Barua za Spika Ndugai kuomba mchango wa 200m ilikuwa ni kwaajili ya Wabunge au Taifa stars?

Hata hivyo bunge haikuwa sawa kuomba pesa kwa Bodi ya utalii wakati bunge Lima kasma yake na bodi y utalii ina kasma yake Kwani hiyo bodi ya utalii ingetoa katika bajeti gani hizo pesa. Hivi kwa utaratibu huo huyo Mkurugenzi akiwa na makandokando kwenye kukagua hesabu zake hilo bunge litapendekeza achuliwe hatua wakati wanamuomba pesa.
 
Vita ni vita, natulia pembeni na juisi ya ukwaju, tusubiri mwisho wa picha
 
Ukiisoma hiyo barua utagundua kuwa wabunge 65 walitaka kuhudhuria cairo wakachanga pesa, sasa pesa ya kuwagharamia hao 65 huko cairo kutoka kwenye michango wiliochanga ikapelea kiasi cha 200mil ndo sasa kiongozi wao ametembeza bakuli sehemu mbali mbali kuomba michango ili kupata hiyo 200mil iliyopelea, utalii huko kaomba 25, na kwingine pia atakua kaomba etc, etc, etc.

Lengo
ni kugharamia wabunge na sio taifa stars
 
Hahaha ulisahau kuuliza na mahaba ya makonda kwa timu ya taofa yameanza lini na kwanini?! Sijaona akiiombea KMC pesa, na hajaomba ruhusa kwa mzee wake kwenda Rwanda.
Tunafahamu hawezi omba ruhusa kwa Jafo, ataomba kwa mzee wake.
 
Kweli kuna ka ufisadi kapo hapo, lakini kwenye hilo ngoja nimtetee Ndugai.
Kwa barua hiyo ni wazi fedha hizo ziliombwa kwa ajili ya kuwasaidia wabunge hao katika safari ya Misri na wala hazikuhusiana na kupelekwa Stars, huko ni kukurupuka kwa Makonda ambaye haombagi ushauri kabla ya kusema hayo.
Katika fedha hizi labda tuhoji kwa namna nyingine mfano kuwaombea fedha za udhamini wabunge kwenye taasisi ya umma kwa kutumia madaraka ya kibunge. Jee kesho na kesho kutwa bunge linaweza kuihoji taasisi hiyo ikikuta kuna matumizi mabaya ya fedha?
 
Heche anasema walijitegemea kisafari, sasa zimetumika kwa lipi?
 
Back
Top Bottom