Bashungwa alikumbusha Jeshi la Polisi kukomesha matukio ya utekaji nchini

Bashungwa alikumbusha Jeshi la Polisi kukomesha matukio ya utekaji nchini

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha linashughulikia masuala ya jinai ikiwemo kukomesha matukio ya utekaji nchini.

Mbali na hilo, ameliagiza jeshi hilo kudhibiti madereva wazembe na vyombo vya moto vilivyo chini ya viwango ambavyo havistahili kuwa barabarani ili kupunguza matukio ya ajali.

Bashungwa ameyasema hayo leo, Agosti 6,2025 wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la Kituo cha Polisi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, lililogharimu zaidi ya Sh300 milioni.

"Nitumie nafasi hii kulielekeza Jeshi la Polisi kuendelea kuzingatia maelekezo mbalimbali yanayohusu masuala ya jinai ikiwemo kukomesha matukio ya utekaji, pamoja na kudhibiti madereva wazembe na vyombo vya moto vilivyo chini ya viwango ambavyo havistahili kuwa barabarani ili kupunguza ajali,"amesema Bashungwa

Aidha, amelitaka Jeshi hilo kuendelea kuharakisha upelelezi wa mashauri mbalimbali kwa kushirikiana na vyombo vingine vya haki jinai, na kuhakikisha linaboresha utoaji huduma kwa wananchi wanapofika katika vituo vya polisi nchini.

Pamoja na mambo mengine, amelitaka Jeshi hilo kuhakikisha linakomesha vitendo vya uvunjifu wa amani na uhalifu nchini na kuhakikisha tunu ya amani inakuwepo.

 
Hili kauli limetoka baada ya mke wa Molel kutekwa.
 
1754495446332.jpeg
 
Back
Top Bottom