Basi la Zuberi lapata ajali Singida

Basi la Zuberi lapata ajali Singida

Naunga mkono wazo la kuwa na board ya kitaifa, itakayokuwa na jukumu la kufuatilia kwa kina kila ajari ya barabarani inayotokea, kwa lengo la kujua visababishi na kutoa taarifa / kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kuzuia ama kupunguza mwendelezo wa ajari unao gharimu mali, nguvu kazi na uhai wa watz wengi. Sumatra wamejikita zaidi ktk leseni, bila shaka kwa lengo la kukusanya mshiko! Hili ni wazo zuri ambalo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani anaweza kulichukua na kulifanyia kazi kwa kuishauri selikari..

Polen sana ndg zang mlopoteza ndg na jamaa zenu
 
Dereva awajibishwe. Sheria inasemaje juu ya kukwepa mmoja ili weng wadhurike

Ni kweli mkuu Dereva awajibishwe.kwani hata huo mwendo aliokua nao kwa walio salimika ni neema ya Mungu tu!
 
Bila kua na chombo chenye mamlaka kamili ya kutoa kusimamia na kuishauri serikali juu ya usalama barabarani tutaendelea kufa kwa ajali na kua nchi ya watu wenye vilema hadi mbingu zishuke.
 
hili basi huwa nasafiri nalo sana,tatizo kunakuwa na dereva mmoja badala ya wawili.huwa anachoka sana na sometime anasinzia.wanahitaji kufuata utaratibu sio kuangalia faida tu
 
Poleni majeruhi na mungu awalaze pema marehemu wote.
 
CCM kwa miaka 50 wameshindwa kuanzisha chombo kama National Transportation Safety Board NTSB ya Marekani, ambacho kina jukumu la kuchunguza kila ajali chanzo chake ni nini na kushauri serikali namna ya kuepuka ajali
Hopefully Chadema wakiingia madarakani 2015 wanaweza kuonyesha juhudi ya kupunguza ajali, MaCCM yameshindwa kwa sababu Ni maFreemasonry yanafurahia damu za watanzania kumwagika
UKISIKIA UMBURULA ndio huu
wewe ajali tu unaihusisha CCM

Eti huko Marekani NTSB

Madege matano yametungua majengo yakiwemo World Tade Center na Pentagon hawakuyazuia ndio CHADEMA leo aje azuie ajali ya gari lililotengenezwa na Binadamu
Ndoto nyingine za Diaspora zinachosha
ww changia Mada km ni Pole au Rambirambi utoe Siasa kwenye Vifo achana nayo kabisa
Msiba ni Msiba uwe wa Mtanzania au Mmarekani onesha hata Ubinadamu sio ooo CCM CCM

attachment.php
 
Ni kweli habari za kukwepa bibi kizee zimezagaa sana lakini haonekana huyo bibi kizee na hapakuwa na watu wa kuthibitsha hilo miongoni mwa abiria kutokana na hali ya taharuki iliyokuwepo hapo. Kwahiyo ni vigumu kuithibitisha habari ya bibi kizee.

mungu awabariki wote
 
-Ilianza kampeni ya vithibiti mwendo
-Ikaja ishu ya mabasi -malori kupigwa marufuku
-Ikaja ishu sijui ya milango ya dharula
-Ikaja ishu ya leseni mpya

Upuuzi wote huo haujapunguza ajali nchini.

Ilianza issue ya mabasi kusafiri mchana
 
Ni kiasi cha km 60 kutokea mji wa singida barabara ya Mwanza-Dar ambapo basi hilo limepata ajali muda mfupi sasahv na tayari maiti 3 zilishatolewa na bado uokozi unaendelea.

Tutaendelea kuwajuza kadri tutakapojaliwa kuyajua yaliopo eneo la ajali.

Taarifa za mwanzo zinaonyesha chanzo cha ajali ni utelezi eneo hilo la lami maana mvua ilikuwa inanyesha.

==========
UPDATES

Isamilo, Princes Munaa, Prince Muro, Ally's na wazee wengine wa njia hiyo nao waliteleza????
 
CCM kwa miaka 50 wameshindwa kuanzisha chombo kama National Transportation Safety Board NTSB ya Marekani, ambacho kina jukumu la kuchunguza kila ajali chanzo chake ni nini na kushauri serikali namna ya kuepuka ajali kama hizo in future. Hapa Tanzania ajali ikitokea Traffic wanaenda na vimita vyao na kamba kamba za kupimia kama wanapiga ramli. Baada ya hapo hautawasikia tena na ajali zinaendelea kutokea. Kila ajali lazima Ina lessons learned ambazo kwa namna moja au nyingine zinaweza kusaidia kuepusha ajali na kuokoa maisha.

Hopefully Chadema wakiingia madarakani 2015 wanaweza kuonyesha juhudi ya kupunguza ajali, MaCCM yameshindwa kwa sababu Ni maFreemasonry yanafurahia damu za watanzania kumwagika

Vp umepewa kazi ya kupiga kampeni na chadema au..!! yaani vitu kama ajali vinatokea we unaleta mambo ya vyama hapa, we njoo toa pole kwa wafiwa na majeruhi, au unagombea u/kiti wa kitongoji nini..!?
 
Hiyo nadhani ni ZUBERI #2 au 3. Mimi mwenyewe jana nimetoka Mwanza na basi la ZUBERI, kwa bahati nzuri #1 na tumefika salama saa 5 usiku. Hawana mwendo mkali sana hawa, kwa hilo madereva wake siwahukumu. Ila madereva hawapokezani, tangu Dar hadi Mwanza na kadhalika Mwanza hadi Dar! Mungu awalaze Mahali pema marehemu na kujalia majeruhi wapone haraka...
 
-Ilianza kampeni ya vithibiti mwendo
-Ikaja ishu ya mabasi -malori kupigwa marufuku
-Ikaja ishu sijui ya milango ya dharula
-Ikaja ishu ya leseni mpya

Upuuzi wote huo haujapunguza ajali nchini.

Hizo zote ni symptoms za underlying problem.....chanzo kikuu cha ajali nchi hii ni uduni wa barabara. Mpaka pale serikali yetu sikivu itakapofanya mapinduzi ya dhati na kuboresha barabara zetu ndio ajali zitakapopungua. Until then tuendelee kushuhudia raia wasio na hatia wakipoteza maisha
 
Hiyo nadhani ni ZUBERI #2 au 3. Mimi mwenyewe jana nimetoka Mwanza na basi la ZUBERI, kwa bahati nzuri #1 na tumefika salama saa 5 usiku. Hawana mwendo mkali sana hawa, kwa hilo madereva wake siwahukumu. Ila madereva hawapokezani, tangu Dar hadi Mwanza na kadhalika Mwanza hadi Dar! Mungu awalaze Mahali pema marehemu na kujalia majeruhi wapone haraka...

Hii habari ya ajali ya Zuberi sio ya jana,ni ya tangu mwezi may 2014
 
Back
Top Bottom