BASATA yaufungia wimbo wa Mwanza ulioimbwa na msanii Rayvanny kwa kushirikiana na Diamond Platnumz

Unajua sio kila wafanyacho serikali tunapinga ama kukubali... hapa huu wimbo ni haki kabisa kuufungia na hata wenyewe kuwafungia..
 
Kuna lugha ya picha mule? Siku hizi wasafi wamegeuka wachafu ni matusi tu hivi yule boss wao hana aibu mbele ya mama yake anaeshinda nae kutwa nzima mtoto ana sifu ngono tu.
Mama mwenyewe vijana wadogo wanamtoa nyegez
 
Kuna lugha ya picha mule? Siku hizi wasafi wamegeuka wachafu ni matusi tu hivi yule boss wao hana aibu mbele ya mama yake anaeshinda nae kutwa nzima mtoto ana sifu ngono tu.
Yeye na mama ake wote wanashabikia Ngono kupita kiasi
 
Cha Ajabu Toka Umetoka Huo Wimbo Haujawah Kupigwa Wasafi Fm Sijui Walishajua Kitakachotokea Mbeleni
 
BASATA kwanini msiweke sheria kabla msanii hajatoa wimbo upelekwa kwanza BASATA wauhakiki maudhui yake ndiyo wauruhusu kutoa hewani?

Kwanini wanaacha hadi wimbo umesha fika mtaani ndiyo wanaufungia???
Hiyo ni changamoto. Wasanii wako wengi sana na kila siku wanatoa nyimbo mpya nafikiria itawawia vigumu kuhakiki kazi ya kila msanii
 
Jana kuna mdau alileta hii kitu watu wakaponda Carlos the jackal ila wengi tulilaaani sana hizi nyimbo na sio nyegezi bali nyingi za dai hazina maadili kabisa...
 
IMG_5870.jpg

Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) leo Jumatatu, Novemba 12,2018, limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yaliyo kinyume na maadili ya jamii na kwamba usipigwe wala kuchezwa mahali popote.





Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema wanafanya mawasiliano na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni na kuongeza kwamba iwapo wataupiga katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza Novemba 24, 2018 nalo watalifungia.





“Tumesikitishwa sana na msanii mkubwa kama Diamond kushiriki kuimba wimbo usio na maadili kwa kuwa ni msanii mkubwa anayetazamwa kama kioo na jamii. Maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.





“Nimesikitishwa sana na maneno yaliyotumika, hivi wanavyoimba hivyo hawaoni kama ndugu zao wanaweza kusikiliza wimbo huo? Maana kutamka hadharani ni sawa na kuongea mbele ya mama yake au watoto wake,” alisema Mungereza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom