Basi la Golden Deer lapata ajali maeneo ya Iyovi, leo Agosti 7, 2023. Mmoja ajeruhiwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Mpaka sasa taarifa zilizopo zinasema basi la Golden Deer T 618 DMG kutoka Kyela kuelekea Dar es Salaam imepata ajali.

Taarifa zaidi zitakujia baadae.

IMG_8197.jpeg

IMG_8198.jpeg
7da48d13-1b1c-469f-8ea2-2d3064819f44.jpg
23317fac-4de8-4f5d-a4b4-6435c888d456.jpg

---
Morogoro. Mtu mmoja amelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito wilayani Mikumi na wengine wametibiwa na kuruhusiwa baada ya basi la kampuni ya New Force walilokuwa wakisafiria kutoka Kyela kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 7, 2023 jioni eneo la Msimba kwenye mteremko na kona za Iyovi Mikumi ambapo amemtaja majeruhi kuwa ni Elinipenda Kishimbo (26) aliyeteguka mkono.

Kamanda Mkama amemtaja dereva wa basi hilo kuwa ni George Obedi (48) huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva huyo kwa kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila ya kuchukua tahadhari na hivyo kukutaka na gari jingine uso kwa uso.
 
Poleni,
Mleta mada tulia na utuambie sasa, imetokea wapi na lini?
..naamini taarifa nyingine tutapata toka mamlaka husika.
 
halafu we wa kukurupuka kweli unakulupuka kama id yako inavyojieleza acha uzwazwa ndugu yangu
 
Vitakuwa vingi na taarifa ya serikali itapunguza idadi.
Hii kampuni ina mpango wa kupunguza population kila mwezi
Shida ni ligi wa upumbavu wa abiria unakuta upo ndani ya gari unamwambia punguza mwendo abaria wengine wanakwambia ongeza huyu mshamba tu kama yule bonge dereva hana maisha marefu wacha wamjaze kichwa.

Mbona kuna gari ukipanda zipo vizuri mwendo kawaida mfano ABC, ngasere
 
Wapunguze idadi ili?
Ni kawaida ya taarifa rasmi kwa na idadi pungufu na tofauti kulinganisha na eneo la tukio. Kwenye ndege ambapo data zote zipo walianza wanatofautiana idadi, Chalamila anataja yake na Precision wanataja yake sembuse kwenye basi ambalo wasafiri kibao humo hawajulikani majina halisi
 
Back
Top Bottom