenye katiba hii ya sasa bado ni hatari kubwa sana kwa watawala wetu kwa sababu wananchi watapoteza Political Legitimacy kwa serikali kwa sababu yapo mambo zaidi ya 200 ambayo ni lazima yabadilishwe kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.. Hapo naona maandamano makubwa kuishinikiza Serikali itekeleze madai ya Wazanzibari juu ya Muungano baada ya kuikwamisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Wengine tupo pia tutakaoandamana kudai Katiba ya Tanganyika.
Wengine tupo pia tutakaoandamana kudai Katiba ya Tanganyika.
Tanzania itakwama kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2015 kwa sababu nyingi lakini kwa leo tuiangalie hii:
Mchakato wa Katiba Mpya:
Itakumbukwa kuwa Serikali imeamua kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ambapo Waziri Mkuu alikaririwa akisema kuwa ifikapo mwaka 2014 katiba hiyo itakuwa tayari. Hata hivyo kuna vikwazo vikubwa vya kisheria na vya kisiasa kwenye sheria yenyewe iliyoweka huo utaratibu wa kuandikwa kwa katiba hiyo. Vikwazo hivyo vina nguvu ya Kuiangusha Serikali nzima kabla ya mwaka 2015; Kwanza, Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inataka wazanzibari zaidi ya 50% wapige kura kuikubali Rasimu hiyo ya katiba itakapokuwa tayari na kadhalika huko Tanzania bara.
Ukweli ulio wazi ni kuwa suala la Muungano limekuwa hadithi inayokosa tafsiri halisi kwa miaka kadhaa sasa. Hata hivyo Muungano umeendelea kukosa tafsiri halisi na ya Ukweli kutokana na usiri mkubwa unaoendelea kufichwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ama kwa kuogopa kuutibu muungano ama kwa sababu zao za 'Kiintelijensia'..
Wakati huu fukuto la Wazanzibari kudai muundo mpya wa Muungano limeshamiri hasa kwenye mchakato huu wa katiba unaoendelea hata wengine kudai kuwa Muungano uvunjwe tuanze upya.Serikali kwa sasa haina namna ya kukwepa wajibu huu wa kuwapa wananchi wake uhuru wa kuamua na kuchagua kama wanataka Muungano au la: na kama wanautaka, wanautaka Muungano wa Sura ipi. (Muungano wa sasa ni kama 'Shombeshombe'). Wazanzibari hawako tayari kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia zinazotakiwa kama bado Tanganyika itakuwa haina Katiba yake na Suala la muungano kurekebishwa.
Kukwamishwa huko kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutakuwa ni kukwama kwa Serikali mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kulinusuru hili; hata kama Serikali itaamua kuandikwa kwa katiba ya Tanganyika bado itakuwa imekwama kabla ya mwaka 2015 kwa sababu itabidi kiwepo kipindi cha mpito ambapo nchi inaweza kuongozwa na Jaji Mkuu kwa Siku 90 kabla ya uchaguzi Mkuu (Si ule wa 2015). Baada ya uchaguzi ndipo Rais ajaye aanzishe mchakato wa kuandikwa kwa Katiba ya Tanganyika na baadaye referendum ya Muungano na kisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa hapa Serikali ilipo ikienda Mbele itakwama;Ikirudi nyuma itakwama. No way Out.
Naomba kutoa hoja.
Asante kwa sahihisho. Mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa hatutakuwa na katiba mpya ifikapo 2014, kwa sababu hiyo hiyo ya 50% kutoka kila upande wa bara na visiwani. Uwezekano wa kupata hata 30% visiwani ni mdogo sana.
Sasa endapo hili litatokea, halitakuwa limeifanya nchi kukosa katiba, ila itakuwa tu imekosa katiba mpya na hivyo kuilazimu kuendelea na katiba iliyokuwepo hadi kura ya rasimu mpya ya katiba inafanyika. Kimsingi, hii inaweza tu kuiweka nchi katika kipindi kingine cha kuweka utaratibu wa kuanzisha mchakato mpya, lakini sio kuiangusha serikali, kwani wananchi ndio wameamua hayo waliyoona kuwa yanafaa kwa uhuru wao. Mie ndahani kitakachoangaliwa hapa na muda tu kuwa nini kifanyike bila kujali kuwa kuna mambo zaidi ya 200 yanayopaswa kubadilishwa. Sijui wewe unaonaje hili