Bashe awaonya Wanasiasa wanaowandanganya Wakulima kuelekea Uchaguzi

Bashe awaonya Wanasiasa wanaowandanganya Wakulima kuelekea Uchaguzi

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,608
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaotafuta kura kwa kukosoa mifumo ya kilimo ikiwemo mfumo wa pamba, BBT (Building a Better Tomorrow) na stakabadhi ghalani, akisema ni hatari kwa ustawi wa sekta hiyo.

Akizungumza leo ljumaa, Agosti 8, 2025 jijini Dodoma katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane, Bashe amesema wapo wanasiasa wanaotumia elimu ndogo ya baadhi ya wakulima kuwapotosha kwa lengo la kupata kura kwa muda mfupi.

"Wanatumia elimu ndogo ya wakulima kuwapotosha...

Naomba wakulima waendelee kuwa wavumilivu.

Tunasaka ruzuku kwa ajili ya maslahi yao. Wasiingize siasa ya wiki moja kuharibu mifumo ya nchi," amesema Bashe mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.

Bashe amesisitiza kuwa mifumo hiyo imejengwa kwa maslahi ya wakulima.

Maadhimisho ya Nanenane mwaka huu yameendelea kulenga kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika kilimo, uvuvi na ufugaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kubadilisha taswira ya sekta hiyo nchini.
 
Back
Top Bottom