Basi la SUMRY lachinja tena, KASULU

Basi la SUMRY lachinja tena, KASULU

Meshacky

Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
50
Reaction score
0
Ndudu , Habari za Uhakika toka Kasulu Basi la Sumry lililokuwa linatoka Kigoma kuelekea Arusha limepata ajali jana asubuhi na kuua huko kasulu.

Habari ni confirmed kwa sababu mm mwenyewe nimepoteza jamaa yangu aliyekuwa anaelekea Arusha. Majeruhi na Maiti walipelekwa jana hiyo hiyo na Ambulance kwenda Hospitali ya Maweni Kigoma.

Idadi ya vifo na majeruhi sikuweza kuulizia kwa sababu nilichanganyakiwa na Kumpoteza jamaa yangu. Wenye taarifa zaidi watafafanua.
 
meshaky pole sana,hawa waarabu watatumalizia ndugu zetu,serikali iko wapi?????
 
mbona umetanguliza kuwa ni la mwanasiasa? hii ni ajali mkuu, tuwaombee majeruhi wapone haraka na kuwapa pole wafiwa wote
wamekufa wangapi?
 
mbona umetanguliza kuwa ni la mwanasiasa? hii ni ajali mkuu, tuwaombee majeruhi wapone haraka na kuwapa pole wafiwa wote
wamekufa wangapi?
ntakupiga BUN tena wewe, kwenye nyekundu hapo ajali zingine wanazisababisha haya wajinga!
 
Pinda si mwanasiasa?

Pinda ana hela hata ya kumiliki basi moja??? Salim Sumry is one of the richest person kule Sumbawanga, kama hujawahi kufika nenda ujionee, hayo mabasi ya Sumry yalikuwepo miaka mingi kabla ya hata Pinda hajawa PM, uache ushambenga kwa kitu usichokijua...mxiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Mweeeeee!!!!!!
 
meshaky pole sana,hawa waarabu watatumalizia ndugu zetu,serikali iko wapi?????
Serikali iko mifukoni mwao.

Thats too bad to take...

Ajali mbili za Sumri ndani ya wiki moja na wanaendelea tu kupakia abiria. Mtoto wa Mkulima ameamua kuua wakulima sasa.
 
Kwa mabasi ya kampuni moja kupata ajali days/weeks apart inaonesha kuna tatizo kubwa sana. Badala ya huu wimbo wa faini mara 30,000 mara 50,000 nilitegemea police/wizara ya mambo ya ndani wasitishe licence ya Summry hadi hapo hatua za kuridhisha kuwa Summary ana-uwezo wa kusafirisha abiria na kuwafikisha salama na sio maiti.

Kila kampuni inayosafirisha abiria iwekewe record, ajali za mara kwa mara maana yake hawana uwezo wa kusafirisha abiria. Inawezekana mabasi haya hayana ubora wa kubeba abiria, au madereva wake hawana uwezo, au pengine Dereva anaendesha gari kwa muda mrefu (10-12 hrs) kwa hiyo wanasinzia, au madereva wanakunywa pombe. Nimeshuhudia mwenyewe dereva anaweza 'KONYAGI' kwenye chupa ya maji ya kunywa (kilimanjaro) abiria wakimuona anakunywa wanafikiri ni maji kumbe ni Konyagi.

Nadhani muda umefika sasa kwa makampuni (sio tu madereva) kuwajibishwa maana tunaanza KUONA ajali kama jambo la kawaida!
 
Kama itakubalika kuwa sumry ana mabasi mengi sana basi watu wa takwimu wanaweza wakakusaidieni ninyi watu wa kuhesabu ajali mbili kwa wiki ndani ya kampuni moja. Kwamba kitakwimu inaweza ikawa mwenye mabasi 8 na akawa anapata ajali moja kila baada ya miezi sita ni hatarishi zaidi kuliko huyo sumry. Ima hili neno mwanasiasa mi naona mtoa mada ni mwana siasa zaidi ndiyo maana akakurupuka na neno mwanasiasa
 
@Nduguyangu, Summry limepata ajali huko same week iliyopita, na sio tu Summry wanaongoza kwa ajali, kuna HOOD, Aboud haya mabasi naona kama wanashindana kwa ajali. Wakijumlisha idadi ya vifo kutokana na ajali za makampuni haya matatu for the last 12 months watu watapatwa na mshutuko.
 
Inasikitisha,kama ajari imetokea jana asubuhi mbona magazeti ya leo hayajaripoti?kuna kitu hapa wakubwa.mungu awape nguvu majeruhi wote na marehemu walazwe pema peponi.amina.
 
mhhhhh!!! Sumry tena jamani??!!! Inakuaje kwani??? mabasi ni mabovu au ndo kafara hizo???!!!!

Poleni majeruhi na wote waliofiwa!
 
Ipo haja kwa serekali kusimamisha huduma za kampuni hii hadi uchunguzi wa ajali zote utakapobainisha chanzo halisi na kuchukua hatua stahiki. It is too much.
 
Back
Top Bottom