Behind the Scene: Serikali itakwama Kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015

Kwa kukusahihisha ni kuwa iliyopitishwa ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si Rasimu ya Katiba.

Kuhusu kurudi kwenye katiba hii ya sasa bado ni hatari kubwa sana kwa watawala wetu kwa sababu wananchi watapoteza Political Legitimacy kwa serikali kwa sababu yapo mambo zaidi ya 200 ambayo ni lazima yabadilishwe kabla ya Uchaguzi Mkuu 2015.. Hapo naona maandamano makubwa kuishinikiza Serikali itekeleze madai ya Wazanzibari juu ya Muungano baada ya kuikwamisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Wengine tupo pia tutakaoandamana kudai Katiba ya Tanganyika.

Asante kwa sahihisho. Mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa hatutakuwa na katiba mpya ifikapo 2014, kwa sababu hiyo hiyo ya 50% kutoka kila upande wa bara na visiwani. Uwezekano wa kupata hata 30% visiwani ni mdogo sana.

Sasa endapo hili litatokea, halitakuwa limeifanya nchi kukosa katiba, ila itakuwa tu imekosa katiba mpya na hivyo kuilazimu kuendelea na katiba iliyokuwepo hadi kura ya rasimu mpya ya katiba inafanyika. Kimsingi, hii inaweza tu kuiweka nchi katika kipindi kingine cha kuweka utaratibu wa kuanzisha mchakato mpya, lakini sio kuiangusha serikali, kwani wananchi ndio wameamua hayo waliyoona kuwa yanafaa kwa uhuru wao. Mie ndahani kitakachoangaliwa hapa na muda tu kuwa nini kifanyike bila kujali kuwa kuna mambo zaidi ya 200 yanayopaswa kubadilishwa. Sijui wewe unaonaje hili
 
Wengine tupo pia tutakaoandamana kudai Katiba ya Tanganyika.

Tanganyika ipi Mkuu, ya Mjerumani au ya Mwingereza? Naona tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele, mataifa makubwa duniani yanaungana, sisi tunatengana, very strange!
 
Kwa hapa Serikali ilipo ikienda Mbele itakwama;Ikirudi nyuma itakwama. No way Out.

Naomba kutoa hoja.
....[/QUOTE]
Mkuu great thinker nimekukubali hapo ni kweli serikali ya Mhe Raisi Kikwete imegonga mwamba mbele ukuta nyuma mwamba pakutokea sipaoni !!! Ngoja waje kina Rejao na Zomba na Ritz labda watatupa njia mbadala!!! Ahsante kwa huu mtihani uliotoa unahitaji majibu!!!!

 
Katiba ya Tanganyika nimeipenda hii, Mchungaji Mtikila atakuja kusaidia!!!Sio rahisi kukimbia kivuli!!

 
Hii 50% inapatikanaje na kama suala ni 50% hawa wazee waliochoka ila madaraka wanayataka si watapitisha tu kwenye makaratasi
 
Wewe unaona kaandika bangi hapa??? Si utoe hoja za maana kupinga hilo aliloliandika badala ya kutukana, sasa aliyevuta bangi nani wewe au mtoa mada???

 
Tanzania itakwama kabla ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2015 kwa sababu nyingi lakini kwa leo tuiangalie hii:

Mchakato wa Katiba Mpya:

Itakumbukwa kuwa Serikali imeamua kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya ambapo Waziri Mkuu alikaririwa akisema kuwa ifikapo mwaka 2014 katiba hiyo itakuwa tayari. Hata hivyo kuna vikwazo vikubwa vya kisheria na vya kisiasa kwenye sheria yenyewe iliyoweka huo utaratibu wa kuandikwa kwa katiba hiyo. Vikwazo hivyo vina nguvu ya Kuiangusha Serikali nzima kabla ya mwaka 2015; Kwanza, Sheria hiyo pamoja na mambo mengine inataka wazanzibari zaidi ya 50% wapige kura kuikubali Rasimu hiyo ya katiba itakapokuwa tayari na kadhalika huko Tanzania bara.

Ukweli ulio wazi ni kuwa suala la Muungano limekuwa hadithi inayokosa tafsiri halisi kwa miaka kadhaa sasa. Hata hivyo Muungano umeendelea kukosa tafsiri halisi na ya Ukweli kutokana na usiri mkubwa unaoendelea kufichwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ama kwa kuogopa kuutibu muungano ama kwa sababu zao za 'Kiintelijensia'..

Wakati huu fukuto la Wazanzibari kudai muundo mpya wa Muungano limeshamiri hasa kwenye mchakato huu wa katiba unaoendelea hata wengine kudai kuwa Muungano uvunjwe tuanze upya.Serikali kwa sasa haina namna ya kukwepa wajibu huu wa kuwapa wananchi wake uhuru wa kuamua na kuchagua kama wanataka Muungano au la: na kama wanautaka, wanautaka Muungano wa Sura ipi. (Muungano wa sasa ni kama 'Shombeshombe'). Wazanzibari hawako tayari kuipitisha Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia zinazotakiwa kama bado Tanganyika itakuwa haina Katiba yake na Suala la muungano kurekebishwa.

Kukwamishwa huko kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutakuwa ni kukwama kwa Serikali mapema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kulinusuru hili; hata kama Serikali itaamua kuandikwa kwa katiba ya Tanganyika bado itakuwa imekwama kabla ya mwaka 2015 kwa sababu itabidi kiwepo kipindi cha mpito ambapo nchi inaweza kuongozwa na Jaji Mkuu kwa Siku 90 kabla ya uchaguzi Mkuu (Si ule wa 2015). Baada ya uchaguzi ndipo Rais ajaye aanzishe mchakato wa kuandikwa kwa Katiba ya Tanganyika na baadaye referendum ya Muungano na kisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa hapa Serikali ilipo ikienda Mbele itakwama;Ikirudi nyuma itakwama. No way Out.

Naomba kutoa hoja.

Yetu macho. Hoja imetulia
 
Asante kwa sahihisho. Mimi ni miongoni mwa wanaoamini kuwa hatutakuwa na katiba mpya ifikapo 2014, kwa sababu hiyo hiyo ya 50% kutoka kila upande wa bara na visiwani. Uwezekano wa kupata hata 30% visiwani ni mdogo sana.

Sasa endapo hili litatokea, halitakuwa limeifanya nchi kukosa katiba, ila itakuwa tu imekosa katiba mpya na hivyo kuilazimu kuendelea na katiba iliyokuwepo hadi kura ya rasimu mpya ya katiba inafanyika. Kimsingi, hii inaweza tu kuiweka nchi katika kipindi kingine cha kuweka utaratibu wa kuanzisha mchakato mpya, lakini sio kuiangusha serikali, kwani wananchi ndio wameamua hayo waliyoona kuwa yanafaa kwa uhuru wao. Mie ndahani kitakachoangaliwa hapa na muda tu kuwa nini kifanyike bila kujali kuwa kuna mambo zaidi ya 200 yanayopaswa kubadilishwa. Sijui wewe unaonaje hili

Mkuu ikiwa itashindikana kupata hizo 50% kutoka pande zote ua mmoja wapo ni bora katiba iliyopo ikaendelea kutumika tukaingia kwenye uchaguzi na katiba hii hii!! Baada ya uchaguzi tutaendelea na mchakato wa katiba mpya, hapo sasa yataangaliwa mambo yote kama ni kuanza na katiba ya Tanganyika nafasi itakuwa imepatikana ya kufanya hivyo!!!

 
Back
Top Bottom