BBC waianika Tanzania tena!


Hawa waandishi wetu vyombo vyao havina fedha za kutosha kuwapa wakina Manyerere kufanya utafiti kama huo wa BBC mara nyingi hela zao hutolewa na balozi mbalimbali kupitia jumuiya zao kama LEAT na wanaoenda kwenye hizo tafiti wengi ni bure kichwani.
 
Wacha unafki jana hata mimi nilikuwa nawatch ile habari aliyekuwa anahojiwa ni Salim Kikeke ambaye anaijua Tanzania vizuri sasa kama kasema watoto wanateseka katika ajira za utotoni isisemwe kwa hiyo?
 
Kwani siyo kweli? Na kwa jina maarufu wanaitwa "nyoka". Je wajua kwa nini wanaitwa nyoka? Ni kwa sababu wanaweza kujipenyeza pale ambapo mtu mzima naweza kupenya na malipo au ujira wao ni mdogo kulinganisha na kuajiri mtu mzima. Ni unyanyasaji wa hali ya juu Bwana Manyerere. Tunajua watoto wana shida na wanahitaji kutafuta ili waweze kuishi, lakini wachimba madini au wenye migodi wasitumie unyonge huo kuwanyonya na kuwatumikisha katika hali duni bila vifaa vya kinga kwa ajili ya afya zao ambazo hazijakomaa kuvumilia mateso wanayopitia
we manyerere wewe
 

Huwa namshangaa anavyojifanya eti mtetezi wa sera za Mwalimu wakati yeye hayaishi maisha yale ya ujamaa namshangaa sana, na mara nyingi yeye huwa anaitetea serikali na hii ni kutokana na kuwa yupo kundi la wale wafalme wasaka urais
.
 

Toka ufanye featuring na Joseph Ludovick kwenye ule gaidi aliofanyiwa Kibanda, akili zako zilikufa kabisa, sijui unajaribu kutetea nini?
 
The Boss, hujui kitu. Watoto wapo nje wanaokota tu. Hakuna anayeingia shimoni. Nimekaa miezi miwili pale sikuona mtoto "nyoka" akizama chini. Wanaozama ni wana-apollo.

Hawa watoto wapo nje eh? Kwa vile wewe ni mhariri usijifanye unajua kila kitu.

Wengine are just common people on the street lakini wanajua zaidi ya hata vyombo vya habari.

Ziko mpaka video zinaonyesha watoto wakiwa ndani ya mashimo halafu wewe unadai watoto wapo nje wanaokota tuu.

Manyerere Jackton ni hatari kwa watoto wa Tanzania. The video speaks itself unless uniambie ni feki.


cc The Boss, Mwananchi, theki, Kitaturu, Ben Saanane, OLESAIDIMU, Katavi
 
Last edited by a moderator:
EMT huyu jamaa ni mweupe mno hajui hata BBC ina operate vipi..yeye anafikiri BBC ni sawa na IPP MEDIA au DAILY NEWS.....anaaandika out of assumptions bila kujifunza........halafu huyu ni editor sasa ....jiulize mtu wa mtaani atakuwaje........
 
Last edited by a moderator:

Shukrani sana mkuu EMT umeongea jambo moja muhimu sana kuwa "wanadhani wanajua" kumbe ni kwa kuwa tu wao wanaandika na kutangaza na hakuna jinsi ya kujibu papo kwa
papo!!!!!!

Sasa imagine hii ingekuwa habari gazetini wangapi wangechukua kama yalivyo!!!?????
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wewe ulikua unachimba wapi ambako hukuona watoto?kijiji au kwa mzungu?na kama ni kijiji ni mgodi gani?maana hata mimi nina experience ya kutosha hapa,watoto wanapolo wapo na wataendelea kuwepo,Kwa mzungu pia nimefanya block zote,kweli kwa mzungu watoto hamna lkn kwa wachimbaji wadogo watoto bado wapo.
 
huu ni ukweli kabisa BBC wamesema na wanaitwa Nyoka!

Hili si swala la kubisha kabisa!
 
watoto wanashuka chini kawaida me ni apollo mtoto ni nyoka wa kirenga tena anaspidi kuliko anashusha nakupandisha tindo haohao nyoka wako waliobaatika na wana maisha yao
Hata Kazandula hapo nimewahi kuwaonana watoto ma nyoka kibao tu wa A-town, na Moshi
 
EMT huyu jamaa ni mweupe mno hajui hata BBC ina operate vipi..yeye anafikiri BBC ni sawa na IPP MEDIA au DAILY NEWS.....anaaandika out of assumptions bila kujifunza........halafu huyu ni editor sasa ....jiulize mtu wa mtaani atakuwaje........

On a lighter note, British journalist Alan Brien: Newspapers' "editors are like madams - soothing, flattering, disciplining their haughty temperamental staff, but rarely obliged to satisfy the clients between the printed sheets."
 

Kwani sio kweli?
 
Ndo yale yale ya Darwin's Nightmare ya mapanki, watu wanaandamana hawali mapanki kumbe watu tunakula balaa kisa mtoa filamu ni mfaransa.Hao BBC wasichoke kuumbua maana waandishi wetu wengi ni makanjanja kama alivyosema Ridhiwani.

Mkuu umeanza vizuri sana,lakini hiyo RIDHIWANI toa iyo.
 
Ah..!! Wewe usingeweza kuandika. Acha BBC waandike na ikibidi wawachore tu.
Kwa hisia na mapenenzi yako unadhani kazi ya 'nyoka' ni nini pale?
unadhani ni kwa nini waliitwa nyoka?
 
Hii inadhihirisha kuwa Uingereza hawakuwahi kufurahi kuiachia Tanganyika iwe huru, wanatamani wangeendelea kututawala mpaka kiama, wivu wa rasilimali wameona njia pekee ni kutuchafua..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…