Basi la Zuberi lapata ajali Singida

Mroojr

Member
Nov 15, 2010
65
8
Ni kiasi cha km 60 kutokea mji wa singida barabara ya Mwanza-Dar ambapo basi hilo limepata ajali muda mfupi sasahv na tayari maiti 3 zilishatolewa na bado uokozi unaendelea.

Tutaendelea kuwajuza kadri tutakapojaliwa kuyajua yaliopo eneo la ajali.

Taarifa za mwanzo zinaonyesha chanzo cha ajali ni utelezi eneo hilo la lami maana mvua ilikuwa inanyesha.

==========
UPDATES

Ni kweli habari za kukwepa bibi kizee zimezagaa sana lakini haonekana huyo bibi kizee na hapakuwa na watu wa kuthibitsha hilo miongoni mwa abiria kutokana na hali ya taharuki iliyokuwepo hapo. Kwahiyo ni vigumu kuithibitisha habari ya bibi kizee.
 
kwa mujibu wa mtu aliyeko kwenye eneo la tukio ajali hii imehusisha basi la Zuberi lililokuwa linatokea Mwanza kwenda Dar, watu wanne wamepoteza maisha na wengine wengi wamejeruhiwa dereva alikuwa akimkwepa bibi kizeee
 
Ni kweli habari za kukwepa bibi kizee zimezagaa sana lakini haonekana huyo bibi kizee na hapakuwa na watu wa kuthibitsha hilo miongoni mwa abiria kutokana na hali ya taharuki iliyokuwepo hapo. Kwahiyo ni vigumu kuithibitisha habari ya bibi kizee.
 
-Ilianza kampeni ya vithibiti mwendo
-Ikaja ishu ya mabasi -malori kupigwa marufuku
-Ikaja ishu sijui ya milango ya dharula
-Ikaja ishu ya leseni mpya

Upuuzi wote huo haujapunguza ajali nchini.
 
CCM kwa miaka 50 wameshindwa kuanzisha chombo kama National Transportation Safety Board NTSB ya Marekani, ambacho kina jukumu la kuchunguza kila ajali chanzo chake ni nini na kushauri serikali namna ya kuepuka ajali kama hizo in future. Hapa Tanzania ajali ikitokea Traffic wanaenda na vimita vyao na kamba kamba za kupimia kama wanapiga ramli. Baada ya hapo hautawasikia tena na ajali zinaendelea kutokea. Kila ajali lazima Ina lessons learned ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kusaidia kuepusha ajali na kuokoa maisha.

Hopefully Chadema wakiingia madarakani 2015 wanaweza kuonyesha juhudi ya kupunguza ajali, MaCCM yameshindwa kwa sababu Ni maFreemasonry yanafurahia damu za watanzania kumwagika
 
Basi liitwalo Zuberi lilokua linatoka Mwanza kwenda Dar limepata ajali eneo la Misuna mkoani Singida.

Muda huu majeruhi wanakimbizwa hospitali ya mkoa Singida.

Chanzo cha ajali dereva kukwepa bibi mtembea kwa miguu.
 
basi liitwalo zuberi lilokua linatoka mwanza kwenda dar limepata ajali eneo la misuna mkoani singida.
Muda huu majeruhi wanakimbizwa hospitali ya mkoa singida.
Chanzo cha ajali dereva kukwepa bibi mtembea kwa miguu.

.......ni isuna
 
Lilikuwa linaelekea wapi mkuu?kama lilikuwa linaelekea Mwanza basi lilikuwa katika mwendo mkali sana maana ni mapema mno kuwa limeshavuka Singida zaidi ya km 60!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Dereva awajibishwe. Sheria inasemaje juu ya kukwepa mmoja ili weng wadhurike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom