Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

Battle ya waliyosoma na wasiyosoma

Kufikia hapa nilipo sijui noseme nipo kundi lipi kwa maana nimeamua kuyaishi maisha ya pande zote na naona kuwepo katikati yao imenipa urahisi katika safari ya mafanikio.

Mkuu, hakuna kitu kigumu duniani kama kuwa katikati, unaweza ukadhani uko nyutro lakini kiuhalisia kukawa na upande umeuchagua au umekuchagua.

Hebu tudokezee uko ngazi gani ya elimu, au ni kipi kimefanya uamini uko nyutro?
 
Naona wanao bishana humu ni waliosoma masikini waliofeli maisha[emoji28][emoji28].... mimi elimu yangu imenisaidia ngoja nikae kimya!

[emoji23] Kwamba Mkuu wewe, ni yupi? Usiosoma ambaye umefanikiwa kimaisha au?

Hebu tupe mtazamo wako, upande upi una nafuu?
 
Hii battle umeibuni wewe, dunia hii inahitaji watu walioelimika na siyo waliosoma.

Intelligent is better than degree.

Asante sana ndugu Matola, komenti yako imeniongezea zaidi uelewa. Vipi lakini sio kwamba ili mtu aelimike inaanza kwa kuwa amesoma?

Nakubali kwamba wapo waliosoma lakini hawajaelimika, lakini napata wasiwasi kama upo uwezekano wa kuelimika bila ya kusoma.
 
Ukikaa Kwa kusubiri ajira eti kwakuwa umesoma hii itakudharaulisha sana ni heri udharaulike kwa kufanya kazi nje ya ulichosomea kuliko kusubiri ukafanye kazi ya ulichosomea, fursa ziko nyingi sana na mpaka uwe na jicho la kuona, mfano, Watu wanazaa sana, na kutokana na changamoto za utafutaji wanakosa muda wakuwalea Watoto wao, kwanini msomi usiwaze namna ya kutatua changamoto hii, Kwa kuanzisha daycare, unatafuta mdada ambaye utamlipa kulingana na unachopata Ili awatunze Watoto na wewe unapata mia mbili mia tatu kuliko kuzurura na bahasha na umecharara??

Mkuu, Ubarikiwe sana. Niamini unaweza kuona ulichoandika ni kidogo lakini kuna watu umewafungua fikra sana na inawezekana wakalitumia hili wazo lako kama lilivyo.
 
Kuna waliosoma wanasota miaka nenda rudi na kuna la saba B wanakula bata hawajui shida zinafananaje.

Ni kweli kabisa, nakuunga mkono kwenye hili. Vipi lakini kwa makadirio bila ya kuwa na takwimu za moja kwa moja, unadhani kundi lipi ni kubwa zaidi?
 
Ifike mahali tujue kutafsiri tuliyoyasomea katika kutatua changamoto tulizonazo ambazo ni nyingi, Kuna wakati nilimsikia waziri wa viwanda na biashara kipindi Cha JK anasema Zanzibar Kuna upungufu wa nyama za kuku kiasi cha kuagiza nje?? Hivi kweli watanzania hatuwezi kufuga?? Au mentality ya color jobs huku tukiota mishahara mikubwa ndio inatuharibu

Nakiri kwamba wewe ni miongoni mwa watu wenye akili zaidi huku mitandaoni.

Asante sana.
 
Hahaha, Mkuu mamilioni hayajaenda na maji, umewekeza. Hata hivyo mbona na wewe bado una nafasi ya kutembea na mabasi, au kinachokukwamisha ni nini?
Umri umeenda, connection kuianzisha leo na mpaka kuja kupata gari sio leo.!
 
Ni kweli kabisa, nakuunga mkono kwenye hili. Vipi lakini kwa makadirio bila ya kuwa na takwimu za moja kwa moja, unadhani kundi lipi ni kubwa zaidi?
Kwakweli sifahamu, nashindwa kukadiria nisije kutoa takwimu za uongo
 
Wakuu! Naomba nitumie salamu zilizo zoeleka zaidi visiwani, “Hamjambo?”, “Mumesalimika?”.

Niende moja kwa moja kwenye mada. Pamoja na mateso yote wanayopitia waliotumia muda mwingi mashuleni ambao kwa sasa wamezagaa kila kona ya taifa hili, kiasi cha baadhi kuwatafsiri kama wamepoteza uelekeo, ndugu zangu aliyesoma kasoma.

Afadhali ya yeye anayeteseka muda huu, lakini matumaini ya kesho yake kubadilika ghafla ni makubwa.

Fikiria mtu ambaye ajira zote zinazotoka iwe ni taasisi nyeti au taasisi yoyote ya serikali au binafsi yeye hazimuhusu kwa sababu hajasoma.

Ni bora aliyesoma anaweza kufanya hata kazi za asiyesoma kuliko asiyesoma ambaye kazi za aliyesoma hazimuhusu.

Ni rahisi zaidi kwa aliyesoma kuishi maisha ya ahueni, yaani kati kwa kati sio chini wala sio juu kuliko asiyesoma, asiyesoma akipigika anapigika kweli.

Najua pande zote mbili zina sumu kali sana, na zinatafuta pakuzitemea. Nawakaribisha kwenye huu uzi, zitemeeni hapa. Bila kujali umesoma au hujasoma, unaweza kukaa upande wowote.

Ama namna gani, wewe unaonaje?

Asante.

MUHIMU
Kuendana na uzi huu, msomi ni mwenye elimu ya fani kwa angalau ngazi ya Cheti.
tuangalie elimu inamchango gani kwa mtu mmoja mmoja mpaka kwa Taifa ....Mataifa yenye maendeleo makubwa Dunian watu wake wakoje ...??na Mataifa yenye maendeleo ya kati na masikini watu wake wakoje ??
 
Mkuu, Ubarikiwe sana. Niamini unaweza kuona ulichoandika ni kidogo lakini kuna watu umewafungua fikra sana na inawezekana wakalitumia hili wazo lako kama lilivyo.
Mkuu ukikaa ukiwaza vipo vingi vya kufanya na hela, ikaingia Kuna wale wenzangu wamesoma masomo ya sayansi, na tunajua kabisa masomo ya sayansi Kuna changamoto kwenye practicals kwanini msomi asifungue center Kwa ajili ya practicals tu, Ili madogo wasaidike??.... Najua vile vifaa ni gharama lakini Kila penye nia Pana njia, tusitumie tu Elimu ya digriii na ya form six pia, na ya form four pia.
 
All in all, elimu ni muhimu na itaendelea kuwa muhimu all time kwetu,
japokuwa kuna baadhi ya dosari zinazojitokeza kwenye mfumo wetu wa elimu na kuifanya iwe ngumu na pia somehow kutengeneza wajinga,
Ila pia na sisi tukumbuke kuwa elimu it's not all about kuajiriwa inawezekana ni umaskini tu unatufanya tuwe na dhana hiyo.But lengo kuu la elimu ni kutatua shida na chabgamoto mbalimbali zinazoikumba jamii yetu kwa kutoa ujinga kwa wanajamii wake, na kuajriwa ni matokeo tu ya kuwa na elimu,
Na pia anaelalamika kukosa ajira akiwa na elimu me naona kama bado elimu HAIJAMSAIDIA kwani malalamiko hayo hayawezi fanya miujiza yeyote kwake zaidi ya kupoteza muda, nashauri " take action msomi elimu uliyonayo inakutosha kukutoa hapo ulipo"
 
Umri umeenda, connection kuianzisha leo na mpaka kuja kupata gari sio leo.!

Mkuu, unaposema umri umeenda unamaanisha miaka mingapi?

Hata hivyo, ili kutoka kimaisha wala idadi ya miaka uliyopambana inaweza isiwe na umuhimu, cha muhimu ni muda wako kufika.

Kuna watu wametumia mwaka mmoja kutengeneza mafanikio na koneksheni ambazo wengine wamezipambana kwa zaidi ya miaka 20 hawajazipata.

Siku pekee umri utakuwa umekwenda sana ni ukifa, lakini kama bado uko hai ni bora kuwekeza kuliko kukaa aido kwa kuamini umechelewa.
 
All in all, elimu ni muhimu na itaendelea kuwa muhimu all time kwetu,
japokuwa kuna baadhi ya dosari zinazojitokeza kwenye mfumo wetu wa elimu na kuifanya iwe ngumu na pia somehow kutengeneza wajinga,
Ila pia na sisi tukumbuke kuwa elimu it's not all about kuajiriwa inawezekana ni umaskini tu unatufanya tuwe na dhana hiyo.But lengo kuu la elimu ni kutatua shida na chabgamoto mbalimbali zinazoikumba jamii yetu kwa kutoa ujinga kwa wanajamii wake, na kuajriwa ni matokeo tu ya kuwa na elimu,
Na pia anaelalamika kukosa ajira akiwa na elimu me naona kama bado elimu HAIJAMSAIDIA kwani malalamiko hayo hayawezi fanya miujiza yeyote kwake zaidi ya kupoteza muda, nashauri " take action msomi elimu uliyonayo inakutosha kukutoa hapo ulipo"

Mkuu, asante sana. Nimetafuta cha kuongezea kwenye andiko lako nimekosa, limetimia kila idara.

Vipi wanaodhani kwamba wasiosoma wanauwezekano wa kuwa mbali zaidi kwa sababu wamekuwa na muda mwingi wa kupambana mtaani kuliko wasomi waliokaa sana darasani baada ya miaka mingi ndipo wakaruhusiwa kurudi uraiani?
 
Mkuu ukikaa ukiwaza vipo vingi vya kufanya na hela, ikaingia Kuna wale wenzangu wamesoma masomo ya sayansi, na tunajua kabisa masomo ya sayansi Kuna changamoto kwenye practicals kwanini msomi asifungue center Kwa ajili ya practicals tu, Ili madogo wasaidike??.... Najua vile vifaa ni gharama lakini Kila penye nia Pana njia, tusitumie tu Elimu ya digriii na ya form six pia, na ya form four pia.

Mkuu, wewe ni mgodi unaotembea.
 
Mkuu, hakuna kitu kigumu duniani kama kuwa katikati, unaweza ukadhani uko nyutro lakini kiuhalisia kukawa na upande umeuchagua au umekuchagua.

Hebu tudokezee uko ngazi gani ya elimu, au ni kipi kimefanya uamini uko

Mkuu, hakuna kitu kigumu duniani kama kuwa katikati, unaweza ukadhani uko nyutro lakini kiuhalisia kukawa na upande umeuchagua au umekuchagua.

Hebu tudokezee uko ngazi gani ya elimu, au ni kipi kimefanya uamini uko nyutro?
Simaanishi katika mtazamo huo bali namanisha kuwa na elimu kiasi na kisha kuishi katika mazingira ya wasiosoma na kutumia fursa zilizopo.
 
Back
Top Bottom