Bashe karibu CHADEMA, una akili za ki-CHADEMA

Bashe karibu CHADEMA, una akili za ki-CHADEMA

Sajirini kina Simba na makapi wengine! Bashe yuko eneo sahihi na si mnafiki wa kunadili gia angani.
bashe siku anahamia chadema ile kesi yake ya uraia itafufuliwa upya na ataitwa MSOMALI cha kushangaxa barafuyamoto unamuona jembe leo ila wiki ijayo akitimuliwa utakuja humu kumuita kapi kana kwamba miaka yote akiwa ccm hamkulijua hilo hadi siku anatimuliwa 😀😀😀😀
 
somo gumu kwa chadema, nani alihamia ccm kutoka cdm akafikia kuwa kiongozi ccm? especially kamati kuu? cdm mnachekesha kweli
Mkuu hivi unajua maana ya kuhamia upinzani?? ni sawasawa na kuyaweka maisha yako rehani ni sacrifice moja kubwa sana ona masha na sumaye wa ccm walinganishe na wakiwa chadema afu nipe conclusion!!!! its not easy mkuu wanawapa uongozi ili kuwaonyesha imani juu ya uzoefu wao kwenye uongozi serikalini kwa miaka mingi lakini mwisho wa siku mbona uongozi wa juu wote wa chadema bado ni ule ule shida ikwapi??? kwani mashinji alihamia 2015 au mwalim au safari???
ccm mbona wamepokea wanchadema wengi tu na kuwapa uongozi kina shonza na mwampamba ni mfano mzuri bado kaborou n.k
 
Of course, Bashe ha-fit kabisa CCM sema nadhani hana imani na wana-Nzega manake Tabora kwa ujumla wake wamekunywa maji ya bendera!!!

Hata CUF ya Lipumba enzi hizo ipo CUF kweli kweli; Tabora hawakuinga mkono hadi hivi majuzi possibly kutokana na nguvu ya UKAWA!!!

Chief Saidi Abdallah Fundikira pamoja na kuwa Chifu wao; lakini wana Tabora hawakutaka kabisa kumuunga mkono na UMD yake hadi mzee wa watu akaamua kurudi CCM alipojiona ndo basi tena!!!

In short, Kanda ya Kati ni wamebugia vya kutosha maji ya bendera ya kijani....

Nadhani hicho kinachomvunja nguvu Bashe... maji ya bendera yaliyonywewa na kuogwa na wana-Tabora!! Lakini nadhani anasahau tu kwamba anaweza kushindwa kuibadili Tabora mzima kama ilivyokuwa kwa Lissu kwa Singida mzima lakini anaweza kuibadili angalau Nzega kama alivyofanikiwa Lissu Singida Magharibi!!!
Ukiona hivyo tambua kuwa ni kiongozi maslahi.
 
Hata huko CHADEMA hakuna Demokrasia kama unavyowanasibu.

Chama kimebadilika si kama kilivyokuwa awali.

Bila pesa hupati nafasi ya kuwawakilisha wananchi, waliokijenga chama kwa muda mrefu wanaachwa kwenye Chaguzi kwa njia za kibabe mathalani Bashe akifukuzwa CCM akaja CDM atapewa nafasi ya kugombea na kumsahau mpinzani aliyekuwepo Uchaguzi uliopita (CCM hawafanyi hayo). Yuko wapi Lembeli? Kawakosesha CDM Jimbo!

Kuna Wabunge walijulikana hawapiti baada ya kushinda chaguzi zilizopita (2010). Je, kulikuwa na Uchaguzi wa ndani kupitisha Wagombea? Hakuna zaidi ya kauli ya Mwenyekiti tu, hawa waacheni waendelee basi.

Mpeperusha Bendera ya Chama kwenye Urais je? Yaleyale, kupiga kura kwa kusimama kikanda pale Mwanza (Seriously!)

Mwisho nimalizie kwa Ushauri.

1. CDM ibadilike kwa kutendea Hali nafasi walizopata, tusiende mbali sana, Serikali za Mtaa. Kugonga mhuri tu unalipia kama ilivyokuwa awali chini ya CCM, Migogoro ya ardhi kutopungua na huduma zingine za kijamii.

2. CDM ijisafishe na skendo ya Ukabila na ukanda

3. Msingi wa kupata Wagombea iwe Demokrasia kweli, maana wanaopiga kura chamani ndiyo wapiga kura kwenye jamii pia wapiga kampeni.

4. Kupokea wanachama toka CCM sawa lakini wasipewe nafasi za juu. Hapa nikazie kidogo, hivi ukiambiwa leo Lowasa kuwa CDM ni mpango wa CCM kuwadhoofisha utakubali?

Tufanye siyo kweli, jiulize tena CCM inashindwa nini kumuandaa MTU atakayekuwa machachali kwa kuwapinga kisha akahama ili kuja kuwadhoofisha bila ninyi kujua (kuvujisha mbinu zenu kwa Wapinzani)?
1. naunga mkono

2. Tujisafishe kwa mangapi walianza wachagga ikaja ukabila then wakristo sijui tena magaidi eg lwakatare!!! tukiafanyia kazi propaganda za ccm hatutosonga mbele ndio maana mikoa ambayo sio ya wachagga mbona iliwabeba sana upinzani wapiga kura wengi sana wa miji mikubwa kma dar tanga mbeya iringa walitupa kura wapinzani je ina maana huko ni kwa wachagga????? watanzania wameamka wamegundua ccm wanawagawa .

3. wapi demokrasia imevunjwa nipe mfano

4. Nani kapewa nafasi ya juu?? lowasa si aligombea urais basi kwani umeskia kapewa uenyekiti au ukatibu mkuu???

eti lowassa kudhoofisha ccm??? mngetimuana hivi leo kisa walimsupport lowasa?? muache propaganfa lowasa alidhamiria kuifuta ccm ndio maana mzimu wake unawatesa
 
72f7ecdae7c61e7c96e9088320633734.jpg
 
hakuna Mkubwa kuliko ccm at least not bashe, mchukueni hata Leo, chadema nacho chama chenye mashiko kwn? chadema ni team mafisadi
Mahakama ya mafisadi si mnayo,polis mnao nini kinachowashida kuwafunga hao timu ya mafisadi?
 
Mmezoea kutafuniwa jifunzeni kutengeneza vyenu kazi kuokota tu acheni uvivu wakufikiri jiimarisheni mwenye
 
ILI KULITOA HILO LICHAMA LA MAJABAZI LAZIMA MASISIEMU YENYEWE YATOKE HUKO
 
bashe siku anahamia chadema ile kesi yake ya uraia itafufuliwa upya na ataitwa MSOMALI cha kushangaxa barafuyamoto unamuona jembe leo ila wiki ijayo akitimuliwa utakuja humu kumuita kapi kana kwamba miaka yote akiwa ccm hamkulijua hilo hadi siku anatimuliwa 😀😀😀😀
Mtazamo wako sio wangu.
 
hakuna Mkubwa kuliko ccm at least not bashe, mchukueni hata Leo, chadema nacho chama chenye mashiko kwn? chadema ni team mafisadi
Sema timu ngada ndio utaeleweka!
 
Nzega Mjini wanaikubali Chadema na wanamkubali Bashe,ushahidi ni kwamba Diwani wa Nzega Mjini ni mwanadada wa Chadema,na jinsi Chadema/Ukawa ilivyochana uchaguzi wa serikali za mitaa hapo mjini.Kwa hiyo Bashe kugombea Chadema utakuwa double coincidence kwa wana Nzega
diwa wa upinzani Nzega ni mmoja tu, wa kata ya Nzega magaribi.Kwa upande wa vitongoji ni kweli ulivyosema ila wamepishana kwa kitongoji kimoja.Ila Bashe endapo akienda upinzani atakuwa na kazi kubwa , wakazi wa Nzega ni wanafiki wa siasa , sijawahi kuona,Kama ni maandali basi anze sasa asisubiri ile miezi ya kampeni.Afanye kama alivyofanya Zitto pale kigoma mjini.Hakukurupuka kama machali
 
diwa wa upinzani Nzega ni mmoja tu, wa kata ya Nzega magaribi.Kwa upande wa vitongoji ni kweli ulivyosema ila wamepishana kwa kitongoji kimoja.Ila Bashe endapo akienda upinzani atakuwa na kazi kubwa , wakazi wa Nzega ni wanafiki wa siasa , sijawahi kuona,Kama ni maandali basi anze sasa asisubiri ile miezi ya kampeni.Afanye kama alivyofanya Zitto pale kigoma mjini.Hakukurupuka kama machali
Machali hamna kitu bure kabisa
 
Back
Top Bottom