Barua: Zitto akataa posho za vikao

We need more info concerning this issue because it is not clear up to now.

napita tu

Majuha ni wale wanaoshabikia mafisadi wanaoifukarisha nchi hii.Kwa mtu yoyote anayeunga mkono ufisadi unaofanywa na watawala wa nchi hii lazima awe na mtindio wa ubongo, hata ni hizo posho mnazolipwa na Nape jamani lakini kuweni wazalendo.

Mkuu Seal Team,
Naona hujamsoma Vizuri Mhe. Zitto na kumuelewa. Zitto anasema mwanzoni alipendekeza Posho zake zipelekwe kusaidia taasisi ya hisani Mkoani Kigoma IKIWA TU ni lazima kusaini fomu za mahudhurio ili zitolewe. Kuona hivyo, watu hasa Wabunge wa CCM wakadai ni unafiki. Hivyo mhe. Zitto akaamua bora asisaini kabisa hizo fomu na pesa zisitolewe kwenda kwake ama kwenye taasisi aliyoilenga isaidiwe.

Unalipwa posho iwapo tu umehudhuria kikao na kusaini mahudhurio. Kama hujasaini hata kama umehudhuria hulipwi posho ya kikao hicho.
Kwa hiyo kama hutaki kuingiziwa fedha hizi kwenye akaunti yako, unaacha tu kusaini mahudhurio. Mie sijaingiziwa malipo ya posho za vikao toka tarehe 8 Juni mwaka 2011. Nyaraka zangu za malipo yaonyesha 0 katika malipo ya posho za vikao.
Kwa nini habari hii imetoka sasa? Kwanza mimi sijaiona kwenye magazeti. Lakini pili ni lazima habari kama hii imekuwa leaked kimkakati ili kuonyesha kuwa chadema sio chama makini. Hivyo inawezekana kuna watu wanataka kuweka mjadala huu kama sehemu ya propaganda za kampeni huko Igunga nk.
Wabunge wa chadema ni wanafiki? Hapana. Wabunge wa chadema wamechukua hatua ya kuandika kwa Spika kwamba fomu za mahudhurio na fomu za posho ziwe mbili tofauti. Ofisi ya Spika haijafanya hivyo.
Suala langu lilikuwa personal kidogo. Wabunge wa ccm walianza kunishambulia mimi binafsi na hivyo nikachukua maamuzi ambayo yanawaziba mdomo moja kwa moja.
Mkakati wa chama ni kusaini daftari la mahudhurio tofauti na daftari la posho.
Mengine ni tafsiri za watu kulingana na mapenzi au chuki zao kwa Zitto au chama changu.

Nadhani hujaelewa kuwa ukisaini kitabu cha mahudhurio unaingiziwa pesa katika akaunti yako ya benki sio unapokelea dirishani - kwa taarifa tu

Kwani haiwezekani kurejesha pesa zikishaingia kwenye akaunti yako?
Kama una utashi utaandika cheki kwa Katibu wa Bunge ili arejeshe hiyo pesa serikalini.

Yaan umeyanukuu maelezo ya Zitto bila kuyasoma??..haya ni matatizo kwelikwelii...

Real By-now I trust in Dr. Slaa, Mbowe, Mnyika and Lissu...and in CCM I do only still remain with Dr. Magufuli and a bit kind of Mwandosya but with some exceptions.

Others use what we call patriotism of their bowels......

wasipochukua wakati they are still entittled itawafanya weak mbele za wenzao

Nadhani suala hili linahitaji umakini zaidi, Kwani hata kama mheshimiwa Zito hizo hela hakuzichukua sidhani kama hawa magamba watafanya matumizi sahihi ya kuachwa kwa hizo hela!! Ni bora utaratibu ukapangwa na maatumizi yakafahamika ambayo yataonekana na Mbunge husika anaweza kuona matunda ya Maamuzi yake ya kuacha posho. Je Kwa hizi hela zilizobaki je tunaweza kujua Kama zitatumika kwa kitu gani? Je wakienda kuhonga watu Igunga huoni upinzani tutakuwa tumejimaliza wenyewe?

Asante sana Mhe. Zitto kwa maelezo mazuri juu ya hujuma hii ya kuwachafua kwa makusudi endeleeni na harakati na ikibidi wabunge wote wa chadema mkutano ujao basi mgome kusaini fomu za mahudhurio ili kushinikiza harakati za kuzitenganisha na fomu za posho hope hii itaspeed up mchakato mzima

Na hii itafanyika baada ya miaka kumi na tano, au siyo?

we kweli huna akiri iweje usaini alafu uchukue nusu,sa si hz nyngne watakula hao na hamna namna unaweza kuwashutumu.,maana inaonekana ulizichukua.acha ushamba!

Muungwana ni matendo yake na shukuru nimeuona uungwana wako. Sasa na kwazika kidogo, nisaidie tena hiki (kama niko sahihi) ni kipindi chako cha pili katika bunge, sawa? Ni lini suala hili la posho za kikao uliliona si sawa, na ulichukuwa hatua gani (kama ni kipindi cha huko nyuma), kwanini baada ya kushambuliwa na wa bunge wa ccm na kuamu kuchukua hatua, hii hatua uliyoichukuwa haikuwezekana kuchukuliwa na wengi wa wabunge wa cdm (achana na shibuda yeye ni pandikizi hilo halina ubishi and his a failure kwa vile imejulikana hivyo)? Uliwashirikisha wa kakataa au ulimua mwenyewe, na kwa mantiki hiyo je? cdm hamna team work katika masuala fulani fulani?

Yaan umeyanukuu maelezo ya Zitto bila kuyasoma??..haya ni matatizo kwelikwelii...
Yawezekana wewe ndiye hukunielewa lakini nina imani kabisa Mh. Zitto atakuwa amenielewa, si haba akaja pia kwa uelewa zaidi

Kuna watu mnapenda kulinda status quo ya umasikini wa walio wengi na utajiri wa walio wachache...siku itakapofika wenye nchi yao wakaanza kuidai..sijui mtakimbilia Algeria kama familia ya Ghadafi au mtahukumiwa kwa kunyongwa na wananchi wenye hasira! (sorry for these words-mnauzi sana..mnaposhindwa ku-appreciate umasikini wa watanzania wenzetu simply because you got vested interests in the ruling clique!). Kila kitu kitu mnakifanya politics za simba na yanga!

And for your information, kuna tuliopanga foleni tukampa kura Kikwete....and regretably he has simply become a spectacular failure and disappointment. So usione wote tunamponda, Yes, Tunaomponda JK kwamba tunamchukia..its simply because the man HAS become a baggage he got no clue on what he should do as the Commander Inchief of our United Republic.

Masanja

Suala hili ni utekelezaji wa ilani ya chama ya mwaka 2010. Kabla ya hapo hatukuwa na suala hili na hivyo halikuhitaji utekelezaji. Kuniuliza zamani ilikuwaje nakuwa sina jibu. Toka mwaka 2005 mpaka April 2011 nilikuwa nachukua posho hizi. Sasa kwa kuwa tunatekeleza ilani ya chama sichukui.
Lakini, hivi ukiwa mlevi kwa miaka kumi. Ukaacha ulevi mwaka wa 11, utaulizwa kwa nini umeacha mwaka huu na sio mwaka jana?

Taarifa za nyongeza ni kuwa posho zote kuanzia sitting allowance , per diem na nyinginezo huwa zinalipwa kila ijumaa kwenye Account za wabunge , na huwa zinachanganywa pamoja na kuingizwa kwenye account husika ya Mbunge .

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…