Basi la mwendokasi lapata ajali mbaya Magomeni Usalama

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,149
3,862
Nipo napita hapa usalama ndani ya UDART, kuna basi limepata ajali mbaya na limeharibika vibaya , nadhani kutakuwa na majeruhi..

Mwenye habari zaidi tafadhali
==========
Salamu Ndugu wana JF
Asubuhi ya leo Tarehe 29 mwez wa Tano imetokea ajali nyingine ya Basi la Mwendo wa Haraka eneo la Magomeni, Ajali hii ni muendelezo wa Ajali ndogndogo za magari haya lakini zikiongezeka kila kukicha ...Hapa inatupa muda wa kuangazia mambo mawili makubwa

1. Kwa kuangalia ajali ya leo inaonesha wazi kwamba upana wa barabara za magai haya ni hatarishi kwa watumiaji wa barabara hii kwani ni nyembamba kiasi cha kupelekea kuhatarisha usalama wa magari ya DART na yaliyo nje ya barabara hizo,,HAPA TUJIULIZE JE NI KWELI HUU NI UPANA HALISI WA BARABARA HIZI AU KUNA KIINI MACHO NYUMA YAKE?

2. Hoja ya pili ni ubora wa Magari haya? Gari la leo limegonga gari dogo aina ya Vitz sasa unajiuliza ni gari lipi lilitakiwa liumie kati ya haya mawili cha ajabu na kusikitisha BASI LA DART LIMECHANIKA KAMA BOXI,,kama karatasi,,,JE wahusika wa agari haya wana assure vipi watumiaji wa magari haya kuwabeba kwenye maboxi yaliyofungiwa Engene? Je Taasisi zinazohusika na magari haya toka kuingia zimefanya kazi yao ipasavyo au ni HAYA TWENDE?
TBS imepima ubora wa magari haya kweli? je hakuna Kiwango chochote cha kuangalia BODI ZA MAGARI HAYA KWELI kama ni bodi au maboxi? inakuwaje GARI LICHANIKE KAMA BOXI? je SUMATRA wamejihakikishia magari haya ni salama kwa watumiaj? je Jeshi la polisi limefanya uhakiki wa kina?

MWISHO: tumuombe Mungu ajali hizi zisiendelee maana tunaelekea kubaya kama USANII utafunikwa kwa kauli za kisiasa na maigizo ya maagizo yasiyozigatia utaalamu wowote....TUZITAKE mamlaka znazohusika zichukue hatua za HARAKA kuhakikisha usalama wa wananchi wa jiji la DAR ES SALAAM....
Uncless UZI HUU UTAKUMBUKWA
Niwatakie Jumapili njema.

Hawa nao utafikiri hawakupewa semina elekezi, kila wa leo ajali mweeee
Dah... kama waliwachukua ex- daladala drivers wanategemea nini? hawakusoma yaliyowapata UDA? Hawa jamaa wameisha komaa hawakunjiki tena. Ningekuwa mimi kwasababu ni mradi mpya wenye mambo mapya basi ningewaajiri madereva wengi kutoka mkoa na sifa ya kukosa kazi ni kuwa uliwahi kuwa dereva wa daladala katika miji mikubwa.:)
 
Hawa nao utafikiri hawakupewa semina elekezi, kila wa leo ajali mweeee
Unahitaji seminar elekezi gani zaidi ya kuheshimu sheria za barabarani? Halafu mkipewa hizo seminar mnataka mpewe na posho sio?
Mm naona hata hivyo hajagongwa vizur. Ingetakiwa hako ka kiberiti kake kangefanywa chapati bakisa ili iwe fundisho kwa wazembe na wapumvavu walio wengi waoaochezea sheria za barabarani na kutia hasara watiifu wa sheria za barabarani.
 
Salamu Ndugu wana JF
Asubuhi ya leo Tarehe 29 mwez wa Tano imetokea ajali nyingine ya Basi la Mwendo wa Haraka eneo la Magomeni, Ajali hii ni muendelezo wa Ajali ndogndogo za magari haya lakini zikiongezeka kila kukicha ...Hapa inatupa muda wa kuangazia mambo mawili makubwa

1. Kwa kuangalia ajali ya leo inaonesha wazi kwamba upana wa barabara za magai haya ni hatarishi kwa watumiaji wa barabara hii kwani ni nyembamba kiasi cha kupelekea kuhatarisha usalama wa magari ya DART na yaliyo nje ya barabara hizo,,HAPA TUJIULIZE JE NI KWELI HUU NI UPANA HALISI WA BARABARA HIZI AU KUNA KIINI MACHO NYUMA YAKE?

2. Hoja ya pili ni ubora wa Magari haya? Gari la leo limegonga gari dogo aina ya Vitz sasa unajiuliza ni gari lipi lilitakiwa liumie kati ya haya mawili cha ajabu na kusikitisha BASI LA DART LIMECHANIKA KAMA BOXI,,kama karatasi,,,JE wahusika wa agari haya wana assure vipi watumiaji wa magari haya kuwabeba kwenye maboxi yaliyofungiwa Engene? Je Taasisi zinazohusika na magari haya toka kuingia zimefanya kazi yao ipasavyo au ni HAYA TWENDE?
TBS imepima ubora wa magari haya kweli? je hakuna Kiwango chochote cha kuangalia BODI ZA MAGARI HAYA KWELI kama ni bodi au maboxi? inakuwaje GARI LICHANIKE KAMA BOXI? je SUMATRA wamejihakikishia magari haya ni salama kwa watumiaj? je Jeshi la polisi limefanya uhakiki wa kina?

MWISHO: tumuombe Mungu ajali hizi zisiendelee maana tunaelekea kubaya kama USANII utafunikwa kwa kauli za kisiasa na maigizo ya maagizo yasiyozigatia utaalamu wowote....TUZITAKE mamlaka znazohusika zichukue hatua za HARAKA kuhakikisha usalama wa wananchi wa jiji la DAR ES SALAAM....
Uncless UZI HUU UTAKUMBUKWA
Niwatakie Jumapili njema.
 
Ni kweli imetokea leo

Kwa taarifa iliyoifikia millardayo.com leo asubuhi ya May 29 2016 ni ajali iliyohusisha moja kati ya Mabasi yaendayo haraka na gari ndogo aina ya Vitz New Model eneo la Magomeni Usalama Jijini Dar es Salaam baada ya gari hizo kugongana, tunazifuatilia taarifa zaidi na nitakuwekea hapa hapa millardayo.com
 
Unahitaji seminar elekezi gani zaidi ya kuheshimu sheria za barabarani? Halafu mkipewa hizo seminar mnataka mpewe na posho sio?
Mm naona hata hivyo hajagongwa vizur. Ingetakiwa hako ka kiberiti kake kangefanywa chapati bakisa ili iwe fundisho kwa wazembe na wapumvavu walio wengi waoaochezea sheria za barabarani na kutia hasara watiifu wa sheria za barabarani.
kila maendeleo mapya lazima kuwepo na madhara kwa wachache iwe kwa kutokujua au kwa ujeuri wao. inabid wafe au kulemaa watu wengi zaid ili wakaid wapate kuheshim hali halisi kwa manufaa ya wengi na maendeleo. hakuna jinsi sasa. ni muhim kuyaripoti matukio haya kwa wingi sana ili mwenye masikio na asikie. nimeona video na dreva wa vitz ana makosa ya wazi. mbona treni ikigonga hatushangai ni kwa sababu tulishaelewa haina makosa katika njia yake. 'DRIVE RESPONSIBLY'
 
Dar es Salaam. Kampuni inayoendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart) inatarajia kuanza kuuza hisa zake ili kuwapa fursa wananchi wengi kumiliki kampuni hiyo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Mkurugenzi Mtendaji wa Udart, David Mgwassa alisema hatua hiyo itatoa fursa kwa wananchi kuwa miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo.

“Kuanzia Oktoba au Novemba mwaka huu tutajiandikisha katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hapo ndipo tutaanza kuuza hisa na kila mwananchi ataruhusiwa kununua,” alieleza Mgwassa ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd inayotengeneza kinywaji cha konyagi.

Mkurugenzi huyo alisema pamoja na kuruhusu wananchi kununua hisa, wamiliki wa daladala nao watapata fursa ya kumiliki asilimia 30 ya hisa zote kama makubaliano ya awali kabla mradi huo haujaanza yanavyosema.

Udart yarahisisha usafiri Dar

Kuhusu ufanisi wa Udart, Mgwassa alisema mradi huo umesadia kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwani kwa siku mabasi hayo husafirisha wastani wa abiria 128,00 katika njia zote huku kwa njia ya Kimara pekee abiria wakifikia 40,000.

Kwa mtazamo wake, mradi huo umefanikiwa kwa asilimia 70 licha ya changamoto kadhaa na kwamba wananchi wameshaanza kuona matunda yake. Alisema sasa watu wameanza kubadili mtindo wa maisha kwa kuwa usafiri si kitu kinachowasumbua kutokana na kuwa wa uhakika nao.

“Awali wakati tunaanza, saa 11.15 alfajiri ulikuwa unakuta abiria wamejazana katika vituo lakini sasa hali ni tofauti tukifika muda huo hakuna abiria, wanaanza kuja vituoni kuanzia saa 12. Nilipowahoji kwa nini, walisema kuwa ni kutokana na kuwa na uhakika wa usafiri,” alieleza.

Alisema hali hiyo inasaidia wananchi kuwa na muda wa kupumzika hivyo kufanya kazi kwa ufanisi tofauti na awali abiria walitumia saa moja mpaka mbili kwa safari za asubuhi na muda kama huo wanaporejea nyumbani wakati sasa wanatumia dakika 45 pekee.

Changamoto

Mgwassa alisema changamoto kubwa waliyokumbana nayo katika kipindi cha wiki hizi mbili tangu mradi huo uanze ni nidhamu mbovu ya madereva wengi wa magari hayo kutokana na wengi wao awali kuwa madereva wa daladala.

“Asilimia 90 ya madereva wetu wametoka katika daladala ndiyo maana inatusumbua sana, wana tabia ambazo si rafiki, unashangaa hawaheshimu sheria za barabarani; wanapita bila kujali taa nyekundu na vivuko vya watembea kwa miguu,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema ili kurekebisha hali hiyo, amefanya mazungumzo na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Veta) kwa ajili ya kutoa elimu upya kwa madereva wao ili waheshimu sheria na alama za barabarani.

“Ni tatizo kubwa la kisaikolojia. Tangu mradi ulipoanza naamka saa 10.00 alfajiri, naanzia Kimara na nazunguka njia zote, mara kwa mara nakuta wanafanya makosa ya wazi kabisa. Mfano, juzi niliongozana na gari moja tukafika Ubungo, dereva akapita katika taa nyekundu nikampigia simu na kumuuliza kulikoni? Ikabidi aombe radhi. Cha kushangaza alipofika Magomeni akarudia kosa lilelile. Sasa unajiuliza hawa watu wanafanyaje kazi?.

“Wapo wengine hawawezi kabisa, tumejaribu kuwaelimisha lakini wapi. Kabla ya mradi kuanza tuliwapa mafunzo lakini bado hali ni mbaya.”

Mgwassa alisema kutokana na tabia hiyo, mpaka sasa madereva hao wameshasababisha ajali zaidi ya 30 ambazo watu wawili wamepoteza maisha huku magari saba yakiharibika.

Alisema changamoto nyingine ni tabia ya mbaya ya abiria kushindwa kufuata taratibu za usafiri jambo linalochangia kuharibu miundombinu ya mradi huo.

“Unashangaa watu hawapangi mistari, wanasukumana mpaka wanaharibu miundombinu ya mradi wakati magari yapo mengi na hata likiondoka litakuja jingine,” alisema Mgwassa na kufafanua kuwa mradi huo una jumla ya magari 105 yanayohudumia kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 6.00 usiku.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni trafiki wanavyoruhusu magari jambo linalosababisha kuharibu ratiba ya mabasi hayo na kutumia muda mrefu zaidi njiani tofauti na matarajio.

Alisema kwa sasa wameweka maofisa katika maeneo mbalimbali ili kuangalia kila kitu kinachoendelea barabarani lakini ripoti zinaonyesha kuwa mabasi hayo yanachelewa kutokana na kukaa muda mrefu katika taa ambazo zinahudumiwa na askari hao.

“Sehemu ambazo zinaongozwa na taa za barabarani hakuna shida, tatizo linakuja kwa baadhi ya taa zinazoongozwa na askari wa usalama barabarani, anaweza kuliweka basi kwa muda mrefu hadi nusu saa wakati mabasi haya ni ya haraka. Hatuna jinsi kwa sababu tunajua wanawahudumia wateja wengine pia, siyo mabasi yetu tu,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, Mgwassa aliliomba Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani kuona jinsi watakavyoweka mpango maalumu utakaosaidia kuboresha usafiri huo.

Ajira

Mgwassa alisema, mradi huo utakapokamilika utatoa ajira kati ya 430 mpaka 450 katika kada mbalimbali. “Hakuna asiyejua ajira ni tatizo kubwa nchini, hivyo mradi huu utapunguza kwa kiasi fulani maana tunatarajia ajira hizo ziwaguse moja kwa moja Watanzania.”

Miundombinu

Japokuwa Mgwassa alikiri mradi huo kuanza kabla ya kukamilika kwa miundombinu yake lakini amewatoa hofu wananchi kuwa bado Serikali inaendelea kuboresha siku hadi siku.

“Kuna vituo ambavyo havijakamilika; viwili miundombinu yake imeharibika, kimoja hakina umeme lakini kingine kimeharibika baada ya ajali iliyosababishwa na gari kukivamia lakini tayari Serikali imeshaanza taratibu za ukarabati kwa kuweka umeme na kutengeneza.”

Alipoulizwa ni nani mwenye dhamana ya kutengeneza miundombinu hiyo baada ya kugongwa au kuharibiwa, Mgwassa alisema jukumu hilo linajulikana na Serikali yenyewe.
 
Poleni sana wadanganyika. Mimi nilitegemea Magufuli ataipiga nyundo hiyo barabara na kujijenga barabara kubwa yaani 5 lanes kulekea mbezi na 5 lanes kurudi mjini na kutafuta namna ya kujenga flyover pale Fire,magomeni,mabibo(mahakama ya ndizi) ubungo bus terminal na ubungo mataa na si kuendelea na huo upuuzi
 
Back
Top Bottom