Beatification of Lowassa starts here

Beatification of Lowassa starts here

Aaah! Lowasa kaza buti mwanangu in way iwe kwa Mungu au kw sangoma upresdent lazima upatikane.
 
Haya makanisa bwana! mtu akisali Tanzania hapati baraka, Mungu anasikia na kutoa baraka kwa wanaosali Nigeria, Irael ....tu? anyway ni haki ya kila mtu kuabudu tuheshimu katiba lakini inatia shaka.

Kwa kina Rwakatale kuna baraka kweli?
 
Kwa kina Rwakatale kuna baraka kweli?
Inawezekana si unaona anavyokula vichwa huku akifanya biashara ya Bajaj na kubadili shule alizoombea msaada kuwa ni za yatima na kuzigeuza za kutoza mamilioni ya fedha huku akiwatimua yatima na nyingine kuzigeuza vyuo vya ualimu na sasa anataka kiwe Chuo Kikuu pale Tabata. Hawa ndio Manabii wetu na uyoga wa makanisa yanaojiotea nchini na Nigeria.
 
Njia nzuri ya kuonesha kwamba wewe ni muaminifu ni kuwa karibu na Mungu. Ndio maana matapeli wengi huwa wanatumia mgongo wa dini kufanya utapeli wao.

Wote hao waende makanisa au miskitini lakini ukweli ni kwamba maovu yao kwa watanzania ni kutokana na kupoteza imani kwa Mungu. Huyo ataenda sana huko Nigeria na wengine watafturisha sana lakini sidhani kama wataweza kutushawishi kuwaamini tena.
 
Mzee wa Kanisa Azania Front naona siku hizi hakauki kwa nabii wa Nigeria. Najiuliza sijui anawapa ujumbe gani maaskofu wetu hapa nchini?
Huko ni kutanga tanga kwa mfa maji. hapa bongo injili inatwangwa hadi mapepo yanatoka. Nigeria watu wanamakanisa yanayotumia nguvu za Giza unaenda tafuta nini? Msizikubali kila roho, zijaribuni na kuzipima, asema bwana wa majeshi.
 
watu bwana, akiharibu tabu, akitengeneza tabu.Endeleeni tu kunyooshea vidole watu.
 
Nampongeza sana Mh. Lowasa, maana mbingu ipo kwa ajili ya waovu endapo watatubu na huwezi kutubu kama haujaonesha nia ya kumtafuta ikiwa ni pamoja na kudumu katika ibada na kujifunza jinsi ya kuenenda maisha mapya.
 
Manabii uchwara, makanisa uchwara na mahubiri uchwara yaliyozingirwa na nguvu za giza.
 
Wakati muda huu Watanzania wenzetu wakipiga kura zao kumchagua Mbunge mpya jimbo la Igunga; Mhe. Edward Lowassa yuko ndani ya Synagogue Church of All Nations (SCOAN) Kwa TB Joshua, jijini Lagos Nigeria muda huu.

Source: Emmanuel TV, Sunday Live Service.

Na mesasge ya TB Joshua leo ni "Overcome your Doubt"

Hivi kama akihudhuria ibada inayoongozwa na Askofu Thomas Laizer hawezi kupata hicho anachokifuata kwa TB Joshua?

Btw, hivi msipomtaja fisadi lowasa hapa JF huwa mnapungukiwa nini? Manake kila uchao ni lowasa lowasa, kha!
 
Hii ndio faida ya kuwa mtu maarufu. Ungekuwa wewe ndio uko Ngeria nani angehangaika kukuanzishia thread kwanza tusingejua kwamba wewe ni mbongo au Mnigeria coz hakuna mtu anayekufahamu. Lakini EL anameuza sura kidogo tu kwenye chupa watu wakang'amua yuko kwa fake prophet Lagos.
 
Ni kweli mkuu fisadi lowasa ni celebrity bongo kwahiyo kutajwa tajwa ni jambo la kaiwada sana.

Tatizo langu hapa naona kama kuna watu wanakula posho kwa fisadi lowasa kila wanapoanzisha thread za kumhusu,kuna vitu vingine wala havihitaji public attention kiasi cha kuvipost hapa JF.
 
ana mahangaiko huyu mmasai.. Kwa waganga yumo, kwa Yesu yumo, sijui tumueleweje? Popoooooooooooooooo........

Lowassa sio mmsai mkuu. Nchi hii imekuwa na wamaasai mawaziri wawili tu tangu uhuru, Sokoine na Ole Nangoro, mbunge wa kiteto. Lowassa ni mmeru/muarusha tu huyu ila amekulia umasaini
 
Kwahiyo mungu yupo lagos?
mungu hayupo bongo?
Damn, sasa nimeenda church kufanya nini leo.
Naombeni schedule ya Mungu basi, mimi sina $ 1500 za kumfuata mungu Lagos bana.
jamani naomba tusimuhukumu kwa kuwepo huko hiyo ni haki yake kumtafuta Mungu pale unapoamini.
 
Lowassa sio mmsai mkuu. Nchi hii imekuwa na wamaasai mawaziri wawili tu tangu uhuru, Sokoine na Ole Nangoro, mbunge wa kiteto. Lowassa ni mmeru/muarusha tu huyu ila amekulia umasaini
Kumbe......sikujua hii!
 
Ni kweli mkuu fisadi lowasa ni celebrity bongo kwahiyo kutajwa tajwa ni jambo la kaiwada sana.

Tatizo langu hapa naona kama kuna watu wanakula posho kwa fisadi lowasa kila wanapoanzisha thread za kumhusu,kuna vitu vingine wala havihitaji public attention kiasi cha kuvipost hapa JF.

Hawatafanikiwa kumsafisha mtu mwenye uchafu kwa kufanya cheap publicity, wanatakiwa wamshauri ajisafishe mwenyewe by revealing the truth, Watanzania wa leo si wale wa enzi za ewala Bwana. Hija ya Israel haikutosha sasa kwa Tapeli Joshua, Nguvu ya fedha haizidi nguvu ya akili na utashi.
 
Wakati muda huu Watanzania wenzetu wakipiga kura zao kumchagua Mbunge mpya jimbo la Igunga; Mhe. Edward Lowassa yuko ndani ya Synagogue Church of All Nations (SCOAN) Kwa TB Joshua, jijini Lagos Nigeria muda huu.

Source: Emmanuel TV, Sunday Live Service.

Na mesasge ya TB Joshua leo ni "Overcome your Doubt"

Pamoja na kwamba huyu jamaa na shutuma nyingi lakini mi nikadhani kwenda kwenye ibada ni mambo binafsi sana. Hiyo ni exposition yake mbele ya Mungu wake ambayo hatuna sababu ya kuijadili sana labda tuwe tumeamua kuingilia mambo binasi ya watu. Nathubutu kusema kuwa mleta uzi ameteleza kutuletea maisha binafsi ya watu ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa. Ungetuambia amerudisha chetu ingekuwa poa na sio kaenda kusali ebo.
 
Wakati muda huu Watanzania wenzetu wakipiga kura zao kumchagua Mbunge mpya jimbo la Igunga; Mhe. Edward Lowassa yuko ndani ya Synagogue Church of All Nations (SCOAN) Kwa TB Joshua, jijini Lagos Nigeria muda huu.

Source: Emmanuel TV, Sunday Live Service.

Na mesasge ya TB Joshua leo ni "Overcome your Doubt"

Jamaa kajipanga ile mbaya...hakuna cha TB Joshua wala nini..akili za wabongo hazitabadilika...
 
Back
Top Bottom