Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

HS CODE

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
1,784
Reaction score
4,413
Wakuu! Naomba nitumie salamu zilizo zoeleka zaidi visiwani, “Hamjambo?”, “Mumesalimika?”.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Pamoja na mateso yote wanayopitia waliotumia muda mwingi mashuleni ambao kwa sasa wamezagaa kila kona ya taifa hili, kiasi cha baadhi kuwatafsiri kama wamepoteza uelekeo, ndugu zangu aliyesoma kasoma.

Afadhali ya yeye anayeteseka muda huu, lakini matumaini ya kesho yake kubadilika ghafla ni makubwa.

Fikiria mtu ambaye ajira zote zinazotoka iwe ni taasisi nyeti au taasisi yoyote ya serikali au binafsi yeye hazimuhusu kwa sababu hajasoma.

Ni bora aliyesoma anaweza kufanya hata kazi za asiyesoma kuliko asiyesoma ambaye kazi za aliyesoma hazimuhusu.

Ni rahisi zaidi kwa aliyesoma kuishi maisha ya ahueni, yaani kati kwa kati sio chini wala sio juu kuliko asiyesoma, asiyesoma akipigika anapigika kweli.

Najua pande zote mbili zina sumu kali sana, na zinatafuta pakuzitemea. Nawakaribisha kwenye huu uzi, zitemeeni hapa. Bila kujali umesoma au hujasoma, unaweza kukaa upande wowote.

Ama namna gani, wewe unaonaje?

Asante.

MUHIMU
Kuendana na uzi huu, msomi ni mwenye elimu ya fani kwa angalau ngazi ya Cheti.
 
Amna maumivu makal kwa mtu aliyesoma af akakosa ajira cio powa

Uko sahihi sana, lakini Mkuu elimu ina manufaa zaidi ya kuajiriwa. Au wewe unalitazamaje hili?
 
Waliosoma ndo wanatutoza tozo hivi si watafute namna nyengine sahivi imebaki tozo ya malimbwata tu!

Hahaha, inawezekana wanazo hoja za msingi kutetea kwanini watutoze.
 
Kikubwa ni akili za maisha tu na bahati (nyota)

Ni sawa Mkuu, lakini huoni kama mtu akiwa amekwenda shule angalau anakuwa amezinoa vizuri akili zake za maisha kuliko asiyesoma?

Kuhusu bahati, mtu akifanya kazi kwa kutumia akili iliyojengeka vizuri na akawa na bidii mara nyingi ni lazima atakuwa na bahati.
 
Achana na hizo ligi tafuta pesa,mishaara yenye ya mbuzi ety degree ya elimu take anachukua chini ya laki 6 c utaahira huo

Hahaha, aliyesoma anaweza pia akajiajiri na kujipangia yeye mwenyewe ajilipe kiasi gani.
 
Tukija kwenye uhalisia wa maisha ya kupambana

Aliyesoma hawezi kupambana mpaka akafika hatua akatoboa.

Kwa sababu atakuwa anaona aibu kujichanganya na hata baadhi ya watu.

Pona yake apate ajira.

Hahaha, Mkuu kwanini unasema hawezi kupambana mpaka kufanikiwa! Hata hivyo suala la kuona aibu mbona hata wasiosoma wapo wenye aibu na wanaochagua kazi!?
 
Ukiachana na ben Carson niambie mtu mweusi ambaye anasifika Duniani kutokana na matumizi ya elimu yake! Jibu ni hakuna wala hatokuja kutokea.
 
Achana na hizo ligi tafuta pesa,mishaara yenye ya mbuzi ety degree ya elimu take anachukua chini ya laki 6 c utaahira huo
Mpaka hapa tushajua upande wako....swala siyo unalipwa mshahara kiasi gani bali unaitumiaje elimu yako kukupatia pesa nje na ajira za serikali
Hata hivyo huku kwetu wwana ambao waliukimbia umande wana hali mbaya sana kimaisha tofauti na waliosoma
 
Mpaka hapa tushajua upande wako....swala siyo unalipwa mshahara kiasi gani bali unaitumiaje elimu yako kukupatia pesa nje na ajira za serikali
Hata hivyo huku kwetu wwana ambao waliukimbia umande wana hali mbaya sana kimaisha tofauti na waliosoma
Kwa elimu ipi ya bongo inayofundisha kutumia elimu yako kupata pesa nje ya ajira? Elimu yetu hii tuliyofundishwa kukalili na sio kukabiliana na changamoto ya ajira?
Tumeandaliwa kusoma ili tuajiriwe na sio vinginevyo vijana wengi tumesoma lakini hajui tufanye nini ili atukabiliane na ukosefu wa ajira,tumesoma lakini hatuna ubunifu wowote ule zaidi ya kuona aibu kuuza matunda.
 
Back
Top Bottom