BBC: Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti ya Human Rights Watch

Mamlaka nchini Tanzania imezuia uzinduzi wa ripoti kuhusu unyanyasaji wa wafanyikazi wanawake kutoka taifa hilo wanaofanya kazi katika mataifa ya Uarabuni.

Shirika la Human Wrights Watch limedai katika matokeo yake kwamba wafanyikazi wa nyumbani kutoka nchini Tanzania walikuwa wakibakwa , kuteswa na kulipwa mishahara duni na waajiri wao katika mataifa ya Uarabuni.

Ripoti yenye kurasa 100 inayodai kuteswa kwa wafanyikazi wa nyumbani wa Tanzania nchini Oman na muungano wa mataifa ya Emirata UAE ilitarajiwa kutolewa leo kwa waandishi wa habari mbele ya waathiriwa lakini hilo halikufanyika.

Katika hatua isiokuwa ya kawaida ,afisa mmoja kutoka shirika linalofadhiliwa na serikali la Sayansi na Teknolojia COSTEC William Kindekete alifutilia mbali mkutano huo katika mji mkuu wa Dar es Salaam akisema kuwa wanaharakati wa shirika hilo la haki za kibinaadamu hawakufuata sheria katika kufanya utafiti wao.

Hatahivyo matokeo ya utafiti huo wa HRW unaonyesha kuwa takriban wanawake 50 walihojiwa wakati wa utafiti huo ambao wanadai kwamba walilazimishwa kufanya kazi kwa kati ya saa 15 na 21 kwa siku huku wakipokonywa pasipoti zao na waajiri wao punde tu walipowasili katika mataifa hayo.

Ripoti hiyo ilibaini zaidi kwamba zaidi ya nusu yao hawakulipwa huku wengine wakisema kuwa hawakulipwa kabisa.

Wawili kati ya watano walidai kupigwa mbali na kunyanyaswa kijinsia.

Ripoti hiyo ya HRW pia inasema kwamba balozi za Tanzania katika eneo la Ghuba hazikutoa usaidizi wowote kwa waathiriwa wakati walipotaka usaidizi

Juhudi za kupata majibu kutoka kwa serikali ya Tanzania hazikufanikiwa kwa kuwa maafisa wengi hawakuwa tayari kuzungumzia swala hilo
Pascal Mayalla
 
Hawa human right watch nao wehu tatizo limetokea Oman halafu ripoti mnazindulia Tanzania kwa kiswahili hao waoman wataelewa kweli
CONSUMERS WA REPORT NI OMAN AU TANZANIA? HUJAHUDHURIA TAFITI (STUDY AREA) ZILIZOFANYIKA NJE YA TANZANIA LAKINI PRESENTATION/DEFENSE ZIKAFANYIKA TANZANIA? MUHIMU HAPO NI KUJUA NANI NI MLAJI MKUU WA HIYO REPORT
 
CONSUMERS WA REPORT NI OMAN AU TANZANIA? HUJAHUDHURIA TAFITI (STUDY AREA) ZILIZOFANYIKA NJE YA TANZANIA LAKINI PRESENTATION/DEFENSE ZIKAFANYIKA TANZANIA? MUHIMU HAPO NI KUJUA NANI NI MLAJI MKUU WA HIYO REPORT
Tanga Kwenu si dhsni kama uko sahihi hoja ya fafiti si kuzuia watu kwenda kufanya kazi Oman bali Oman waacha kunyanyasa wafanyakazi wageni- watenda kosa na watendewa kosa wote wako Oman SASA HRW wanaleta kelele hapa- good work out of place
 
Kama tungekuwa na Jeshi lenye nidhamu na lenye upendo wa hili taifa, CCM ingekuwa History kitambo.

karibu wakubwa wote huko ni makada wa ccm. it will take time mpaka makada wastaff huko jeshinj kumbuka mageuzi yameanza miaka ya 90. so tutegemer mpaka kwenye 2030-40 tutakuwa na jeshi lisilo na makada.
 
Zama hizi za mtandao waiweke mtandaoni tu, mbona tushasikia dondoo BBC World Service tayari?

The East African lilifungiwa lakini watu wakasoma mtandaoni, itakuwa ripoti?
 
Hakuna haja ya kuzuia uzinduzi wake . Bora ukweli usemwe ili waarabu wajue kuwa tunajua matendo yao
Swala sio ukweli. Kila kitu serikali inajua na inafangia kazi swala kama ni tafiti kwa nini haikufuata taratibu inayotakiwa? Huwezi ingia nchi ya watu na kufanya utafiti bila kuhusisha taasisi zinazohusika na tafiti. Je unajua mtafiti anaelimu gani? Je njia anayotumia inaweza toa jibu sahihi ya tatizo? Ni maswala ya kiitaalamu na sio siasa
 
Back
Top Bottom