BASATA yaufungia wimbo wa Mwanza ulioimbwa na msanii Rayvanny kwa kushirikiana na Diamond Platnumz

Binafsi naona BASATA wamefanya maanmuzi mazuri lakini kwamuda usio sahihi.

Huku ni kutiana hasara tu.
Just imagine msanii ameimba wimbo na ametoa hadi video kwa gharama kubwa ndipo wanafungia wimbo.

USHAURI
Inatakiwa kabla ya msanii kutoa wimbo au nyimbo kwa umma. Nyimbo hizo zikaguliwe ili kuona kama hazivunji tamaduni na kuharibu maadili ya kitanzania.

Basata ipitie nyimbo za diamond zile za nyuma za hivi karibuni nyingi zimejaa lugha ya matusi na hats kama wanatumia tafsida...hizo tafsida ni common sana kufikia kiasi zinaekeweka hata na watoto.

ASANTENI
 
Waufungie na ule wimbo wa kwangwaru...
"Weka mate ili utereze uingie pangoni.." pango gani? utajaza mwenyewe
 
Baraza la Sanaa nchini limeufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny aliomshirikisha Diamond likisema unahamasisha masuala yaliyo kinyume na maadili

==================================

Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza ameiambia Mwananchi leo Jumatatu Novemba 12,2018 kuwa wameufungia wimbo huo ambao amemshirikisha Diamond Platnumz na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote.

Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni.

Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.

“Tumesikitishwa sana na msanii mkubwa kama Diamond kushiriki kuimba wimbo usio na maadili kwa kuwa ni msanii mkubwa anayetazamwa kama kioo na jamii,” anasema.

Ameainisha kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.

“Nimesikitishwa sana na maneno yaliyotumika, hivi wanavyoimba hivyo hawaoni kama ndugu zao wanaweza kusikiliza wimbo huo? Maana kutamka hadharani ni sawa na kuongea mbele ya mama yake au watoto wake,” alifanunua.

Mwananchi

Habari zaidi, soma=>BASATA , hamuoni jinsi WCB wanavyowaharibu vijana? - JamiiForums
Ndiyo mtakapojua wakisema "huyu hajasoma sana"
 
hata marekani hua kua radio version ya wimbo na explicit version . Wasanii wetu wawe woke
 
Back
Top Bottom