Basi la mwendokasi lapata ajali mbaya Magomeni Usalama

Basi la mwendokasi lapata ajali mbaya Magomeni Usalama

Kwa wao kua makini Ni kuendelea kupita kwenye Lane (barabara) zao, haihitaji Elimu ya ziada kulielewa hilo
Kwa taarifa yako hamna gari wala pikipiki inayopta hzo barabara isipokuwa sehemu za kuvukia kwa miguu na sehemu za mataa za kutuhusu magari mengine yapite ndo inaonyesha waligogana tatizo mnaona watu wa magari binafsi tu ndo wanamakosa. Kwanza Ku cross sehemu isiyotengwa ni ngumu kwa vitz
 
Chanzo cha ajali ya leo Ni kutofanya kazi kwa taa kwenye U-turn, hivyo dereva wa vitz akatumia uzoefu wa mjini wa mwenye kuwahi apite, duuuuh!, mwendokasi kumbe hawana fair play panapotokea hitilafu ya taa!. Sasa sijui kwa hapo sheria zinambeba nani!. Nawasilisha
Tatizo wanajiona wako above kuna cku mtoto alidondoshwa na boda boda u turn ya shekilango dereva akamgonga mtoto makusudi kabisa nashangaa watu kuwatetea hawa mbona daladala hazigongi hovyo
 
Tatizo wanajiona wako above kuna cku mtoto alidondoshwa na boda boda u turn ya shekilango dereva akamgonga mtoto makusudi kabisa nashangaa watu kuwatetea hawa mbona daladala hazigongi hovyo
Shida ya JF ni kwamba watu wanapenda hukumu kwa hisia kabla hata hawajajua uhalisia wa jambo!, Na Kuna wengine kwa comment zao utagundua hawapo dsm Na hata mradi wa mwendokasi wanaujua kupitia media tu, lakini wanavyochangia utadhani wapo eneo la tukio!
 
Hata madereva wa mabasi haya wana tatizo pia, wanakwenda speed kubwa mno,kawaida ya hizi basi nashkuru mungu nimezitumia nchi kadhaa hizi basi nafahamu utaratibu wake, hizo speed zao zimezidi hizi basi abiria wengi wanasimama wao wanakwenda speed na breki Kila sehemu yaani ndani ya bus full kugongana tu,
Asante ndugu kwa kuzitumia hizi BUS kwenye Nchi mbali mbali
 
Kuna ulakini wa Hiyo gari ndogo kuingia njia siyo yake!
 
Hata madereva wa mabasi haya wana tatizo pia, wanakwenda speed kubwa mno,kawaida ya hizi basi nashkuru mungu nimezitumia nchi kadhaa hizi basi nafahamu utaratibu wake, hizo speed zao zimezidi hizi basi abiria wengi wanasimama wao wanakwenda speed na breki Kila sehemu yaani ndani ya bus full kugongana tu,


Wanakwenda spidi kubwa mno ngapi? Taja km/saa wanazokwenda!
 
Nalia na elimu tu. Tuanzie hapo, la sivyo hatwendi popote!
 
toka lini kinyozi akajinyoa?
Poleni sana wadanganyika. Mimi nilitegemea Magufuli ataipiga nyundo hiyo barabara na kujijenga barabara kubwa yaani 5 lanes kulekea mbezi na 5 lanes kurudi mjini na kutafuta namna ya kujenga flyover pale Fire,magomeni,mabibo(mahakama ya ndizi) ubungo bus terminal na ubungo mataa na si kuendelea na huo upuuzi
 
Munaizungumzia u-turn mbona hio vitz inaonekana kama iko ndani kabisa ya barabara ya dart na ilikuwa ikitembea kwenda mbele ila ninachofikiri kwamba huyo mwenye vitz speed ilikuwa si kubwa ukilinganisha na speed ya bus. Cha msingi watanzania tufuate sheria za usalama barabarani tu kinyume na hivyo tutaishia kulaumu kila siku huku ajali zikiendelea kutokea.
 
Salamu Ndugu wana JF
Asubuhi ya leo Tarehe 29 mwez wa Tano imetokea ajali nyingine ya Basi la Mwendo wa Haraka eneo la Magomeni, Ajali hii ni muendelezo wa Ajali ndogndogo za magari haya lakini zikiongezeka kila kukicha ...Hapa inatupa muda wa kuangazia mambo mawili makubwa

1. Kwa kuangalia ajali ya leo inaonesha wazi kwamba upana wa barabara za magai haya ni hatarishi kwa watumiaji wa barabara hii kwani ni nyembamba kiasi cha kupelekea kuhatarisha usalama wa magari ya DART na yaliyo nje ya barabara hizo,,HAPA TUJIULIZE JE NI KWELI HUU NI UPANA HALISI WA BARABARA HIZI AU KUNA KIINI MACHO NYUMA YAKE?

2. Hoja ya pili ni ubora wa Magari haya? Gari la leo limegonga gari dogo aina ya Vitz sasa unajiuliza ni gari lipi lilitakiwa liumie kati ya haya mawili cha ajabu na kusikitisha BASI LA DART LIMECHANIKA KAMA BOXI,,kama karatasi,,,JE wahusika wa agari haya wana assure vipi watumiaji wa magari haya kuwabeba kwenye maboxi yaliyofungiwa Engene? Je Taasisi zinazohusika na magari haya toka kuingia zimefanya kazi yao ipasavyo au ni HAYA TWENDE?
TBS imepima ubora wa magari haya kweli? je hakuna Kiwango chochote cha kuangalia BODI ZA MAGARI HAYA KWELI kama ni bodi au maboxi? inakuwaje GARI LICHANIKE KAMA BOXI? je SUMATRA wamejihakikishia magari haya ni salama kwa watumiaj? je Jeshi la polisi limefanya uhakiki wa kina?

MWISHO: tumuombe Mungu ajali hizi zisiendelee maana tunaelekea kubaya kama USANII utafunikwa kwa kauli za kisiasa na maigizo ya maagizo yasiyozigatia utaalamu wowote....TUZITAKE mamlaka znazohusika zichukue hatua za HARAKA kuhakikisha usalama wa wananchi wa jiji la DAR ES SALAAM....
Uncless UZI HUU UTAKUMBUKWA
Niwatakie Jumapili njema.
Kwani dereva wa Dart aligongana na vitz kutokana na wembamba wa barabara? Mbona kama vitz ilimsogelea?
 
Kweli sio mchezo watu wanapiga kelele wAnaumia wengine wako bize kufukua simu zao wapate picha za kurusha facebook,
Kweli hizo ndizo baadhi ya faida za utandawazi
 
Nimetafakari juu ya hizi ajali, badae nikakubali pendekezo la jamaa mmoja kwamba Watz tunapaswa kupimwa akili.... Kwanini? Nina jibu... Hizi njia za mabasi yaendayo kasi zimetengwa na taarifa imekuwa ikitolewa kuwa magari mengine yasiingie kwenye hizo njia... Lakini bado wanaingia na kusababisha ajali hizi... Ni sawa na kuingilia reli halafu ugongwe na treni ulalamike. Kwangu mimi suala kubwa ni madreva wa vyombo vya moto vingine kufanya maamuzi ya tija kabla ya kuingia kwenye njia ya haya magari ya DART. Ni wazi na ni kweli kwamba madreva wengi hawapendi kufuata sheria za usalama barabarani, mfano utaona njia ni "one way" kwenda, ajabu watu wanatumia njia hiyo hiyo kuingia!!!

Period!!!
 
Hawa wote wana makosa wa Udart na vitz sio mda wote yanapita moja kwa moja kuna sehemu yanatakiwa kusimama kupisha magari mengine kuvuka barabara sasa hapo ndo wa udart na normal cars hawafati sheria tatizo mwapenda kulaumu upande moja mbona daladala hazigongi hovyo tena wao wako changanyikeni. Uendeshaji wa madereva wengi dar ni mubovu na kutokua makini
Diva, uendeshaji wa magari madogo katika mji huu unajulikana, sio jambo la kudiscuss hapa..
Madereva wengi hawafuati sheria, wengi wana haraka, wengi wana papala, wengi wana kiburi..."""hapa naziwahi hizi taa ngoja ninyooshe mguu"""
Faini kali lazima zitumike kuogopesha wahuni, maana hakuna namna ....
 
Shida ya JF ni kwamba watu wanapenda hukumu kwa hisia kabla hata hawajajua uhalisia wa jambo!, Na Kuna wengine kwa comment zao utagundua hawapo dsm Na hata mradi wa mwendokasi wanaujua kupitia media tu, lakini wanavyochangia utadhani wapo eneo la tukio!
umeongea ukweli mtupu kaka
 
Tatizo wanajiona wako above kuna cku mtoto alidondoshwa na boda boda u turn ya shekilango dereva akamgonga mtoto makusudi kabisa nashangaa watu kuwatetea hawa mbona daladala hazigongi hovyo
itakua unatia chumvi wachukiwe,hyo ajali bodaboda aliingia njia ya mwendokasi na navowajua alikua speed kufanya timing,fuateni sheria
 
Back
Top Bottom