Beauty pageants - T/Bara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Beauty pageants - T/Bara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Jan 31, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Je huu ni utamaduni wa Kitanzania inajulikana wazi kuwa katika zoezi hili la beauty pageants (Miss ?) mambo yanayotazamwa ni mengi na ya aibu au haya yanawafurahisha vigogo wetu na viongozi wetu ambao ni miongoni mwa waumini wa Dini ambazo naamini kabisa hakuna hata moja inaloliona jambo hilo kuwa linafaa katika jamii na hasa jamii yetu ya KiTanzania kwani tunajijua tunapotoka.
  Ingawa sina uhakika lakini nasikia huwa mwanamke anapekuliwa kila kona na zaidi awe hajaolewa ndio huweza kupata ushindi,au bunge limeridhia kitendo hiki eti kuijulisha Tanzania nchi za Nje ,Zanzibar wamepiga marufuku kufanyika. Tanzania wameruhusu Zanzibar marufuku
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha ..unajua unanikumbusha mbali sana mzee Mwiba.

  Kipindi kile cha awali kuna mashindano fulani yakihusisha wasichana (kitaalam, walimbwende) kutoka sehemu zote Tz. Yule msichana kutoka ZnZ alipigwa stop na SMZ kushiriki.

  Yule waziri wa SMZ aling'aka sana na mwishowe, huku akiwa amekabwa na jazba alisikika akisema, nanukuu, " huyu msichana kama ni mrembo mbona hajaolewa mpaka sasa sasa ?" Kwa maana nyengine kwa kigezo cha SMZ, hakuna mrembo ambaye hajaolewa..teh :D teh :D teh :D

  Kaazi kweli kweli..
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Kaazi kweli kweli, sijui kuna nini zaidi hapo, urembo, kuolewa, ud...?
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  http://www.thisday.co.tz/images/main.jpg[/IMG
  State House Chief Secretary Philemon Luhanjo,(Top) and Home Affairs Minister Lawrence Masha.

  Sasa nenda kwenye gazeti la Thisday umuone Luhanjo.Huo ni uzembe wa kuajiri watu wasio na uwezo wa kujua mambo yatafika wapi,tumetafuta habari za warembo ambazo ni aibu kwenye jamii yetu,umasikini wetu wa ndugu zetu ndio viongozi wachache wanaojitajirisha kwa kutumia jamii yetu katika mambo yasiyopendeza,jamii inapotea sana kuhusiana na mikasa ya hawa tunaowaiita warembo.Faida ni kwa wachache lakini hasara ni kwa wengi.Luhanjo anaweza kulishitaki gazeti kuwa limemzalilisha na akadai mabilioni,watu wachache wanatia hasara Taifa.
  Ila ukweli bado utabakia kuwa jamii inapelekwa kwenye mambo ambayo hayana utamaduni nayo si yetu.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Muzee Mwiba,

  Hii picha mbona naona maluweluwe? Au macho yangu yana matatizo siku hizi?
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nenda hapo ukaione kama bado ipo ThisDay umuone Luhanjo na mkokoteni pale juu nimondoa ile ] ya mwisho kwani ni picha pana sana.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..kuna mambo mengi sana yanakera Tanzania. mojawapo ni haya mashindano ya urembo. mapesa yanayotumika, pamoja na muda unaopotezwa, huko yangeelekezwa kwenye ELIMU Tanzania ingekuwa mbali sana.

  ..kwanini pesa zinazotumika mijini ktk mashindano ya urembo zisielekezwe vijijini kukampeni ili watoto wa kike wazingatie masomo?

  ..zaidi kuna Kocha wa Mpira Maximo. naambiwa mshahara wake ni USD 15,000 kwa mwezi!! tunamlipa mapesa yote hayo halafu tunashindwa kuifunga timu ya Somalia.
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jan 31, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hivi Tanzania tuna utamaduni mmoja tu? Kama upo mmoja, huo utamaduni ndo ukoje?
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwani ukisikia utamaduni wetu akili yako inakwambia ni kitu gani?Au hili neno utamaduni wewe unalifikiria ni nini?
   
 10. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  NI mawazo ya kizamani kusema eti u-miss ndo inaleta uhuni na vitu kama hivyo. Kama mwanamke anajiamini na yuko tayari kupima uzuri wake na wenzake kuna ubaya gani? And it is a form of entertainment! Kama msichana akiamua kuwa model na kutengeneza pesa kama Alek Wek na wanawake wengine wa kiafrika kuna ubaya gani?
  Ni matatizo ya kuwa tuna mfumo dume unaoamua kwamba eti utamaduni wetu utakuwa determined na wanaume tu.
  Mi binfasi sipendi kusikia unafiki wa watanzania unaosema eti urembo si utamaduni wa mwafrika. Kwani kuogelea katika olimpiki ni utamaduni wa mtanzania? Come on! Dunia imebadilika na kila mtu anajaribu kutafuta njia ya kuishi. We have no right to deny any citizen that right.
  Mi nakumbuka miaka ya 70 akina dada zetu walikuwa wanakamtwa na polisi eti wamevaa nguo fupi mini sketi. Ni unafiki wa hali ya juu wakati mababu na mabibi zetu walikuwa wanatembea nusu uchi. Huu ndo utamaduni wetu wa asili na ni ukoloni ndo ulileta Victorian values za kuvaa magauni marefu na suruali! Tuache unafiki!
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Nyani, unajua unacho nifurahisha ni kwamba sometimes una observation nzuri sana. Isingekuwa mapenzi yako kwa Mccain na Limbaugh.... anyway tuyaache hapa hayo....
   
Loading...