Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

Aliesoma hua anaamini na kujipa matumaini ipo siku atapata kazi nzuri na kutoboa, wengi wao hushusha morali ya kazi, sasa stres za aliesoma afu bado maskini sana ni kubwa sana.
Asiesoma hua anapambana sana sababu anahisi hana nafasi nyingine kwa kua hana elimu, stres yake hua ya kawaida na kuridhika na umaskini sababu anajua hana elimu.
 
Kwa elimu ipi ya bongo inayofundisha kutumia elimu yako kupata pesa nje ya ajira? Elimu yetu hii tuliyofundishwa kukalili na sio kukabiliana na changamoto ya ajira?
Tumeandaliwa kusoma ili tuajiriwe na sio vinginevyo vijana wengi tumesoma lakini hajui tufanye nini ili atukabiliane na ukosefu wa ajira,tumesoma lakini hatuna ubunifu wowote ule zaidi ya kuona aibu kuuza matunda.
Nafikiri kama nimemwelewa vizuri mtoa mada ni kwamba tunajaribu kulinganisha upande upi una maisha mazuri Kati ya waliosoma na wasiosoma,achilia mbali madhaifu ya elimu yetu ambayo kimsingi haimpi mnufaika ujuzi wa MOJA kwa MOJA kwenda kupambana na life la kitaa
 
Wakuu! Naomba nitumie salamu zilizo zoeleka zaidi visiwani, “Hamjambo?”, “Mumesalimika?”.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Pamoja na mateso yote wanayopitia waliotumia muda mwingi mashuleni ambao kwa sasa wamezagaa kila kona ya taifa hili, kiasi cha baadhi kuwatafsiri kama wamepoteza uelekeo, ndugu zangu aliyesoma kasoma.

Afadhali ya yeye anayeteseka muda huu, lakini matumaini ya kesho yake kubadilika ghafla ni makubwa.

Fikiria mtu ambaye ajira zote zinazotoka iwe ni taasisi nyeti au taasisi yoyote ya serikali au binafsi yeye hazimuhusu kwa sababu hajasoma.

Ni bora aliyesoma anaweza kufanya hata kazi za asiyesoma kuliko asiyesoma ambaye kazi za aliyesoma hazimuhusu.

Ni rahisi zaidi kwa aliyesoma kuishi maisha ya ahueni, yaani kati kwa kati sio chini wala sio juu kuliko asiyesoma, asiyesoma akipigika anapigika kweli.

Najua pande zote mbili zina sumu kali sana, na zinatafuta pakuzitemea. Nawakaribisha kwenye huu uzi, zitemeeni hapa. Bila kujali umesoma au hujasoma, unaweza kukaa upande wowote.

Ama namna gani, wewe unaonaje?

Asante.

MUHIMU
Kuendana na uzi huu, msomi ni mwenye elimu ya fani kwa angalau ngazi ya Cheti.
Kufikia hapa nilipo sijui noseme nipo kundi lipi kwa maana nimeamua kuyaishi maisha ya pande zote na naona kuwepo katikati yao imenipa urahisi katika safari ya mafanikio.
 
Naona wanao bishana humu ni waliosoma masikini waliofeli maisha[emoji28][emoji28].... mimi elimu yangu imenisaidia ngoja nikae kimya!
 
Ukiachana na ben Carson niambie mtu mweusi ambaye anasifika Duniani kutokana na matumizi ya elimu yake! Jibu ni hakuna wala hatokuja kutokea.

Ndugu yangu, asante kwa komenti nzuri. Japo naomba ufafanuzi zaidi, nahisi kama mada umeipindua sana, umeipeleka kwenye rangi ya ngozi kuwa nyeusi au nyeupe na badala ya hali za kimaisha umejadili kwa upande wa umaarufu.
 
Mpaka hapa tushajua upande wako....swala siyo unalipwa mshahara kiasi gani bali unaitumiaje elimu yako kukupatia pesa nje na ajira za serikali
Hata hivyo huku kwetu wwana ambao waliukimbia umande wana hali mbaya sana kimaisha tofauti na waliosoma

Hahaha, asante Mkuu. Japo na wewe tumeshagundua upande wako.
 
Kwa elimu ipi ya bongo inayofundisha kutumia elimu yako kupata pesa nje ya ajira? Elimu yetu hii tuliyofundishwa kukalili na sio kukabiliana na changamoto ya ajira?
Tumeandaliwa kusoma ili tuajiriwe na sio vinginevyo vijana wengi tumesoma lakini hajui tufanye nini ili atukabiliane na ukosefu wa ajira,tumesoma lakini hatuna ubunifu wowote ule zaidi ya kuona aibu kuuza matunda.

Msweden naomba nijipambanue mimi kuwa ni miongoni mwa tuliofika shule japo kwa uchache. Ila kote huko sijawahi kufundishwa au kupewa onyo kwamba niliyojifunza darasani siruhusiwi kuyatumia nje ya ajira, au kuelekezwa kwamba ni lazima nisubiri kuajiriwa.

Hivi ni kweli msomi hawezi kutumia elimu yake nje ya ajira au kutengeneza ajira badala ya kusubiri kuajiriwa?
 
Aliesoma hua anaamini na kujipa matumaini ipo siku atapata kazi nzuri na kutoboa, wengi wao hushusha morali ya kazi, sasa stres za aliesoma afu bado maskini sana ni kubwa sana.
Asiesoma hua anapambana sana sababu anahisi hana nafasi nyingine kwa kua hana elimu, stres yake hua ya kawaida na kuridhika na umaskini sababu anajua hana elimu.

Mkuu uko sahihi sana, unaonaje mtazamo wa kwamba asiyesoma msongo wake una nafuu kwa sababu anamatumaini ya kupata kazi, wakati aliyesoma anajikuta na msongo wa mawazo kwa kutokuwa na chaguo lolote mbadala?
 
Hahaha, nikadhani Nyerere alishamalizana na haya mambo ya ukabila. Tupe tafsiri kwa kiswahili tuokote cha kujifunza.
Nyerere alikataza tusitumie lugha zetu za asili? Sioni mahali nilipichochea ukabila unaouzungumzia
 
Wakuu! Naomba nitumie salamu zilizo zoeleka zaidi visiwani, “Hamjambo?”, “Mumesalimika?”.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Pamoja na mateso yote wanayopitia waliotumia muda mwingi mashuleni ambao kwa sasa wamezagaa kila kona ya taifa hili, kiasi cha baadhi kuwatafsiri kama wamepoteza uelekeo, ndugu zangu aliyesoma kasoma.

Afadhali ya yeye anayeteseka muda huu, lakini matumaini ya kesho yake kubadilika ghafla ni makubwa.

Fikiria mtu ambaye ajira zote zinazotoka iwe ni taasisi nyeti au taasisi yoyote ya serikali au binafsi yeye hazimuhusu kwa sababu hajasoma.

Ni bora aliyesoma anaweza kufanya hata kazi za asiyesoma kuliko asiyesoma ambaye kazi za aliyesoma hazimuhusu.

Ni rahisi zaidi kwa aliyesoma kuishi maisha ya ahueni, yaani kati kwa kati sio chini wala sio juu kuliko asiyesoma, asiyesoma akipigika anapigika kweli.

Najua pande zote mbili zina sumu kali sana, na zinatafuta pakuzitemea. Nawakaribisha kwenye huu uzi, zitemeeni hapa. Bila kujali umesoma au hujasoma, unaweza kukaa upande wowote.

Ama namna gani, wewe unaonaje?

Asante.

MUHIMU
Kuendana na uzi huu, msomi ni mwenye elimu ya fani kwa angalau ngazi ya Cheti.
Hii battle umeibuni wewe, dunia hii inahitaji watu walioelimika na siyo waliosoma.

Intelligent is better than degree.
 
Ukikaa Kwa kusubiri ajira eti kwakuwa umesoma hii itakudharaulisha sana ni heri udharaulike kwa kufanya kazi nje ya ulichosomea kuliko kusubiri ukafanye kazi ya ulichosomea, fursa ziko nyingi sana na mpaka uwe na jicho la kuona, mfano, Watu wanazaa sana, na kutokana na changamoto za utafutaji wanakosa muda wakuwalea Watoto wao, kwanini msomi usiwaze namna ya kutatua changamoto hii, Kwa kuanzisha daycare, unatafuta mdada ambaye utamlipa kulingana na unachopata Ili awatunze Watoto na wewe unapata mia mbili mia tatu kuliko kuzurura na bahasha na umecharara??
 
Kuna mdogo angu hajasoma anatembea na mabus average amekula,amelaka akiba anabakiw na 50 elfu.

Mimi kupata elfu 5 ni mtihani zaidi nawaziwa mamilioni yaliyoenda na maji.

Hahaha, Mkuu mamilioni hayajaenda na maji, umewekeza. Hata hivyo mbona na wewe bado una nafasi ya kutembea na mabasi, au kinachokukwamisha ni nini?
 
Ifike mahali tujue kutafsiri tuliyoyasomea katika kutatua changamoto tulizonazo ambazo ni nyingi, Kuna wakati nilimsikia waziri wa viwanda na biashara kipindi Cha JK anasema Zanzibar Kuna upungufu wa nyama za kuku kiasi cha kuagiza nje?? Hivi kweli watanzania hatuwezi kufuga?? Au mentality ya color jobs huku tukiota mishahara mikubwa ndio inatuharibu
 
Nafikiri kama nimemwelewa vizuri mtoa mada ni kwamba tunajaribu kulinganisha upande upi una maisha mazuri Kati ya waliosoma na wasiosoma,achilia mbali madhaifu ya elimu yetu ambayo kimsingi haimpi mnufaika ujuzi wa MOJA kwa MOJA kwenda kupambana na life la kitaa

Hahaha, Mkuu asante kwa ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom