Mwanakijiji,
Mimi nimekuja na historia ambayo si wengi walikuwa wamepatapo
kuisikia.
Haikuwepo kabisa.
Nimeeleza historia ya Tanu toka African Association na waasisi
nimewataja kwa majina: Kleist Sykes, Ibrahim Hamis, Zibe Kidasi,
Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Raikes Kusi, Mzee bin Sudi,
Rawson Watts na Cecil Matola.
Nimeeleza historia ya miaka michache kabla ya kuundwa kwa Tanu
kulikuwa na harakati zipi.
Hadi
Nyerere kafika na kupokelewa na
Abdul Sykes.
Sasa hapa ndipo penye maneno.
Hii kumuunganisha
Nyerere na
Abdul likawa tatizo kubwa.
Sina haja ya kujirudia.
Kazungumza
Prof. Hirji kuhusu Meru Citizens Union ya akina
Kirilo na
Sablak hii ni 1952.
Abdul Sykes ndiyo aliowaunganisha na
Earle Seaton kutengeneza
petition kwenda UNO kuhusu ardhi yao waliyodhulumiwa na Wazungu.
Abdul ndiyo aliyempokea
Kirilo Dar es Salaam na kumsaidia kupata
pasi ya kusafiria. Kazungumza
Prof. Hirji siasa za Usukumani.
Hii ni 1952 pia
Abdul kenda hadi Mwanza kuonana na
Paul Bomani
kuunganisha nguvu.
Prof. Hirji kama anaweza aje na kitabu anikamate uongo.
Soma hapo chini nini Wakoloni wanasema:
"Tanganyika Political Intelligence Summary, March 1952":
"...it is reported that the Secretary of the Association,
Abdul Wahid
Sykes has dispatched letters to all branches asking members for
suggestions under the following heads for a memorandum to be
prepared for the Royal Commission..."
...
Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association
who, as reported in last month's summary (paragraph 20) was going
on safari up country, visited Mwanza, where he met
Paul Bomani,
President of the Bukoba African Association, and accompanied him to
Bukoba.
Sykes then visited Kampala alone.....on 8[SUP]th[/SUP] March, a secret
meeting was held, attended by leading members of the Mwanza Branch...
(Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya
kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti
yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.)
Kusubiri mtu kaandika na wewe ukaja kupiga "critique" kila mtu anaweza
na hili
Prof. Hirji analijua.
Kushoto: Abdulwahid Ally Sykes na Mwandishi Nyumbani kwa Japhet Kirilo Usa River 1989 wakati wa utafiti