Mpango wa miaka 15 ? nilijuwa huna akili lakini sikudhani u mwepesi kichwani kiasi hiki,kuna MPANGO WA MWAKA 1 pia wa kuwauza nje wote wenye fikra kama zako.Katika mpango wa miaka 15 uliozinduliwa na Kikwete pale Dodoma, moija ya mpango ni kuzipitia upya posho zote na kuziondoa au kuzipunguza inapobidi. Nawashangaa magwanda kuidakia hiyo hoja na kuipiga zumari kama vile ni hoja yao. Hii ni plagiarism at its best. Mnawazuga majuha wenzenu, wengine saa sita kamili.

Acheni kisingizio cha kutenganisha fomu kuwa kigezo cha kuendelea kupokea hizo posho.

Kwani akiisha saini mahudhurio ni lazima achukue pesa yote? Si achukue ile anayoona ni halali yake na kuacha ile anayoiona ni haramu???

CDM ni Unafiki mtupu!
Hiyo cheki utaandika kwa kufanya malipo ya kitu gani na kwa sheria ipi? Na ikirudishwa serikalini itatambuliwa kama malipo kutoka wapi? Na huko serikalini ni wizara ipi au taasisi ipi au idara ipi itahusika kupokea hiyo pesa na itatambuliwa kuwa malipo halali ya kitu gani na kwa sheria ipi? Na Zitto akishalipa hiyo pesa atapewa risiti? Hiyo risiti atapewa na nani???Kwani haiwezekani kurejesha pesa zikishaingia kwenye akaunti yako?

Kama una utashi utaandika cheki kwa Katibu wa Bunge ili arejeshe hiyo pesa serikalini.
Acheni kisingizio cha kutenganisha fomu kuwa kigezo cha kuendelea kupokea hizo posho.
Kwani akiisha saini mahudhurio ni lazima achukue pesa yote? Si achukue ile anayoona ni halali yake na kuacha ile anayoiona ni haramu???
CDM ni Unafiki mtupu!

ila mi naona dhana hapa ni tonge la ugali
Naona itikadi inakusumbua. Pole, better you be realisticReal By-now I trust in Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika and Lissu...and in CCM I do only still remain with Dr. Magufuli and a bit kind of Mwandosya but with some exceptions.
Others use what we call patriotism of their bowels......
Katika mpango wa miaka 15 uliozinduliwa na Kikwete pale Dodoma, moija ya mpango ni kuzipitia upya posho zote na kuziondoa au kuzipunguza inapobidi. Nawashangaa magwanda kuidakia hiyo hoja na kuipiga zumari kama vile ni hoja yao. Hii ni plagiarism at its best. Mnawazuga majuha wenzenu, wengine saa sita kamili.
Katika mpango wa miaka 15 uliozinduliwa na Kikwete pale Dodoma, moija ya mpango ni kuzipitia upya posho zote na kuziondoa au kuzipunguza inapobidi. Nawashangaa magwanda kuidakia hiyo hoja na kuipiga zumari kama vile ni hoja yao. Hii ni plagiarism at its best. Mnawazuga majuha wenzenu, wengine saa sita kamili.
Mara nyingine pia mtatuzuga namna hiyo! Unasema katika mpango wa miaka 15,kwanza sidhani kuna mpango km huo! pia km upo mbona wadau hatujauona?Kwa hiyo kwa kuwa hatujauona basi unatuzuga tu kwamba jambo hilo limo! Na km limo mbona linapingwa na wabunge wake? au Cccm kwa CCM wanapingana!
Hii hoja ni ya Chadema maana wanayo kwenye ilani ya uchaguzi 2010( nina copy -Ilani ya CHADEMA 2010-2015),japo namna ya kuitekeleza ndio inaleta uatata,Lakini kwa kuwa kuna nia,basi itatekelezeka tu!
Hoja iliyopo ni ngumu kwani kwa mfano nikiuliza hivi itakuwaje Mbunge ambaye hakusaini mahudhurio na yupo Bungeni wakati wa kupiga kura je?Kura yake itakuwa halali ama laa na kama sio halali wakati wa kusema ndio na hapana sauti yake huwa inahesabiwa?

Unalipwa posho iwapo tu umehudhuria kikao na kusaini mahudhurio. Kama hujasaini hata kama umehudhuria hulipwi posho ya kikao hicho.
Kwa hiyo kama hutaki kuingiziwa fedha hizi kwenye akaunti yako, unaacha tu kusaini mahudhurio. Mie sijaingiziwa malipo ya posho za vikao toka tarehe 8 Juni mwaka 2011. Nyaraka zangu za malipo yaonyesha 0 katika malipo ya posho za vikao.
Kwa nini habari hii imetoka sasa? Kwanza mimi sijaiona kwenye magazeti. Lakini pili ni lazima habari kama hii imekuwa leaked kimkakati ili kuonyesha kuwa chadema sio chama makini. Hivyo inawezekana kuna watu wanataka kuweka mjadala huu kama sehemu ya propaganda za kampeni huko Igunga nk.
Wabunge wa chadema ni wanafiki? Hapana. Wabunge wa chadema wamechukua hatua ya kuandika kwa Spika kwamba fomu za mahudhurio na fomu za posho ziwe mbili tofauti. Ofisi ya Spika haijafanya hivyo.
Suala langu lilikuwa personal kidogo. Wabunge wa ccm walianza kunishambulia mimi binafsi na hivyo nikachukua maamuzi ambayo yanawaziba mdomo moja kwa moja.
Mkakati wa chama ni kusaini daftari la mahudhurio tofauti na daftari la posho.
Mengine ni tafsiri za watu kulingana na mapenzi au chuki zao kwa Zitto au chama changu.
Hongera Zitto. Katika mapambano si lazima wote muanza kwa wakati mmoja wengne watajiunga baadae. Naamini huo ni mwanzo mzur kwa Zito, muda si mrefu wengne wataunga mkono kwa vitendo isipokuwa Shibuda. Kila la kher kamanda Zito.
Katika mpango wa miaka 15 uliozinduliwa na Kikwete pale Dodoma, moija ya mpango ni kuzipitia upya posho zote na kuziondoa au kuzipunguza inapobidi. Nawashangaa magwanda kuidakia hiyo hoja na kuipiga zumari kama vile ni hoja yao. Hii ni plagiarism at its best. Mnawazuga majuha wenzenu, wengine saa sita kamili.
Kwanza kabisa mapenda kunukuu maneno ya Mh. Zitto. Kisha ningependa kumuuliza maswali kwa ufahamu zaidi.
Hebu tupe ufafanuzi kwa mambo yafuatayo.
- Napenda nifafanue masuala kadhaa hapa.
Moja, sisi kama Kambi ya Upinzani inayoundwa na CHADEMA tulikwishaamua kwamba posho za vikao sio stahili sahihi kwa Mbunge. Mnadhimu Mkuu wa Kambi alikwishaandika kwa Spika wa Bunge kutaka kutenganisha fomu za mahudhurio na fomu za posho. Mbunge wenje pia katika moja ya michango yake alisema Bunge litengenishe fomu hizi mbili.
Kuhusiana na mimi kama an indivual MP, nilipewa kazi na chama kama Waziri kivuli Fedha na tangazo la posho alilitoa Naibu wangu ndugu christina Lissu. Mie nikalitolea ufafanuzi kwa vyombo vya habari. Wabunge wa CCM wakaanza kunishambulia na kusema ni unafiki kwamba ninatangaza posho zifutwe ilhali nazichukua. Nikamwandikia Spika barua kuwa posho zangu ziende kwenye charity org jimboni kwangu. Hili nalo likaonekana kama ni unafiki pia. Nikaamua kuzikataa kabisa. Hivyo toka tarehe 8 Juni mimi sipokei posho ya vikao. Njia ninayotumia ni kutosaini mahudhurio Bungeni ili wasipate sababu ya kunilipa.
Sasa kuna mchangiaji hapa kasema usiposaini ndani ya siku tatu unaadhibiwa. Kanuni inasema Mbunge asipohudhuria MIKUTANO mitatu ya Bunge anakuwa amejifukuza ubunge. Tutofautishe mikutano na VIKAO. Kikao ni kila siku na mkutano ni session nzima, mfano session iliyopita ilikuwa ni mkutano wa 4 wa Bunge nk.
Sasa, ikitokea sitasaini pia katika mkutano wa 5 na wa 6 wanaweza kuanza mchakato wa kunifukuza Ubunge. Lakini je mchakato huo utategemea karatasi za mahudhurio tu? Kwa mfano, nikiwa Bungeni ninauliza swali au kuchangia hoja, hansard inarekodi kuwa nilikuwepo Bungeni. Karatasi ya mahudhurio inaonyesha sikuwepo Bungeni. Audio na video records zinaonyesha nilikuwepo Bungeni, watanifukuza kwa vigezo vipi?
Katika harakati lazima ni lazima kuchallenge rules ili zibadilike. Nadhani katika hili tutafanikiwa.
Hivyo, wabunge wa chadema sio wanafiki kwani tayari wameandika rasmi kutaka fomu tofauti za kujaza mahudhurio. Pili, Zitto hasaini kama njia ya kutoa changamoto kwa rules. Lakini pia ninaamini kwa dhati kabisa kwamba posho ya kikao (sitting allowance) sio stahili halali (legitimate?)Kwa mbunge anayelipwa mshahara kwa kazi ile ya kukaa na kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi.
Nadhani waliowengi wamekuelewa kutokana na ufafanuzi wako. Labda kwa kuongezea hapo nitoe pia maelezo kuwa hata Mh. Mbowe alishalitolea ufafanuzi jambo hili tena kwa umahiri mkubwa sana. Katika kumbukumbu zangu Mh. Mbowe alisema, Swala si kufuta POSHO zipo zilizohalali kama Per DieM lakini siyo SITTING Allowance. Pia likazuka suala la Spika MAKINDA kukemea wabunge wote wanaokataa posho hizo kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu ni kukiuka kanuni za Bunge. Swali linakuja Nani aliyewachanganya Wabunge ni Spika au Mh. Zitto! Jambo la msingi ilikuwa ni kufuta posho zote kuanzia kwa Wabunge hadi Serikalini rejea maneno ya WAZIRI Mkuu Posho zisizo za lazima kufutwa, swali je hayo yametekelezwa? Kwa mantiki hiyo endapo Chadema wangezikataa ina maana hata baadhi ya stahiki zao zilizo halali wangezikosa kwa sababu form za kusaini posho hizo hazikutenganishwa. Ingekuwa ni halali kwa wananchi kuwalaumu Chadema ikiwa tu form hizo zingekuwa zimetenganishwa kisha wakaamua kuzichukua zote, lakini kwa hili hatuwezi kuwatupia lawama chadema. Swali langu kwa Mh. Zitto. Unatuambia nini wananchi kuhusu Posho yako kupelekwa Jimboni kwako, je zimekwishapelekwa? Ikiwa zitapelekwa je utasaini form hizo? Sasa kutakuwa na tofautigani na Wabunge waliozichukua kisha wakaenda majimboni mwao na kuwasaidia wapigakura wao? Bado ni kizungumkuti kwani inaonekana Serikali haijawa tayari kutekeleza adhima hiyo ya kufuta posho legelege. Ni mawazo tu yenye mlengo wa kati.
Kama Mwenyekiti wa Chama na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbowe, ameshindwa kuonyesha uongozi na kuendekeza maslahi yake binafsi, hawa Wabunge wengine wataweza vipi??akina Sugu, Wenje, na Lema kwa uchache wataziacha vip? sio rahisi kama unavyodhani, inahitaji sana kujitoa na kujikana kwa dhati...
Zitto anastahili sana pongezi kwa hili, kaonyesha kwa vitendo kuwa yupo juu ya maslahi yake binafsi, ata kama Wabunge wengine wa Chadema pamoja na wala CCM hawatakuunga mkono kwa muda mrefu ujao, Watanzania wanajua...