Kuna kipindi miaka ya nyuma nilipataga deal la kuua mbwa koko wasio na wenyewe wanaozurura mtaani kwa kutumia bunduki
Siku ya kwanza ilienda vizuri niliua mbwa 47 kwenye vitongoji viwili siku iliyofuata yule afsa mifugo akaniambia leo ni jumapili tutatembelea mabucha nikakwambia sawa by saa 12 asubh tukaanza kupita bucha moja baada ya jingine
Tulipita mabucha kama matatu ukweli nililenga mbwa zaid ya 15 waliokuwa wanazurura kwa kuokota mifupa na finyango za nyama zilizodondoka chini.
Bucha la nne hapa ndipo nilipoona tukio la ajabu tumefika tu na byke jamaa akapaki mbali kidogo tukasogea pale buchani kwa miguu taratibu ....niliangaza macho eneo la pale buchani nikaona mbwa kama watatu bs nikatarget wa kwanzia nikapiga kuja kupiga wapili loooh akanguka chini na milio mkali gafla akabadilika na kuwa bibi kizee huku akilia kwa uchungu na akafia palepale huku mdomo wake na mikono ikiwa imechafuka mafuta na midamu kibao haikuwa hallucinations na nilikua sjanywa pombe hii ilinishangaza sana inawezekana vipi mbwa kubadilka na kuwa binadamu?
Ilikua ni tukio la kustajabisha sana pale buchani baadhi ya raia wakaanza kuongea chini chini huyu ni bibi flani tunamjua na ni mchawi mkubwa tukawauliza leo alikuwa hapa buchani wakajibu hapana dah afsa alipiga simu police na kuripot tukio.
Ikabidi nistop lile deal aise.