Alhabiby GS,
Prof anashindwa kutofautisha baina ya MAU MAU na MAJI MAJI.
:heh: :heh:
Shukran Kaka na tuko pamoja kwa saana! Nimekusoma na nimekufahamu kwa utuvu mwingi mno, japo Bwana Hirji asipofanza tahadhari basi aezageuka yakua Professor of comedy....yaani mtaalamu wa dhihaka na mas'khara!? Daah! Teeh! Teeeh!
Yaani ukasoma kwa undani ile critique ya huyu mwanataaluma Bwana Hirji...basi utayaona mapungufu mangi kiasi...kuliko hata yale anayojaribu kuyatolea yeye mapungufu! Daah!
Mfano kiduchu, yaani jinsi ile mojawayapo ya premise yake alofanza na ile mifano na kushabihisha alikofanza...basi haina tafauti na labda na Mwanamke anaekwenda lalama kwa mwenyekiti wa kitongoji kukhusu domestic violence zinazomsulubu...lakini anapewa majawaba yakua, wee endelea kustahamili tu, maana hilo ni tatizo lenye kuwasulubu wanawake wanzio takriban woote wa kitongoji hiki!? Duuh!
Yaani nalistaajab mno, kumsoma Dr Hirji akijiweka penye level ya chini kiasi kile...tena huku ati aki-justify kwa kutuekea zile triangular excuses/explanations za mifano ya pale Amerika and USA, sexism na mangineyo... na hata kuthubutu kufananiza history zisolingana kwa mangi, ili tu kuandika na kutetea mfumo mbovu uloasisiwa,kusimikwa na kurithishwa Taifa letu changa toka kwa yule "Baba Taifa"! Daah! Yaani Hirji kwa hili simlaumu mno, maana yeye na genge lake wanafahamika yakua ni Nyereres' apologists!
Jangine muhimu zaidi...yeye Dr Hirji kabla ya kufungua mdomo wake na kuwaasa wangine waache kulalama...yatakiwa pia yeye kama Tanzanian with Indian Sub Continent background...ni priviledges na social favours zipi walifaidika nazo tangia zile nyakati za Wakoloni dhdi ya wale Natives/Indigenous...japo kwa hizi never ending political correctiness zilotamamalaki hivi sasa hunu duniani...hii yaeza kuchukua tone ya racism au hata discrimination...lakini soote twafahamu yakua hii ni reality itokayo ndani ya historical facts!
Yaani Dr Hirji, yatakiwa awe cautious japo kiduchu anapofungua mdomo wake hadharani...khasa ukazingatia yakua yeye na society yoote ya Asians with Indian Sub Continent background wamepata/wamefaidika na priviledges/social favours, na kuekewa ile safety net tangia zama za ukoloni na haikua tafauti kubwa mno hata baada ya uhuru! Sasa ataezaje yeye kuthamini amma kuyatambua kwa kina matatizo na nakma za Natives Muslims, Animists or even Christians!?
Nakhis tafauti kubwa hapa yajionyesha kuwa...yeye Prof Hirji anatumia tu zile academic theories ku-justify maandiko yake amma kwa hapa hiyo critique yake! Lakini yeye mwenyewe anafahamu yakua hata zile socialist ideology alizokua akifuata na kujinasibu nazo tangia zama zile, ilikua ni kama hobby au ile intelectual luxury tu!
Sasa, yeye Dr Mohamed Said History anayoizungumza ni yakua ameishi history hiyo...yaani ana ile social,political and blood connection ya hizo harakati za mapambano ya kuleta Uhuru wa Taifa letu!
Hao baadhi ya hata walokua wanaharakati wakuu/mashuhuri zama hizo au anaowazungumza penye mangi ya maandiko yake...basi kwa njia moja amma nyangine pia walikua ni jamaa zao...yaani kwa lugha za kisasa nafikiri mwaita ndo ile "family friend"!?
Yanilazim kugura hapa kwa muda...tajitahidi labda kurejea tena kesho!
Ahsanta sana!