May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,162
- 8,820
Mimi ni miongoni mwa wasikilizaji wa redio mbalimbali hapa nchini, miongoni mwa hizo ni BBC SWAHILI kupitia washirika wao. Si kwamba wanachonikwaza wao hakitokei kwenye redio nyingine la hasha ila naangalia na ukubwa wa shirika husika.
Hakuna shaka kuwa sehemu kubwa ya Wasikilizaji wa Kiswahili wanapatikana Tanzania, sasa Mtangazaji anapoleta taarifa kutoka Rwanda, na kusema "bei imepanda kutoka faranga elfu moja mpaka elfu tatu" mimi Mtanzania hapo naelewa nini?, najuaje hiyo bei kweli ni kubwa kwa kulinganisha na bei ya nilipo?. Kwa nini mnapotaja pesa za nchi nyingine msimsaidie Msikilizaji wenu kuelewa...kwa mfano mngeweza kulinganisha na shilingi au dola ya Kimarekani ambayo walau inatumika kwa kila nchi ya EAC...ili nami nitafanya hisabati kujua huo ughali ukoje.
Au wakati mwingine Mnamuhoji, kwa mfano raia wa Jamuhuri ya Congo, raia ataunga unga kiswahili hapo alafu Mtangazaji (Lubunga Byaombe au mwingine) atapokea na kuendelea na matangazo kana kwamba kila kitu kilichoongelewa na Raia huyo kimeeleweka, na wakati mwingine huwa najua kabisa kuwa hata wao Watangazaji hawajamuelewa huyo Mzungumzaji.
Sasa huwa najiuliza ni kwa vipi hamuoni haja ya Msikilizaji wenu kuelewa kila taarifa mnayoitoa?.